Hizi ndiyo fedha watakazolipwa Washindi wa Kombe la Dunia 2022

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,350
8,031
1669269645328.png
 
Baada ya kuwa mabingwa wa Kombe la Dunia, bingwa anakabidhiwa kiasi hicho cha fedha sawa na Dola Milioni 42, Ufaransa (wa pili) anapata Dola Milioni 30 (Tsh. Bilioni 70), wa tatu na wanne, Croatia Dola Milioni 27 (Tsh. Bilioni 63), Morocco Dola Milioni 25 (Tsh. Bilioni 58).

Kila timu iliyofika Robo Fainali Dola Milioni 17 (Tsh. Bilioni 39.5), iliyofika 16 Bora Dola Milioni 13 (Tsh. Bilioni 30), iliyoishia Hatua ya Makundi Dola Bilioni 9 (Tsh. Bilioni 21).
 
Unamaanisha waliofikia makundi watalipwa zaidi ya alie chukua ubingwa!!!!!!??

Hakikisha ulichoandika halafu karekebishe
 
Unamaanisha waliofikia makundi watalipwa zaidi ya alie chukua ubingwa!!!!!!??

Hakikisha ulichoandika halafu karekebishe
bro..aloshnda atapitwaje mtonyo asee!?il uwe bingwa lazma upte hatua zote kumbuka kla hatua unapata mgawo..kwa hyo Argentina amebeba hela kweny kila hatua
 
Pesa nyingi sana, FIFA wanavyazo gani vya mapato? Wana hela nyingi hivi.
Ndio wenye haki miliki ya kuuza maonyesho ya Tv , kila mechi moja ya kombe la dunia wanaiuza kwa Dola za Marekani 500,000 ( sawa na TSh. Milioni 1,175 au 1.175b ) kwa kituo kimoja cha Tv , sasa jiulize vituo vipo vingapi vya Tv duniani na mechi zipo kama sikosei 64, pia wanapata pesa nyingi kupitia udhamini /Sponsorship deals na mauzo ya vifaa vya michezo.
 
Asante kwa ufafanuzi.
Nilikua sifahamu lakini sasa nimeelewa.
Hakika kwenye mpira kuna pesa.
 
Back
Top Bottom