Hizi mbinu zinazotumiwa kufifisha mijadala kuna siku zitaleta balaa kubwa nchini

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,292
3,962
Ni kawaida watu wakileta hoja hapa dhidi ya serikali mijadala huingiliwa na watu kwa kuibinafsisha ama kwa BAVICHA ama kwa dini mojawapo kubwa.

Kwa hiyo ni kumaanisha kuwa wananchi wamewagawa katika makundi mawili ama CCM ama BAVICHA. Kwamba CCM huwa wameridhika na kila kitu kinachofanywa na serikali na BAVICHA wanasubiri kukosoa kila kitu.

Ama kama ukiwasema watu wa dini fulani basi ni kwa vile uko dini nyingine. Kwamba John akifanya mabaya basi wale wa dini yake wanaridhika tu.

Hapo nyuma tuliona suala la ukabila likitumika sana.

Watanzania tumeshindwa kujibu hoja kwa hoja hadi tuwagawe watu kwa itikadi au ukabila ili tuungwe mkono hata kama hatuna hoja?

Siku moja mtaleta balaa maana matatizo ni ya kweli na hayajui itikadi.
 
Kwa hiyo tukusaidieje Sasa! Hoja zenyewe ujinga tuuu
Kweli upumbavu ni kipaji Kama urefu na ufupi

Mtoa mada anakazia swala la kujibu hoja kwa hoja ila wewe umekuja kudhihirisha jinsi gani tuna hali mbaya Kama nchi
 
Back
Top Bottom