Hizi ndiyo Amri 10 za Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndiyo Amri 10 za Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lunyungu, Feb 5, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Usiwe mwongo kama KARAMAGI

  Mwizi kama BALALI

  Mbishi kama ZITTO

  Makelele mengi yasiyo na maana kama MAKAMBA

  Mbabe kama SITTA

  Usihukumu kama MUDHIHIRI

  Usiue kama DITOPILE

  Usidandie hoja kama MREMA

  Jali masilahi ya nchi kama Dr SLAA na wapinzani

  Usichecheke ovyo na kutoa ahadi hewa kama KIKWETE
   
 2. S

  Siao Member

  #2
  Feb 5, 2008
  Joined: Jan 4, 2008
  Messages: 96
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  irritating kwa kumtusi kaka Zitto.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Zitto kuwa mbishi mimi sioni kama wamemtusi .Ni kweli ni mbishi ambaye anataka kuoa usawa unatendeka . Zitto huwezi kumhamisha kirahisi kwenye issue ya manufaa kwa Taifa eti kwa kumkemea .Ndiyo wanamshindwa wanaamua kutumia kanuni ambazo hazipo . Zitto endelea kubisha kwa point na hilo sote twalijua hubishi kwa kuwa una nguvu na mdomo unabisha kwa logic.
   
 4. K

  Kalamu JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2008
  Joined: Nov 26, 2006
  Messages: 874
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lunyungu:
  Amri ya Malicela mbona haionekani hapo, au ni dead wood?
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kalamu kwa kuwa ni amri za Tanzania na sisi ndiyo watanzania basi ongeza ya Malecela hapo
   
 6. N

  NakuliliaTanzania JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 560
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  tehe tehe tehe!
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 6, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Usiwe fisadi kama MKAPA

  Usijione wewe ni wa maana sana kama SITTA

  Utetee nchi yako kwa uwezo na nguvu zako zote kama SLAA na ZITTO

  Usiwe msanii wa kutoa ahadi hewa na kutoa vitisho visivyokuwa na vitendo na kukenuakenua hovyo hovyo kama KIKWETE

  Usibwabwaje hewa kama MAKAMBA

  Useme ukweli ili kutetea maslahi ya nchi yako bila woga kama BUTIKU

  Usiwe muongo na kutoyajali maslahi ya nchi yako kama KARAMAGI

  Usiwe mbaibashaji na kutaka kuficha madhambi yako kama LOWASSA

  Usiwe tapeli na muongo wa kutetea kitu usichokijua kama MZINDAKAYA na MKONO (Walitetea BoT kumbe wamechukua mabilioni ya pesa toka BoT)

  Uwe muadilifu na kuwapenda Watanzania wenzio na siku zote kuweka maslahi ya Tanzania mbele kama NYERERE
   
Loading...