Hizi kodi za TRA za kuingiza magari nchini zikoje?

Mi nalipiaga tu ila nakuja pandisha bei kwa ninaowauzia basi. Yaani kadiri TRA anavonikamua ndo na mie ninavohamishia burden ile kwa ninaemuuzia gari. sina muda wa kuhoji

Hilo nalo neno ila siku ukilipa kodi kubwa alafu unaoenda kuwauzia katika kipindi hicho purchasing power yao imekuwa ndogo kutokana na gharama za maisha kupanda nadhani ndio itakuwa muda muafaka kwako kupiga kelele.
 
Hizo formula tu zinahitaji jitihada ya ziada kuzielewa na kuzifafanua, sasa kwa wabunge wetu ambao ni wazee wa imepita bila kupingwa so long mswada umeletwa na serikali hapo ndio inakuwa kasheshe ukichanganya tena ni mambo ya hisabati wataishia kusema haya ni mambo ya kitaalamu, kiukweli kodi kwa Tanzania inalipwa na watu wachache kwa niaba ya wengine na sidhani kama serikali ingebuni vyanzo vingine vya kodi hili tatizo lingeendelea

Unajua mkulu hizi sheria zinaanzia kwenye kamati za kisekta, wizarani hatimaye zinaenda mpaka bungeni... sasa tukiwalaumu wabunge tutakuwa tunawaonea kwa sababu wenyewe (wengi wao si wataalam wa mambo mbalimbali).... na pale bungeni hawapati muda wa kupitia vipengele vyote kwa undani.... ndiyo maana wanasema tu ndiyoooo.... na hapo waheshimiwa wabunge wakiingiza ushabiki wa kivyama hali inakuwa mbaya zaidi, maana wanaunga mkono hoja bila hata kuitafakari na kuipima ilimradi tu inatoka chama chake.....
 
Unajua mkulu hizi sheria zinaanzia kwenye kamati za kisekta, wizarani hatimaye zinaenda mpaka bungeni... sasa tukiwalaumu wabunge tutakuwa tunawaonea kwa sababu wenyewe (wengi wao si wataalam wa mambo mbalimbali).... na pale bungeni hawapati muda wa kupitia vipengele vyote kwa undani.... ndiyo maana wanasema tu ndiyoooo.... na hapo waheshimiwa wabunge wakiingiza ushabiki wa kivyama hali inakuwa mbaya zaidi, maana wanaunga mkono hoja bila hata kuitafakari na kuipima ilimradi tu inatoka chama chake.....

Hapo kwenye ushabiki wa kisiasa wakiacha mambo yatakwenda kama maslahi ya taifa yatazingatiwa maana kuna wabunge hasa wa CCM kila mswada unaoletwa na serikali kwao upo sahihi na ndio maana kwenye sheria ya mifuko ya jamii walipitisha bila kujijua na mwisho wa siku wanarudi upya kujipanga kujadili upya. Ni kweli hawapati muda wa kujadili lakini miswada ile si wanapata in advance kabla ya kikao hivyo wanaweza ku-share na wadau mbalimbali (mbunge makini anahitaji mbinu mbadala ya kujifunza issue ili akiingia bungeni angalau mawili matatu ayajue japo si yote na ndio maana kukaundwa kamati mbalimbali za kudumu ili wawe wanaangalia kwa kina kabla ya mswada kufika bungeni ikiwa na maana wanawasiliana na wataalamu mbalimbali ambao wanatoa inputs). Naungana na wewe kwamba tusiwalaumu wabunge pekee bali hata hawa wataalamu wa wizara nao pia though kwa upande mwingine maamuzi ya wataalamu hawa huwa yanaingiliwa na wanasiasa (Waziri wa wizara husika ambae ni sehemu ya bunge anaweza ku-influence some issues ziwe incorporated kwenye mswada pia)
 
Ningeomba kupata uzoefu kwa ambao wameshapitishia magari Mombasa. Maana uozo wa TPA na urasimu wa TRA pale bandarini unanitia kinyaa.

Nikipitishia gari Mombasa na kuingiza mpaka wa Namanga au border post yoyote bado ni lazima paper work ifanyike Dar kupata makadirio ya kodi? au Offisi za TRA mipakani wanaweza kufanya makadirio na nikalipa kodi.

Swali langu la pili iwapo ninaishi Dodoma ninaweza kupeleka documents za gari ofisi za TRA Dodoma na kufanyiwa makadirio ya kodi au mpaka nipeleke document hizo Dar es salaam.

Swali la tatu je ninaweza kupeleka document mwenyewe au ni lazima nipitie kwa wakala wa kodi (au maarufu kama clearance and forwarding agents).

Ingawa nimeomba maoni ya wazoefu, Ningefurahi kupata majibu toka kwa maofisa wa kodi lakini watoe majibu kwa misingi ya sheria za kodi. Ruksa pia kutoa maoni yao iwapo wataona yatasaidia lakini yawe kama nyongeza kwenye majibu ya msingi
 
uliyoyaongea yana maana sana.
Yani kitu kipo "compounded" badala ya kua from base. Maana ni kua tax base haijulikani.

Ni sawasawa ukatwe sdl kwenye mshahara, kiwango kinachopatikana kijumlishwe tena kwenye mshahara ukatwe paye, wizi mtupu huu.


Cha ajabu kingine formula zao zina mikwara mingi tu badala ya kua straight. Hayo yote ni kutengeneza mazingira ya kula.

uko sawa sawia mkulu......

Mfano unalipwa mshahara basic tshs 100, halafu paye ni 20%.........
Ina maana utabakiwa na tshs 80. Sasa wakikukata tena nssf (mfuko wa hifadhi) 5%...... Watakata kwenye ile ile basic tshs 100....... Hivyo utabakiwa na take home ya tshs 75.

Sasa wanachofanya tra ni kama kukata nssf kwenye ile balance yaani asilimia 5 ya tshs 80..... Badala ya ile basic tshs 100.

Wahusika hawataki kutoa majibu.......
 
Back
Top Bottom