Hizi mboga na nafaka kiingereza chake ni kipi?

Habarini wana JF wenzangu.
Naomba kufahamishwa pia ivi vitu vinaitwaaaje kwa KINGEREZA.
1.pili pili kichaa.
2.pili pili mbuzi
3.magimbi.
Asanteen
Mkuu, Kwa "Kichaa" nami ni mtupu kabisa hapo.

Utaona "Chilli Peppers" wakisema ni "Pilipili Kali" kigugumizi ni pale uki search "Pilipili Kichaa".

Lakini ukiangalia images zake pale www.google.com kwa "Chilli Peppers" au "Pilipili Kali" zinakuja, na muonekano ni ule ule wa "Pilipili Kichaa".

Safisha mboni hapa mkuu
www.african-food-recipes.blogspot.com/2019/02/translation-of-spices-from-english-to.html?m=1
 
Mkuu Alaik

Nimevuna vuna madini katika kiunga ulichonipatia.

Nashukuru sana mkuu, Kuna kitu pale sijakiona "Types za true nuts"
 
Mlenda= Jutemallow
Bamia= Okra
Nyanyamshumaa= African eggplant
Mchicha= Amaranth
Kunde= Cowpea
Mbaazi= Pegionpea
Dengu= Lentil
Majani ya kunde= Cowpea leaves
Matembele= Sweet potato leaves
Biringanya= Eggplant
Figiri= Ethiopian Mustard
Choroko= Greengram/Mungbean
Hoho= Sweet pepper
Mkuu Alaik uko vizuri mkuu , lakini naomba ucheki vizuri figili/ figiri sidhani kama inaitwa hivyo as Ethiopian mustard naomba utuchekie tena
 
Mkuu Alaik uko vizuri mkuu , lakini naomba ucheki vizuri figili/ figiri sidhani kama inaitwa hivyo as Ethiopian mustard naomba utuchekie tena
Mkuu, Shukrani sana kwa mchango wako.

Nami natatizika hapo kwenye neno, "mustard"

Hivi "Haradali" siyo "Mustard" kwa Kiingereza kweli!?!!
 
Habari za muda huu wa wanaJF!

Kama yalivyo maelezo hapo juu.

Naomba kufahamu kwa Kiingereza majina ya mboga na nafaka zifuatazo:-

Mlenda, Bamia, Nyanyamshumaa, Mchicha, Kunde, Mbaazi, Dengu, Majani ya Kunde, Matembele, Bilinganya, Msusa, Figiri, Choroko, na Pilipili Hoho.

Natanguliza shukrani.
Bamia - okra
Dengu - lentils
Choroko - green gram
Kunde - cow peas
Bilinganya - egg plant
Pilipili hoho zimetajwa na mdau hapo juu
Mengine watajazia wadau
 
msahada wana JF wenzangu,
as ina hizi za maharagwe kwa kingereza zinaitwaaaje?
Nawasilisha.
Screenshot_20210916-231356.jpg
 
msahada wana JF wenzangu,
as ina hizi za maharagwe kwa kingereza zinaitwaaaje?
Nawasilisha.View attachment 1941093
Shukrani sana kwa mchango wako wa dhati katika uzi huu.

Mimi pia binafsi aina hizo zisifahamu, Labda waje wakuu wengine watusaidie hapa.

Na mkuu Dream Queen simpati kwa wiki kadhaa hivi, Angeonekana hapa huenda angetia neno.
 
Mlenda - Mucus
Bamia - Lady finger
Nyanyamshumaa - Tomato-Candle
Mchicha - Leafy greens
Kunde - Micro beans
Mbaazi - Green Soy
Dengu- Yellow beans
Majani ya kunde - Micro bean leaves
Matembele - Front Saliva
Bilinganya - Purple Billi
Msusa - Muabandon
Figiri - Feegys
Choroko - Bad Meets Evil
Pilipili HoHo- Green Pepper
Haya majina ulikuwa unafanya masihara .....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom