Hizi ndio mbinu anazutumia Mwajiri wako kuhakikisha unaendelea kuwa Mtumwa wake

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,465
2,000
Ajira ni kitu kizuri sana, maana kupitia ajira ndio tunapata watu wa kutufanyia kazi mbalimbali na pia kutupatia huduma mbalimbali. Na kuna kipindi ajira ilikuwa kitu muhimu sana kiasi kwamba aliyekuwa na ajira alionekana kuyashinda maisha. Lakini nyakati hizo zimepita sasa na tumeingia kwenye kipindi ambacho ajira zimekuwa na changamoto kubwa sana.

Kwanza nafasi za ajira zimekuwa chache kuliko idadi ya wanaozihitaji hivyo kufanya idadi ya wasiokuwa na ajira kuwa kubwa.

Na pili, hata waliopo kwenye ajira hawaridhishwi na ajira zao kwa maana kwamba wanajikuta wanafanya kazi miaka mingi lakini hawaoni mabadiliko makubwa kwenye maisha yao.

Pamoja na changamoto hizi za ajira, kuna fursa nyingi ambazo zipo nje ya ajira, ila waliopo kwenye ajira na hata wanaotafuta ajira bado hawahangaiki kuzitumia vizuri. Bado mtu atang'ang'ania kufanya kazi aliyoanza kuifanya miaka 10 iliyopita japo hakuna chochote anachoweza kukionesha kwa miaka hiyo kumi zaidi ya madeni na msongo wa kila siku hasa linapokuja swala la fedha.Jambo hili limenifanya kufanya utafiti wa ndani zaidi ili kujua kwa nini waliopo kwenye ajira hata kama haiwaridhishi hawapo tayari kutafutra fursa nyingine? Na pia kwa nini vijana wanaomaliza masomo yao, wapo tayari kukaa nyumbani mwaka mzima, kuzunguka na bahasha ya kuomba kazi badala ya kufikiria kutumia fursa nyingine?

Katika kulitafiti hilo nimegundua mbinu mbili ambazo waajiri wote wanazitumia kuhakikisha waajiriwa wanaendelea kuwa watumwa wao. Naposema watumwa, iko wazi kwamba kama mtu anafanya kazi ambayo haimridhishi na wala haifurahii hakuna neno rahisi la kutumia zaidi ya utumwa.

Mbinu hizi mbili zimetumiwa vizuri sana na waajiri na zimeingia kwenye akili ya waajiriwa kiasi kwamba ni vigumu sana kunasua kwenye mtego walioingia.

Mara nyingi unakutana na mtu anayeanza ajira na anakuambia atafanya kwa miaka kadhaa na baadae ataacha afanye mambo mengine makubwa, ila kadiri miaka inavyozidi kwenda ndivyo anavyozidi kuwa na hofu ya kuacha ajira ile. Hii yote inatokana na mbinu hizi zilizotengenezwa na waajiri.

Mbinu ya kwanza; Kuwashawishi kwamba kupitia ajira ndio wataweza kumudu maisha yao;

Kupitia mbinu hii waajiri wanawafanya waajiriwa kuamini kwamba kupitia ajira ndio wanaweza kuyamudu maisha yao. Wanafanya hivi kwa kumhakikishia mfanyakazi mshahara wake wa mwezi, iwe kampuni au taasisi imefanya kazi kwa faida au la. Mfanyakazi hata kama ana mshahara mdogo kiasi gani ana uhakika wa kuupata kila inapofika mwisho wa mwezi.

Pia kupitia mbinu hii waajiri wanawahakikishia wafanyakazi wao maisha mazuri hata baada ya kustaafu. Wanawachangia katika mfuko wao wa mafao ya uzeeni na pia mfuko huu unawafanya waajiriwa kuona kuna kitu kizuri na kikubwa mbeleni, hivyo kuendelea kuwa wafanyakazi watiifu.

Mbinu ya pili; Kumwogopesha mwajiriwa kwamba hakuna maisha nje ya ajira;

Kupitia mbinu hii waajiri wameweka sheria mbalimbali ambazo zinamfanya mwajiriwa aendelee kuwa mtumwa kwa mwajiri wake. Kwa mfano mwajiriwa ameshakaa kwenye ajira kwa miaka kumi na ameshachangia kiasi kikubwa kwenye mafao yake, ataambiwa akiacha kazi au kufukuzwa kazi mafao yake, ama anayapoteza au atayadai akishafikisha umri halali wa kustaafu.

Hiki ni kifungo kikubwa sana kinachomhakikishia mwajiri kwamba anaendelea kuwa na watu wanaomtumikia hata kama hawataki kufanya hivyo.


Mbinu hizi mbili zimeshaingia kwa wafanyakazi ambao ni wakongwe kazini na ndio maana wengi wanaweza kupanga kuacha kazi na kufanya mambo mengine lakini wanashindwa. Swali la kushangaza ni je mbinu hizi mbili zimepandikizwaje kwa vijana ambao bado hawajaingia kwenye ajira kabisa?

Kwa vijana ambao bado hawajaingia kwenye ajira kabisa nao wameshanasa mtego huu. Wameshaoneshwa kwenye ndoto kwamba kupata ajira kwanza ndio kujiwekea usalama wa maisha na hata kama ni kuangalia fursa nyingine basi ni baada ya kuwa kwenye ajira kwanza. Hivyo wanakazana kuingia, wakifikiri wataweza kutoka watapotaka, ila wakishanasa mtego wanaishia kuwa watumwa kwa kipindi kirefu kwenye maisha yako.

Unahitaji maarifa na nguvu ya ziada ili kunasua kwenye mtego huu. Unahitaji kuangalia uhalisia ili uweze kujua kwamba lolote linawezekana iwe ni kwenye ajira au nje ya ajira. Na unahitaji uweze kufanya maamuzi yako mwenyewe, kuyasimamia na kutokusikiliza wanaokukatisha tamaa ndio utaweza kuondoka kwenye mtego huu.

Vinginevyo utakuwa unaweka mipango kila siku ya kujikomboa lakini ikifika kuchukua maamuzi, unajikuta upo kwenye mtego aliokuwekea mwajiri wako.

Mwaka 2014 umeisha, je umefanya nini? Umefikia malengo uliyopanga? Na je umejipangaje kwa mwaka 2015? Karibu kwenye semina ya siku 21 za mafanikio makubwa mwaka 2015 itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina hii itakuwezeshakuweka malengo ambayo utaweza kuyafikia, kubadili fikra mbaya ulizopandikizwa zinazokufanya uendelee kuwa mtumwa na pia kukupa mbinu za kuboresha kazi au biashara unayofanya. Kushiriki semina hii andika email kwenda amakirita@gmail.com

Nakutakia kila la kheri katika kujiandaa na mwaka 2015, naamini utakuwa mwaka bora sana kwako.


Tupo pamoja.
 

ssafari

Senior Member
Jul 17, 2013
174
225
Barikiwa sana mtumishi Kwa maneno mazuri yenye kututia hamasa ya kubadili mawazo mgando vichwani mwetu.
 

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,465
2,000
Asanteni sana wakuu,
Tufanyie kazi haya tunayojifunza ili maisha yetu yapate kubadilika na kuwa bora zaidi.
 

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,211
2,000
Asante, kuna kampuni moja mwanza haijalipa wafanyakazi wake mishahara kwa miezi mitano sana sijui wafanyakazi wake wanaishije na maisha haya magumu Mungu wangu, na sijui kama wanafanya maendeleo yoyote.
 

Fundisi Muhapa

JF-Expert Member
Nov 25, 2013
4,433
2,000
Kuajiriwa kamwe si utumwa. Sijui ni kwanini umeamua kuutafsiri hivi: "... kwamba kama mtu anafanya kazi ambayo haimridhishi na wala haifurahii hakuna neno rahisi la kutumia zaidi ya utumwa ...". Au umeamua 'kuunda' tafsiri itakayofaa mada yako?

Makirita Amani unaendelea kusema mwajiri ...kwa kumhakikishia mfanyakazi mshahara wake wa mwezi, iwe kampuni au taasisi imefanya kazi kwa faida au la... ni kwakua anataka waendelee kuwa 'watumwa'. La hasha! Ujira ni stahili yao hata kama mwenye mtaji atapata hasara kipindi hicho kwakua tayari kuna kazi walifanya. Ndio maana mshahara hulipwa mwisho wa mwezi. Ikiwa mwenye mtaji atahisi hatokaa apate faida katika uwekezaji wake, unadhani atahitaji kuwa na 'watumwa'?

Mkuu, usitengeneze mazingira kuwa kuajiriwa ni utumwa. Itakugharimu sana siku za usoni. Fikiria NGO/Kampuni yako ikifikia hatua ya kuajiri. Kwa upande mwingine, naamini utawatoza hao watakaohudhuria hiyo semina ya siku 21.
 

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,465
2,000
Kuajiriwa kamwe si utumwa. Sijui ni kwanini umeamua kuutafsiri hivi: "... kwamba kama mtu anafanya kazi ambayo haimridhishi na wala haifurahii hakuna neno rahisi la kutumia zaidi ya utumwa ...". Au umeamua 'kuunda' tafsiri itakayofaa mada yako?

Makirita Amani unaendelea kusema mwajiri ...kwa kumhakikishia mfanyakazi mshahara wake wa mwezi, iwe kampuni au taasisi imefanya kazi kwa faida au la... ni kwakua anataka waendelee kuwa 'watumwa'. La hasha! Ujira ni stahili yao hata kama mwenye mtaji atapata hasara kipindi hicho kwakua tayari kuna kazi walifanya. Ndio maana mshahara hulipwa mwisho wa mwezi. Ikiwa mwenye mtaji atahisi hatokaa apate faida katika uwekezaji wake, unadhani atahitaji kuwa na 'watumwa'?

Mkuu, usitengeneze mazingira kuwa kuajiriwa ni utumwa. Itakugharimu sana siku za usoni. Fikiria NGO/Kampuni yako ikifikia hatua ya kuajiri. Kwa upande mwingine, naamini utawatoza hao watakaohudhuria hiyo semina ya siku 21.
Mtu ambaye anafanya kazi ambayo haipendi, kipato anachopata ni kidogo na hakimtoshelezi na kila siku anapata msongo wa mawazo kutokana na kazi hiyo, lakini bado anaogopa kuacha kazi hiyo akiamini maisha hayawezekani unaweza kutumia neno gani rahisi kwa mtu huyo ukiacha utumwa??
Kama umesoma na kuelewa vizuri nilichoandika, siko kinyume na kazi kwa sababu ni muhimu sana, na nimeandika kwenye sentensi ya kwanza kabisa.
Nachosema mimi ni mtu afanye kazi ambayo anaipenda, kila siku inampa shauku ya kufanya kwa juhudi zaidi na hata kuwa mbunifu zaidi, hii ndio itamfanya mtu aweze kuwa na uhuru na maisha yake.
Lakini kama mtu anaenda kazini kwa kuwa tu inampatia kipato, kutekeleza majukumu yake ni mpaka apangiwe na asimamiwe, anatafuta kila sababu ya kukwepa baadhi ya majukumu, huu ni utumwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom