Hizi ndio aina 10 za mbwa hatari duniani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,439
Inajulikana kwamba mbwa ni rafiki mkubwa wa binadamu ambapo licha ya kuumbwa kuishi karibu na binadamu, wanayama hawa wanatajwa kuwa miongoni mwa viumbe wenye akili ukimuondoa binadamu. Wako vizuri kwenye kuwinda, ulinzi na wakati mwingine hutumika kama mwandani katika matembezi ya binadamu.
Hata hivyo, kuna report zinazoonesha kuwa Mbwa wanaweza kuwa maadui wakubwa wa binadamu na zipo aina nyingi za Mbwa lakini zipo zinazotajwa kuwa...
tishio zaidi duniani.


10.DOBERNMAN PINSCHERS
1d8bda20a16bcde10145556688ae6eb0.jpg

Mbwa huyu anajulikana kuwa na akili na mwenye nguvu nyingi. Anafaa sana kuwa mlinzi mzuri kwa binadamu. Pia huwa wanatumiwa na Polisi kutafuta wahalifu lakini hata hivyo asipopata mafunzo mazuri anaweza kuwa tishio na anaweza kumuua binadamu.


9.HUSKIES
2a7d3de066e2ef3966a8527e73672055.jpg

Mbwa huyo ni maarufu sana kutokana na macho yake ambayo ni tofauti na mbwa wengine. Wanatumika sana kwenye michezo ya kuteleza kwenye theluji na wanajulikana kuwa na uwezo mkubwa wa kusukuma vitu kwa muda mrefu kuliko mbwa yeyote.


8.BULLMASTIF
037e176f500fb2da6885fc52343438b7.jpg

Mbwa huyu anajulikana kuwa mkali na hatari Sana. inashauriwa kuweka watoto mbali naye. Zipo kuwa mwaka 2014 mbwa aina hii aliwashambulia vijana wawili waliokuwa wakicheza mpira kwenye nyumba ya jirani. Kijana mmoja aliuawa na baada alimshambulia mmiliki wake. Wanatumika sana kwenye ulinzi na wana maumbo makubwa.


7.WOLFDOG
6abf7ffa11006985b50996322816be77.jpg

Huyu ni mchanganyiko wa uzao wa Ujerumani na Shepherd ambapo mchanganyiko huu unafanya mbwa huyu kuwa mkali sana. Wanaweza kubadilika kutona na hali watakayokutana nayo.


6.MIDACET SULA SHEPHARD
ab878dbe8ae49b1a79236383ecceae2b.jpg

Mbwa huyu anatoka kwenye uzao usiojulikana, dhumuni la mchanyiko huo ni kupata mbwa mkali na hatari zaidi Duniani. Mbwa huyu angefaa kulinda binadamu lakini kutokana na ukali wake hawezi kuwa karibu na binadamu na amezuiliwa kwenye baadhi ya nchi.


5.FILA BRASILEIRO
87afb3bfbc5d50a5f4a5b6b789c79495.jpg

Kama hupendi Mbwa mkali basi usimiliki mbwa huyu. Asili yake ni Brazil na hutumika kwenye shughuli za uwindaji. Anatajwa kuwa mkali na hatari kwa binadamu.


4.ROTWELLER
75a88b26411847c13c1e56e0011e0b7c.jpg

Kama k4.ROTWLER una mbwa aliyesababisha vifo vingi ni huyu. Imeripotiwa kuwa Mbwa huyu amesababisha vifo vingi Marekani. Wana uwezo wa kuruka juu sana na kudhuru koo la binadamu. Inashauriwa kuwa mbali na mbwa huyu.


3 PERRO DE PRESA CANARIO
c9636fd97819b48f069dcfca9bed7b2d.jpg

Mbwa huyu ametoka kwenye Visiwa vya Canary. Alitengezwa kwa kutumia mchanganyiko wa mbwa tofauti ili apatikane mbwa mwenye uwezo wa kupambana na wahalifu.


2.PITBULL
d1144054e939f676b0f002eca28fa117.jpg

Mbwa huyu amezuiliwa kwenye nchi nyingi duniani kutokana na ukali wake na ni hatari kwa binadamu. Aina hii ya mbwa kama hawajafunzwa tangu utotoni wanaweza kuwa mashine ya mauaji. Hutumika kwenye mashindano halifu ya kupigana na mbwa wengine mpaka kifo na wamiliki wao hujipatia pesa kupitia biashara hiyo.


1.CAUCASIAN SHEPHERD
7987a7cf01c8305358d7b77c46d30589.jpg

Asili ya mbwa huyu ni Urusi ambapo kwa karne kadhaa amekuwa akitumika kulinda mashamba ya mifugo milimani. Ana uzito unaokadiriwa kufika zaidi ya KG 100 (220lb) ambao ni uzito wa misuli pekee.
 
Dah umenikumbusha mbwa wangu Jimmy alikuwa habweki maisha yake yote yeye ilikua ni action tu.

R.I.P Jimmy mpaka leo sijawahi kufuga tena mbwa kutokana na majukumu na kuhama home, au kwenye nyumba za kupanga tunaruhusiwa kufuga mbwa?
 
Back
Top Bottom