KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Wana madudu mengi anayoyafahamu Magufuli. Na wanajua hana staha, atayatangaza madudu hayo mbele za wananchi.Wewe ungeweza kuyasema haya uliyoyaandika mbele ya Magufuli?! Inaonekana anatisha sana.
Kuna wakati aliwaita viongozi wastaafu woote ikulu, akawaambia WAMUACHE AFANYE ATAKAVYO , KAMA WAO WALIVYOFANYA WAKATI WAO.
Na aliwakumbusha WAACHE KUWASHWA WASHWA.
Tangu siku hiyo kimyaaaa, tunawasikia kwenye kumbukizi za Mwl Nyerere wanapumua utadhani wana pumu, vifua vimewajaa wanagombea mic.
Kwanini wasiite press waka sema tu,, wanaogopa nini?! Au nao wanashughulikiana au kushughulikiwa?!
Mwalimu aliweza kusema chochote bila ya hofu kwa sababu hakuwa na 'kabati lililojaa mifupa.'