wwww
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 350
- 252
Ndugu wanaJF,
Kumekuwa na kauli mbalimbali za baadhi ya viongozi kutoa matamko mfano; Wakuu wa Mikoa, Wilaya au Wenyeviti/ Mameya wa Halmashauri/Manispaa kwamba ni Marufuku kufanya kitu fulani kwenye eneo lake la utawala kwa kuita, MKOA WANGU, WILAYA YANGU, HALMSHAURI YANGU, MANISPAA YANGU n.k.
Hii kauli imekuwa ikinisikitisha sana mimi hasa ninapomsikia kiongozi kama Mkuu wa Mkoa anaita Mkoa ni wake eti kisa tu kapewa dhamana ya kuuongoza. Hivi hawa wanajua maana ya dhamana? Hivi mtu kama Paul Makonda anaweza kuumiliki mkoa wa Dar-es-salaam ukawa wake kweli, au nikutojitambua?
Nimewasikia watawala wengi tu kama Morogoro, Iringa na kwingineko na leo mkuu wa Mkoa mwingine kule Kigoma mwanajeshi mstaafu wa JWTZ naye eti anaumikili mkoa wa Kigoma hivyo anapiga marufufu shughuli za kisiasa kwenye mkoa wake. KWELI?
Inawezekana naye Rais wetu mpendwa sana JPM akajimilikisha nchi yetu ya Tanzania na kuanza kupiga marufuku mtu yeyote kufanya kitu chochote kwenye nchi yake mpaka pale yeye atakapoamue vinginevyo.
Wanajf naomba tujadili maana hawa jamaa wananitia kichefuchefu sana mimi kwa kujimilikishwa himaya zetu kirahisi rahisi tu.