Hizi ndio feeling za maaskari tanzania, kumbe wanalazimishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndio feeling za maaskari tanzania, kumbe wanalazimishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by howard, Nov 23, 2011.

 1. howard

  howard Senior Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wakati vurugu zinaendelea sehemu mbalimbali za nchi yetu napokea ujumbe usemao, “Mwalimu mwema naomba usiandike namba yangu gazetini kwa sababu mimi ni polisi. Naendesha gari la washawasha. Kila ninapowamwagia wananchi wenzangu maji ya kuwasha wanapodai haki zao roho yangu huniuma sana. Tufanye nini?”

  Source: Tanzania Daima: makala ya mwalimu mkuu wa watu - Paschally Mayega

  MYTAKE: Mimi nahisi maaskari wanachokifanya ni kwa sababu ya amri za viongozi wao, siku wakija kusema kwa nini tuwatese wananchi wenzetu wakazima magari na kuweka mabomu ya machozi chini kitatokea nini Tanzania. tulishuhudia libya, tunisia na misri askari wakiungana na wananchi wenzao kwa nini isitokee Tanzania siku moja. ikumbukwe inakuwa ngumu kuikataa amri ya wakubwa wako, mimi ninachojua maaskari nao wana matatizo mengi mno, kuanzia kwenye familia, makazi yao, sehemu zao za kazi nk.
   
 2. the grate

  the grate JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 205
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  me naamin hawa polisi hawana makosa bali wanatekeleza amri za wakubwa wao
   
 3. howard

  howard Senior Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mungu atusaidie hawa maaskari siku waje kusema no hatutaweza kuwapiga watanzania wenzetu sasa imetosha
   
 4. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,213
  Likes Received: 2,077
  Trophy Points: 280
  Unadhani bei za petroli na sukari zinapopanda haziwagusi polisi? Unadhani wanafunzi wanaokosa mikopo toka bodi ya mikopo hawamo watoto wa polisi na polisi wenyewe ndani yake? Nao inawauma, lakini kwa sababu wanafanya hayo wafanyayo chini ya kiapo wanakuwa hawana ujanja wa kubadili maamuzi. Jamaa aendelee tu kumwaga maji ya upupu na kurusha risasi za moto, kuna wakati huwa vinaua ndugu zao, nao wanalia.
   
 5. P

  Panda Kapesi JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 284
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Tusisahau kuwa wengine wamezaliwa hivyo hivyo na roho mbaya haijalishi wana kipato au hawana. Wangapi tumeona ni senior officers lakini ndio wamekubuhu kwa uonevu na ukatili. mifano ipo hai to au mmesahau akina Zombe na akina Mahita! Je yule wa Arusha naye mmemsahau?
  Wapo polisi wazuri tu ambao ni professionals lakini pia tunao "criminal elements" nyingi tu ndani ya jeshi letu la polisi ambao wanatumia kivuli cha nafasi yao kufanya maovu ya kutisha na wengine huwa wanafurahia saaana ukatili huo!
  Tusidanganyike!
   
Loading...