Hizi likizo za Rais Magufuli ni tofauti na watumishi wengine?

Chifyono

JF-Expert Member
Oct 16, 2017
921
1,658
Watumishi wengi wa serikali kawaida husain likizo zao mara moja kwa mwaka au mara mbili(i stand to be corrected)

Inafahamika wazi rais ni sehemu ya utumishi wa umma, tangu huu mwaka uaenze amekwenda kwao Chato kwaajili ya mapumziko (likizo) si chini ya mara 4

Je hivi likizo zake ziko tofauti na watumishi wengine katika nchi hii?
Vipi malipo ya likizo zake nani huzigharamia?
 
Aliyekuambia rais ni mtumishi wa umma kakudanganya, rejea hotuba ya JK wafanyakazi walipotaka kugoma alisema “mimi ndio muajiri Number one” wafanyakazi muamue kunisikiliza mimi au mmsikilize katibu mkuu TUCTA (Mgaya by then). Mgomo haukufanyika. Kwa taarifa yako tu Likizo kwa viongozi wakubwa wengi kama Rais, RC, Mawaziri huwa likizo zao wanachukua siku chache chache kwa mwaka mfano siku saba, baadae siku kumi etc hadi siku 28 zinaisha. So Mh. Rais hajakosea
 
sijaona tatizo....ye huwa haendi mwezi+ kama watumishi wengine....so hata kama anaenda siku tatu kila mwezi bado hafikii jumla ya siku za likizo za annual ambazo huwa hazijumlishi weekend na holidays....NB:sio kila kitu ni chakukosoa
Kama anaenda likizo achukue mwezi kueleweke na asubiri hadi mwaka uishe ndio arudi kwao, sasa kila mtumishi akiwa anajichukulia siku 3 then anarudi kazini hali itakuwaje

Sio kila baada ya muda mfupi anarudi chato
 
Mida mingine tuwe positive naona hawa Marais wengi wa Kiafrika hawachukui likizo kwa maana halisi bali wanaenda kwao kutembelea ndugu!hata wakiwa hiyo "likizo" bado wanafanya kazi za kijamii au kisiasa;
 
Aliyekuambia rais ni mtumishi wa umma kakudanganya, rejea hotuba ya JK wafanyakazi walipotaka kugoma alisema “mimi ndio muajiri Number one” wafanyakazi muamue kunisikiliza mimi au mmsikilize katibu mkuu TUCTA (Mgaya by then). Mgomo haukufanyika. Kwa taarifa yako tu Likizo kwa viongozi wakubwa wengi kama Rais, RC, Mawaziri huwa likizo zao wanachukua siku chache chache kwa mwaka mfano siku saba, baadae siku kumi etc hadi siku 28 zinaisha. So Mh. Rais hajakosea

Mbona mwisho wa mwezi analipwa kama watumishi wengine wa umma?
 
Back in the days on the account of history wise masters of the land or people adviced by them were politicians,,,contrary to our age where bold opportunists are greedy for the control of the govn and party's helm,,,I cry for Mama Tanganyika
 
Mkuu Grey256 ,katika likizo za kiserikali,sikukuu na mwisho wa juma hujumuishwa. Siku 28 huhesabiwa mfululizo tu.
labda kwa baadhi ya taasisi za serikali ila kwa ninayoijua mimi,weekend na holidays haziesabiwi kwenye annual leave ndo maana watu huwa wanagombea mwezi wa 12 maana una holidays nyingi so badala ya siku 28 unapata mpaka 40+
 
Hapo kuna hoja lakini kwa sababu ya ushabiki itapotezwa!

Hakuna hoja hapo. Mafuriko,ukame, njaa, maji, umeme,mishahara ,mikopo wanafunzi chuo kikuku, barabara, vivuko, 50 milloin kila kijiji,ujenzi wa viwanja vya ndege,kutumbua majipu etc. zote anaangaliwa yeye. Sawa ni mtumishi lakini si kama hao unaowatambua wewe. HAKUNA HOJA HAPO
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom