Hizi kodi za TRA za kuingiza magari nchini zikoje?

eliakeem

JF-Expert Member
May 29, 2009
15,629
13,764
Wadau kuna rafiki yangu ameniuliza swali kuhusu kodi za kuingiza magari yaliyo tumika toka Japan. Sasa ananiambia ameona kanuni za kukokotolea kodi kwenye tovuti yao http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=460&Itemid=59. Lakini kilichomshtua ambacho hata mimi nimekiona ni kwamba kodi inatozwa kodi....
Ona hapo chini...

Formula:

  • I/D = CIF * 25%
  • EXA = (CIF+I/D) * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18%

Where:

  • CIF – Cost Insurance and Freight (Taxable Value)
  • I/D – Import Duty
  • EXA – Excise duty for vehicles aged more than 10 years
  • EX – Excise Duty
  • VAT – Value Added Tax

Sasa ukiangalia hapo juu kwenye hiyo milinganyo sahili (FORMULA) utagundua kuwa I/D (Import Duty) ambayo ni kodi nayo inatozwa kodi. Kwa lugha nyingine kwa wale wanaokumbuka milinganyo (a simple algebra), zile kanuni za pale juu ni sawa na kuziandika

  • EXA = (CIF+I/D) * 20% = CIF * 20% + I/D * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5% = CIF * 5% + I/D * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18% = CIF * 18% + I/D * 18% + EXA * 18% + EX * 18%

Sasa kimsingi swali ambalo hata mimi nimeshindwa kumjibu rafiki yangu...... ni halali kodi kutozwa kodi???? katika mlinganyo huo hapo juu inaonekana kuwa I/D (Import Duty ambayo pia ni kodi) lazima itozwe EXA, EX na VAT. Pia EXA (Excise duty for vehicles aged more than 10 years ambayo pia ni kodi) na EX (Excise Duty ambayo pia ni kodi) nazo zinatozwa kodi.
Nauliza tena hiyo ni halali??? Sheria zinasemaje kuhusu hili????... Nina hamu sana kujua jinsi sheria zinavyo sema... vinginevyo mimi naweza kusema hii si haki kwa watanzania kutoza kodi kwenye kodi.....

Maana mimi nilifikiri kuwa kila kodi itatozwa kutoka kwenye kiwango cha msingi (a base) kwa hapa tuna maanisha CIF ambayo hata TRA wenyewe kwenye valuation yao ya magari wanasema ndiyo inayopaswa kutoza kodi (taxable) lakini cha kushangaza wanatoza hata kwa kodi ambazo hazipaswi kutozwa kodi (non - taxable) ......
Mimi binafsi nilifkiri kanuni ya kodi ingekuwa kama ifuatavyo

I/D = CIF * 25%

EXA = CIF * 20%
EX = CIF * 5%
VAT = CIF * 18%

Halafu lingine la msingi ni kuwa, kwa nini EX na EXA ambazo ni kitu kimoja zinatozwa mara mbili? Kwa nini isitozwe mara moja tu? Kwa mfano ungeweza kusema Gari lenye umri wa chini ya miaka 8 Excise Duty ni 10% na Gari lenye umri wa zaidi ya miaka 8 Excise Duty ni 15% ili mlinganyo uwe kama ifuatavyo....

I/D = CIF * 25%
EX = CIF * Q% (Q inategemea umri wa Gari. < miaka 8 ni 10%; > miaka 8 ni 15%)
VAT = CIF * 18%

Wanajamii nikipata mawazo ambayo yanaegemea sheria nitafurahi zaidi.....

Naomba kuwasiilisha...

Wasiliana na TRA wenyewe watakupa majibu ya hio kitu. Namba za simu na huduma kwa wateja zipo kwenye website yao www.tra.go.tz
 
Mi nalipiaga tu ila nakuja pandisha bei kwa ninaowauzia basi. Yaani kadiri TRA anavonikamua ndo na mie ninavohamishia burden ile kwa ninaemuuzia gari. sina muda wa kuhoji
 
Ni kweli unawapa mzigo wa kodi mnunuaji wa mwisho...... Lakini pia ni lazima tujue kwa nini kodi inatozwa kodi...
 
Asante sana mkuu, mpaka hapo HONGERA SANA ELIAKEEM,,... SIJAAMINI KAMA PANA WATANZANIA KAMA WEWE, Hakika tukipata wazalendo wenye kutumia bongo zao kama ELIAKEEM Nchi yetu tutajikomboa na utumwa huu wa ujinga na Umaskini,

NACHOJUA KWA UJUMLA KODI YA TRA INATOKANA NA UJINGA WETU, HAKUNA LOGIC AINA YEYOTE, Ujinga wako ni pesa kwao, kama hamtaamini tuendelee kufuatilia hili lililoko wazi kabisa na umechambua vizuri sana, na hao maafisa wa TRA wapo humu nawajua tena wengi sana, tuone watatujibu nini ? ? zaidi ya kukuomba uende ofisini kwao... ukiwabana sana watakuambia ''WEWE UNADHANI KODI ITAPATIKANA WAPI ? ? ? '' TUTAFIKIAJE MALENGO TULIYOPANGIWA ? ? ?'' na zaidi tena watakuzulia vijikosa, penalty, wana UPLIFT x10, utanywea tu kisa "Unajifanya mjanja"

Tafadhali wwadau wote wa TRA mtuelimishe hapa hapa JF tunawasubiri ? ?
 
Uliyoyaongea yana maana sana.
Yani kitu kipo "compounded" badala ya kua from base. Maana ni kua Tax base haijulikani.

Ni sawasawa ukatwe SDL kwenye mshahara, kiwango kinachopatikana kijumlishwe tena kwenye mshahara ukatwe PAYE, wizi mtupu huu.

Cha ajabu kingine formula zao zina mikwara mingi tu badala ya kua straight. Hayo yote ni kutengeneza mazingira ya kula.
 
Ahsante sana eliakeem kwa kudadavua hiyo formula,kwa kuongezea kutokana na elimu yangu kiduchu ya kodi;
EX =Excise duty inayotozwa kwa magari yenye CC>1000cc.
Na kinachofanya kuwe na hiyo cummulative effect ni sheria ya VAT(Kodi ya Ongezeko La Thamani)Ndo maana kwenye kodi zote tax base ni CIF lakini ukija kwenye VAT kwa mujibu wa hiyo sheria kodi nyingine yaani I\DUTY,EXA na EX ndo zinazoongeza thamani ya CIF kwa hiyo VAT =18%( CIF+I\DUTY+EXA+EX)
 
hapo penye red...... kodi, isipokuwa I/D ambayo inatozwa kwenye CIF, lakini zingine zote zinatozwa kwenye CIF + I/D na VAT ndiyo usiseme... Halafu kitu kingine cha kujua kodi haiongezi thamani ya kitu ila inaongeza gharama...

T. R. A. siku zote ni wagumu kuwaelewa.... halafu wanatumia ujinga wetu wa kutojua sheria kutuumiza... mfano wa kodi nyingine inaitwa capital gain tax ambayo inatozwa endapo utauza viwanja, shamba, nyumba n.k..... sasa hiyo inatozwa kwenye faida (gain) au ..... hapa ni eneo lingine ambalo wanatuchakachua.....
 
Utaratibu wa sasa una gharama nafuu zaidi kuliko ule wa awali na upo fair regardless CIF umelipa bei gani. Ila kwa wezi ambao wamezoea kuiibia TRA wanaona si mzuri. Mimi nimeagiza gari katika mfumo wa zamani na mfumo mpya. Huu mpya uko fair sana
 
Unaweza labda fafanua zaidi.... ni jinsi gani mfumo wa sasa ni nafuu kuliko wa zamani.... na vipi kuhusiana na kodi... ziko kwa mujibu wa sheria au vp...
 
Utaratibu wa zamani kodi zilikuwa zinabase kwenye CIF na kwa hiyo watu walikuwa wanatemper na CIF ili kodi iwe ndogo. Sasa hivi TRA hawaangalii hicho, wanaangalia bei ya soko kwa gari kwa mwaka gari ilipotengenezwa then wana adjust na depreciation ndo wanaanza kulamba kodi zao. So unaweza kukuta gari umenunua kwa milion 1 kodi ukalipa milioni 3 au umenunua Milion 3 kodi ukalipa milioni 1. Need to say more?
 
That's valuation or assessment... ok lakini swala la kodi kutozwa kodi hujalijibu.... yaani I/D kutozwa EX na EXA na pia zote hizo kutozwa V.A.T.
 
Mkuu niliuliza hilo swali, jamaa kidogo wanifanye niache gari bandarini. Halafu kila mtu anasema amezikuta na sio position yake kujibu.
At some point mimi hua nachoka tu kudadisi sana mambo hapa nchini kwetu, maana napata frustrations tu!
 
je kodi ya uchakavu kwa magari ya uzalishaji kama pick-up, lorry na mabasi imeondolewa kama ilivyopendekezwa ?
 
Utaratibu wa zamani kodi zilikuwa zinabase kwenye CIF na kwa hiyo watu walikuwa wanatemper na CIF ili kodi iwe ndogo. Sasa hivi TRA hawaangalii hicho, wanaangalia bei ya soko kwa gari kwa mwaka gari ilipotengenezwa then wana adjust na depreciation ndo wanaanza kulamba kodi zao. So unaweza kukuta gari umenunua kwa milion 1 kodi ukalipa milioni 3 au umenunua Milion 3 kodi ukalipa milioni 1. Need to say more?

Ndugu polisi huo ufairness unaousema ni katika kudetermine CIF kwa wateja wote. I mean wateja wote wakiagiza mfano Rav 4 ya mwaka 2005 wanachajiwa CIF iliyo sawa regardless ya amenunua toka kampuni gani. Lakini katika ukokotoaji wa kodi formula ni ile ile, na ambayo ni kweli ni kandamizi kama alivyouweka eliakeem maana kodi inatozwa kwenye fedha yenye kodi ndani yake. Hili ndio swali la msingi!
 
Mkuu hili sina majibu yake kwa kina kwa sababu ndivyo sheria inavosema na wewe uko sahihi kwa maoni yako kuwa si sahihi ingawa mimi naona ni sahihi kabisa
 
TRA inaitaji kusafishwa haswa tena na fagio la chuma, Mwakyembe pekee hawezi, ningekuwa na huwezo ningelimfufua Sokoine, pale long room hapafai kabisa, kukupigia hesabu tu wa ushuru unachukua wiki kadhaa kama utoi rushwa, kila siku system hiko down, wewe unapata storage kwa uzembe wao, system itakuwa vipi down kitengo muhimu kama kile, cha ajabu uchakavu umeondolewa, lakini kwenye system bado hupo, means ukipewa R namba hata kama wenyewe wanajuwa kwamba uchakavu umeondolewa inabidi ulipe hivyo hivyo, kutoa uchakavu kwenye system inachukua days, nashangaa mie, pale unapewa hesabu unalipa,unaenda chini eti unakutana na mtu ana uplift ushuru uliolipa, sasa kwanini wasifanye hivyo toka mwanzo, si wanajuwa gari hipo wapi mle ndani, wanapopata karatasi zako si wakaikague kwanza kabla ya kukutoza ushuru.
je kodi ya uchakavu kwa magari ya uzalishaji kama pick-up, lorry na mabasi imeondolewa kama ilivyopendekezwa ?
 
Wadau kuna rafiki yangu ameniuliza swali kuhusu kodi za kuingiza magari yaliyo tumika toka Japan. Sasa ananiambia ameona kanuni za kukokotolea kodi kwenye tovuti yao http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=460&Itemid=59. Lakini kilichomshtua ambacho hata mimi nimekiona ni kwamba kodi inatozwa kodi....
Ona hapo chini...

Formula:

  • I/D = CIF * 25%
  • EXA = (CIF+I/D) * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18%

Where:

  • CIF &#8211; Cost Insurance and Freight (Taxable Value)
  • I/D &#8211; Import Duty
  • EXA &#8211; Excise duty for vehicles aged more than 10 years
  • EX &#8211; Excise Duty
  • VAT &#8211; Value Added Tax

Nisaidieni hapo kwenye red, baada ya PM kubadili huo muda TRA wameshaanza kutumia uchakavu baada ya miaka 10 badala ya miaka 8? Nimeingia kwenye hiyo web ya TRA nimekuta bado hawajabadilisha.
 
Mi sijari ilimradi makusanyo yanafika serikalini na yanarudishwa kwenye shughuli za ujenzi wa taifa.ila kwa tz ni ukanjanja tu kwani kati ya kodi yote inayokusanywa ni 45% tu ndo inafika serikalini na ikifika huko sasa kati ya hizo ni 10% tu ndizo zinawarudia wananchi the rest zinawekwa kwenye chai ya ikulu na misafara yake ya kifisadi hapa ndipo ulipo ugomvi wangu
 
Wadau kuna rafiki yangu ameniuliza swali kuhusu kodi za kuingiza magari yaliyo tumika toka Japan. Sasa ananiambia ameona kanuni za kukokotolea kodi kwenye tovuti yao http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=460&Itemid=59. Lakini kilichomshtua ambacho hata mimi nimekiona ni kwamba kodi inatozwa kodi....
Ona hapo chini...

Formula:

  • I/D = CIF * 25%
  • EXA = (CIF+I/D) * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18%

Where:

  • CIF – Cost Insurance and Freight (Taxable Value)
  • I/D – Import Duty
  • EXA – Excise duty for vehicles aged more than 10 years
  • EX – Excise Duty
  • VAT – Value Added Tax

Sasa ukiangalia hapo juu kwenye hiyo milinganyo sahili (FORMULA) utagundua kuwa I/D (Import Duty) ambayo ni kodi nayo inatozwa kodi. Kwa lugha nyingine kwa wale wanaokumbuka milinganyo (a simple algebra), zile kanuni za pale juu ni sawa na kuziandika

  • EXA = (CIF+I/D) * 20% = CIF * 20% + I/D * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5% = CIF * 5% + I/D * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18% = CIF * 18% + I/D * 18% + EXA * 18% + EX * 18%

Sasa kimsingi swali ambalo hata mimi nimeshindwa kumjibu rafiki yangu...... ni halali kodi kutozwa kodi???? katika mlinganyo huo hapo juu inaonekana kuwa I/D (Import Duty ambayo pia ni kodi) lazima itozwe EXA, EX na VAT. Pia EXA (Excise duty for vehicles aged more than 10 years ambayo pia ni kodi) na EX (Excise Duty ambayo pia ni kodi) nazo zinatozwa kodi.
Nauliza tena hiyo ni halali??? Sheria zinasemaje kuhusu hili????... Nina hamu sana kujua jinsi sheria zinavyo sema... vinginevyo mimi naweza kusema hii si haki kwa watanzania kutoza kodi kwenye kodi.....

Maana mimi nilifikiri kuwa kila kodi itatozwa kutoka kwenye kiwango cha msingi (a base) kwa hapa tuna maanisha CIF ambayo hata TRA wenyewe kwenye valuation yao ya magari wanasema ndiyo inayopaswa kutoza kodi (taxable) lakini cha kushangaza wanatoza hata kwa kodi ambazo hazipaswi kutozwa kodi (non - taxable) ......
Mimi binafsi nilifkiri kanuni ya kodi ingekuwa kama ifuatavyo

I/D = CIF * 25%

EXA = CIF * 20%
EX = CIF * 5%
VAT = CIF * 18%

Halafu lingine la msingi ni kuwa, kwa nini EX na EXA ambazo ni kitu kimoja zinatozwa mara mbili? Kwa nini isitozwe mara moja tu? Kwa mfano ungeweza kusema Gari lenye umri wa chini ya miaka 8 Excise Duty ni 10% na Gari lenye umri wa zaidi ya miaka 8 Excise Duty ni 15% ili mlinganyo uwe kama ifuatavyo....

I/D = CIF * 25%
EX = CIF * Q% (Q inategemea umri wa Gari. < miaka 8 ni 10%; > miaka 8 ni 15%)
VAT = CIF * 18%

Wanajamii nikipata mawazo ambayo yanaegemea sheria nitafurahi zaidi.....

Naomba kuwasiilisha...

Mkuu wewe unatoka Dunia gani kiasi hujui matatizo yanayotupata tunaoagiza magari
kwa kifupi hizo ndio formula sijui walidesa wapi maana zimetulia kushinda hat za USA

haya ndio matatizo;
1. ucheleweshaji wa document kiasi kwamba watu wanapata Storage charge kubwa
2. kitu kidogo kwa mofisa wa TRA yaani usipotoa kitu kidogo utalia na ushuru utakaopewa au hata document itapotea ili kukuzingua tuu
3. Nchi imejaaliwa kuwa na bandari nyingi iweje all paper work zifanyiwe DAR yaani ukishusha mzigo Tanga inabidi mambo yote yafanyike Dar hii sijui ni akili au matope kutokana na ubinafsi wao

nawakilisha
 
Back
Top Bottom