Hizi ndio nchi 10 pekee Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya Serikali.

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Messages
433
Points
500

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2016
433 500
Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
 1. Botswana
 2. Cape Verde
 3. Eritrea
 4. Mauritius
 5. Mozambique
 6. Namibia
 7. Sao Tome and Principe
 8. Senegal
 9. South Africa
 10. Tanzania
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
11,725
Points
2,000

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
11,725 2,000

Mkuu mwaka 1964 kulikuwa na mapinduzi ambayo kwa bahati nzuri yalizimwa mapema, vinginevyo hakuna ajuaye madhara yake yangekuwa vipi kwa vizazi vilivyofuatia. Jeshi liliasi ikabidi waingereza warudi kuokoa mambo.
 
Rockefeller

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Messages
433
Points
500

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2016
433 500
Mkuu mwaka 1964 kulikuwa na mapinduzi ambayo kwa bahati nzuri yalizimwa mapema, vinginevyo hakuna ajuaye madhara yake yangekuwa vipi kwa vizazi vilivyofuatia. Jeshi liliasi ikabidi waingereza warudi kuokoa mambo.
Nakubali mkuu ila kutokana na source yangu TZ haikuwekwa kutokana kua waasi wa kijeshi hawaku state kwamba walitaka serikali itolewe madarakani bali walidai maslai yao binafsi. Hatuwezi hata kusema ni jaribio lilishindikana.
 
mkuu wa kijiji

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2017
Messages
593
Points
1,000

mkuu wa kijiji

JF-Expert Member
Joined Apr 7, 2017
593 1,000
Kuna Nchi nyingi hazijawahi kupinduliwa japo yalikuwepo majaribio ya mapinduzi.
South Africa
Namia
Zambia
Malawi
Mozambique
Tanzania
Angola
Lesotho
Eswatin etc
Na ikumbukwe Nchi nyingi Afrika ya magharibi zinafahamu ladha ya mapinduzi ya kijeshi,Kama
Burkanabe
Niger
Nigeria
Mauritania
Senegal
Ivory Coast
Siyeralone
Liberia
Equatorial Guines etc
 
Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Messages
7,263
Points
2,000

Titicomb

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2012
7,263 2,000
Mkuu mwaka 1964 kulikuwa na mapinduzi ambayo kwa bahati nzuri yalizimwa mapema, vinginevyo hakuna ajuaye madhara yake yangekuwa vipi kwa vizazi vilivyofuatia. Jeshi liliasi ikabidi waingereza warudi kuokoa mambo.
Yale hayakuwa mapinduzi ya utawala wa serikali. It was not a 'COUP DETAT'.

Ule ulikuwa mgomo au uasi wa baadhi ya wanajeshi kudai maslahi flani. It was a 'MUTINY'.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
5,919
Points
2,000

elvischirwa

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
5,919 2,000
Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
 1. Botswana
 2. Cape Verde
 3. Eritrea
 4. Mauritius
 5. Mozambique
 6. Namibia
 7. Sao Tome and Principe
 8. Senegal
 9. South Africa
 10. Tanzania
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
Hauko sahihi, tuambie Zambia na Malawi mapinduzi yalifanyika mwaka gani.
Shelisheli na Swaziland mapinduzi yalifanyika lini!
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
21,320
Points
2,000

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
21,320 2,000
Sababu kuu ziko Kama ifuatavyo Kuna nchi Zina utawala wa majimbo.Ambazo Zina nguvu kuliko serikali kuu kwenye Mambo mengi.Sasa upindue ili umpindue Nani uvamie Jimbo la mwingine au?
Mfano Ni south Afrika.

Pili Ni composition ya makabila mengi .Nchi zenye makabila makubwa machache makubwa kutwangana kwao kawaida.Nchi ikiwa na makabila mengi uasi unakuwa mgumu mno kuupanga .

Tatu uwepo wa utitiri wa dini nyingi zenye Imani tofauti tofauti.Kuna faida kubwa Sana nchi kuwa na dini nyingi na madhehebu mengi utitiri yenye Imani tofauti tofauti.Kupanga mapinduzi huwa Ni kugumu mno sababu ya tofauti kubwa za kiimani.Nchi mfano zenye dini moja au mbili tu mfano rahisi mno kupanga mapinduzi.nchi Kama somalia ,nchi Kama Rwanda iliwezekana sababu ya tatizo Hilo Hilo mauaji ya kimbari yalikuwa rahisi kupangwa ndani ya kanisa Katoliki sababu ndio wako majority ndio dini ya wanyarwanda wengi ukiunganisha na nch ihiyo kuwa na makabila makubwa mawili tu ya wahutu na watusi unaona kabisa ilivyo rahisi kufanya mapinduzi kwa kutumia muundo mbinu wa kanisa Katoliki au wa kikabila wa kitusi au kihutu.Ukiwa na dini nyingi zenye imani tofauti husaidia mfano waislamu wa siasa Kali wakilianzisha waislamu wenye msimamo wa wastani wanapinga,walokole wakilianzisha wakatoliki hawaungi mkono,wakatoliki wakilianzisha wasabato wanalikataa nk nk kwa hiyo amani inadhibitiwa kwa kuruhusu dini ziwe nyingi iwezekenavyo na zenye Imani tofauti tofauti.Hapa ndipo wanasiasa husema dini Zina mchango mkubwa katika amani ya nchi.Nchi zenye dini moja au mbili kubwa mapinduzi marahisi kuyapanga.Nchi za Latin America Ni moja ya mifano na nchi za kiarabu.Nchi Kama Iran nk .

Nne Tatizo la Ardhi huchangia Sana.Ajira kubwa kwa watu wengi Ni kwenye kilmo.Watu wanachohitaji kwanza Ni uhakika wa chakula.Sasa watu wengi Kama Ni vigumu kupata ardhi Vita yaweza fumuka na mapinduzi kirahisi.Mapinduzi ya Urusi yalitokea sababu ya ardhi kuhodhiwa na wachache na kuacha umati ukiwa hauna ardhi na haujui uishije.Tanzania watu walio wengi Wana uhakika wa chakula akishashiba karidhika hataki Shari.

Tano Ni sababu ya gharama za kuendesha mapinduzi.Wapinduaji huhitaji support kubwa ya fedha na vifaa vya kivita huo ni mtihani mkubwa.Hivyo unakuta Hakuna mwenye hamu ya mapinduzi.

Sita Ni aina ya watu walioko katika nchi.Kuna nchi unakuta watu wao Sio washari by nature mfano Tanzania majority Sio watu wa Shari na hawapendi Shari.Hivyo kupata uungwaji mkono ukianzisha Shari SI rahisi kupata support.Mfano mikoa ya Pwani ,mikoa ya katikati ya nchi makabila makubwa Kama wasukuma ,wanyamwezi,wanyakyusa ,wangoni,wamatengo,wafipa,waluguru,wapogoro,wazanzibari weusi. Hivyo mwanzisha mapinduzi lazima akwae kisiki kupata support Sio rahisi.

Saba Ni kiwango Cha mwamko wa kupenda madaraka na vyeo kwa raia na wanajeshi .Kuna wanajeshi na raia nchi unakuta kila Askari au raia mfano anaota kuwa genetali wa Jeshi.Sasa unakuta vikoplo aau raia vinapindua nchi kila kukicha vijipe vyeo vya generali au vishike nchi kwa mapinduzi .Tanzania mfano watu walio wengi hawako interested kabisa na vyeo vya kisiasa.Ni wachache ndio huvitolea macho

.Nane Ni kiwango cha kuridhika cha watu watu kuridhika na woichonacho.Wakishajiridhikia hawahitaji chochote.Kuna siku kiongozi mmoja wa Upinzani alipita mtaani alisema CCM kumejaa mafisadi CCM inabidi iondolewe madarakani.Kuna Wazee walikuwa wakicheza bao mmoja akamjibu hao mafisadi walichukua pesa ya mama yako? Yanakuhusu Nini? Wazee wengine wakaanza kuunga mkono kauli ya Mzee mwenzao na kusisitiza kumhoji hao mafisadi wamechukua pesa ya ya mama yako?.Wakamwambia Tuondokee hapa na porojo zako.Akaondoka mnyonge .Wazee wa watu wamejilia kipande Cha mhogo na fungu la dagaa la shilingi Mia mbili wameridhika zao!!! Kupindua nchi ya watu walioridhika na walichonacho Sio kazi rahisi.
 
Rockefeller

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Messages
433
Points
500

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2016
433 500
Kuna Nchi nyingi hazijawahi kupinduliwa japo yalikuwepo majaribio ya mapinduzi.
South Africa
Namia
Zambia
Malawi
Mozambique
Tanzania
Angola
Lesotho
Eswatin etc
Na ikumbukwe Nchi nyingi Afrika ya magharibi zinafahamu ladha ya mapinduzi ya kijeshi,Kama
Burkanabe
Niger
Nigeria
Mauritania
Senegal
Ivory Coast
Siyeralone
Liberia
Equatorial Guines etc
Kwenye list yangu nilisema nchi zilizopinduliwa au jaribio la mapinduzi.
 
Rockefeller

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Messages
433
Points
500

Rockefeller

JF-Expert Member
Joined Nov 21, 2016
433 500
Sababu kuu ziko Kama ifuatavyo Kuna nchi Zina utawala wa majimbo.Ambazo Zina nguvu kuliko serikali kuu kwenye Mambo mengi.Sasa upindue ili umpindue Nani uvamie Jimbo la mwingine au? Mfano Ni south Afrika.Pili Ni composition ya makabila mengi .Nchi zenye makabila makubwa machache makubwa kutwangana kwao kawaida.Nchi ikiwa na makabila mengi uasi unakuwa mgumu mno kuupanga .Tatu uwepo wa utitiri wa dini nyingi zenye Imani tofauti tofauti.Kuna faida kubwa Sana nchi kuwa na dini nyingi na madhehebu mengi utitiri yenye Imani tofauti tofauti.Kupanga mapinduzi huwa Ni kugumu mno sababu ya tofauti kubwa za kiimani.Nchi mfano zenye dini moja au mbili tu mfano rahisi mno kupanga mapinduzi.nchi Kama somalia ,nchi Kama Rwanda iliwezekana sababu ya tatizo Hilo Hilo mauaji ya kimbari yalikuwa rahisi kupangwa ndani ya kanisa Katoliki sababu ndio wako majority na nguvu ndio dini ya wanyarwanda wengi ukiunganisha na nchi kuwa na makabila makubwa mawili tu ya wahutu na watusi unaona kabisa ilivyo rahisi kufanya mapinduzi kwa kutumia muundo mbinu wa kanisa Katoliki au was kikabila wa kitusi au kihutu.Ukiwa na dini nyingi zenye imani tofauti husaidia mfano waislamu was siasa Kali wakilianzisha waislamu wenye msimamo wa wastani wanapinga,walokole wakilianzisha wakatoliki hawaungi mkono,wakatoliki wakilianzisha wasabato wanalikataa nk nk kea hiyo amani inadhibitiwa kwa kuruhusu dini ziwe nyingi iwezekenavyo na zenye Imani tofauti tofauti.Hapa ndipo wanasiasa husema dini Zina mchango mkubwa katika amani ya nchi.Nchi zenye dini moja au mbili kubwa mapinduzi marahisi kuyapanga.Nchi za Latin America Ni moja ya mifano na nchi za kiarabu.Nchi Kama Iran nk .Nne Tatizo la Ardhi huchangia Sana.Ajira kubwa kwa watu wengi Ni kwenye kilmo.Watu wanachohitaji kwanza Ni uhakika wa chakula.Sasa watu wengi Kama Ni vigumu kupata ardhi Vita yaweza fumuka na mapinduzi kirahisi.Mapinduzi ya Urusi yalitokea sababu ya ardhi kuhodhiwa na wachache na kuacha umati ukiwa hauna ardhi na haujui uishije.Tanzania watu walio wengi Wana uhakika wa chakula akishashiba karidhika hataki Shari.Lingine Ni sababu ya gharama za kuendesha mapinduzi.Wapinduaji huhitaji support kubwa ya fedha na vifaa vya kivita huo ni mtihani mkubwa.Hivyo unakuta Hakuna mwenye hamu ya mapinduzi.Sita Ni aina ya watu walio katika nchi.Kuna nchi unakuta watu wao Sio washari by nature mfano Tanzania majority Sio watu wa Shari na hawapendi Shari.Hivyo kupata uungwaji mkono ukianzisha Shari SI rahisi kupata support.Mfano mikoa ya Pwani ,mikoa ya katikati ya nchi makabila makubwa Kama wasukuma ,wanyamwezi,wanyakyusa ,wangoni,wamatengo,wafipa,waluguru,wapogoro,wazanzibari weusi hivyo mwanzisha mapinduzi lazima akwae kisiki kupata support Sio rahisi.Saba Ni kiwango Cha mwamko wa kupenda madaraka na vyeo kwa raia na wanajeshi .Kuna wanajeshi na raia nchi unakuta kila Askari au raia mfano anaota kuwa genetali wa Jeshi.Sasa unakuta vikoplo vinapindua nchi kila kukicha vijipe vyeo vya generali.Na wananchi Wana uroho wa vyeo hasa.Tanzania mfano watu walio wengi hawako interested kabisa na vyeo vya kisiasa.Ni wachache ndio huvitolea macho.Kingine Ni watu kuridhika na woichonacho.Wakishajiridhikia hawahitaji chochote.Kuna siku kiongozi mmoja wa Upinzani alipita mtaani alisema CCM kumejaa mafisadi CCM inabidi iondolewe madarakani.Wazee walikuwa wakicheza bao mmoja akamjibu hao mafisadi walichukua pesa ya mama yako? Yanakuhusu Nini? Wazee wengine wakaanza kuunga mkono kauli ya Mzee mwenzao na kusisitiza kumhoji wamechukua ya mama yako.Tuondokee hapa na porojo zako.Akaondoka mnyonge .Wazee wa watu wamejilia kipande Cha mhogo na fungu la dagaa la Mia mbili wameridhika zao!!! Kupindua nchi ya watu walioridhika na walichonacho Sio kazi rahisi.
Umeeleza vizuri mkuu
 
Careem

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Messages
19,032
Points
2,000

Careem

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2013
19,032 2,000
Habari za wakati wanajamvi,
Leo nimekuja kwenu na orodha ya nchi 10 Afrika ambazo hazijawahi kuwa na mapinduzi ya serikali ya aina yoyote. Nchi nyingi za kiafrika baada ya uhuru ziliangukia katika wimbi kubwa la mapinduzi ya serikali zilizoachwa na wakoloni, kwa kipindi hicho sababu kuu za mapinduzi hayo ilikua ni uchu na tamaa za madaraka walizokua nazo viongozi wa mapinduzi au wadau wa mapinduzi, tuliona viongozi wengi waliofanya mapinduzi na mwishowe kuharibu utaratibu na kuhujumu uchumi na mali za nchi mfano Idd Amin na Mobutu, nchi karibu zote za Africa zilikumbwa na hili tatizo isipokua zifuatazo:-
 1. Botswana
 2. Cape Verde
 3. Eritrea
 4. Mauritius
 5. Mozambique
 6. Namibia
 7. Sao Tome and Principe
 8. Senegal
 9. South Africa
 10. Tanzania
Swali: Je unadhani kutokua na mapinduzi ya kiserikali ni alama ya ukomavu wa kisiasa, au kukosa watu wenye maono tofauti yenye ushawishi, au woga?
BONUS: Kenya ndio nchi pekee Afrika yenye jina linaloanza na K.
NAWASILISHA.
Uganda ndio nchi pekee inayoanzia na U
Rwanda ndio nchi pekee inayoanzia na R
 
Forum statistics

Threads 1,390,783
Members 528,265
Posts 34,061,793
Top