Hizi kauli za kusema wapinzani hawajajiandikisha; wapinzani ni kina nani, na zina lengo gani?

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Kila mtu ana haki ya kuchagua mgombea anayemkubali, awe mwanachama wa chama chochote au asiwe mwanachama. Kuna watu wengi tu hatuna kadi ya chama chochote, lakini hii haitunyimi haki ya kuamua ni nani tumchague.

Nijuacho mimi, suala la kujiandikisha kupiga kura lilipokelewa vizuri sana na kila mwananchi. Sababu ni kwamba huduma nyingi za muhimu kama benki n. k,walihitaji kitambulisho kinachotambulika. Na kwa mtu wa kawaida ambaye hana passport, leseni ya udereva, na kitambulisho cha NIDA, ilikuwa ni rahisi kupata hiki cha mpiga kura. Hizi kauli za kusema wapinzani hawajajiandikisha, wapinzani hao ni kina nani? Au wanaishi porini wasipohitaji huduma kama benki?

Hili swali nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema,je wamepita kwenye daftari la mpiga kura na kuchunguza wakagundua kuwa wapinzani hawajajiandikisha? Wanawezaje kujua huyu ni mpinzani na huyu siye? Au kutokuwa na kadi ya CCM ndiyo upinzani?

Kwa taarifa yenu, wapo wafanyabiashara wengi wana kadi za CCM, Chadema, na ACT. Wanafanya hivi kwa kuogopa usumbufu ambao wangeweza kupata kwa kutokuwa CCM, ila mioyo yao iko mbali kabisa na CCM.

Pia wapo wenye kadi za vyama vya upinzani kama akina Mrema, Cheyo na wengine kama hao walioshirikishwa keki ya taifa, mioyo yao ipo CCM ila ni vile tu wakijiunga huko watamezwa na wanaweza wasionekane.

Nashauri propaganda zisizo na lengo zuri ziachwe na kila mtu apewe Uhuru wa kuchagua.Vyama vingi vipo kwa mujibu wa sheria na msivichukulie kama vikundi vya waasi.
 
CCM ina utaratibu wa kuwapa wanachama wake elimu ya uchaguzi kuanzia kujiandikisha, kuhakiki na kwenda kupiga kura.

Vyama vya upinzani vinaridhika na nyomi za masokoni.

Watu wanaohudhuria mikutano ya CCM ni wapiga kura wa CCM. Wanaohudhuria mikutano ya wapinzani ni just random people with no clear objective.
 
Angalia kijani na njano ilivyo tawala hapa ! Hawa ndo walliga kura! wanachama halisi na CCM kindakindaki

IMG_20200928_173707_458.jpg
 
CCM ina utaratibu wa kuwapa wanachama wake elimu ya uchaguzi kuanzia kujiandikisha, kuhakiki na kwenda kupiga kura.

Vyama vya upinzani vinaridhika na nyomi za masokoni.

Watu wanaohudhuria mikutano ya CCM ni wapiga kura wa CCM. Wanaohudhuria mikutano ya wapinzani ni just random people with no clear objective.
Una uhakika kwamba hao mliwafindisha hawana uwezo wa kuwachagua wapinzani?
 
Kila mtu ana haki ya kuchagua mgombea anayemkubali, awe mwanachama wa chama chochote au asiwe mwanachama. Kuna watu wengi tu hatuna kadi ya chama chochote, lakini hii haitunyimi haki ya kuamua ni nani tumchague.

Nijuacho mimi, suala la kujiandikisha kupiga kura lilipokelewa vizuri sana na kila mwananchi. Sababu ni kwamba huduma nyingi za muhimu kama benki n. k,walihitaji kitambulisho kinachotambulika. Na kwa mtu wa kawaida ambaye hana passport, leseni ya udereva, na kitambulisho cha NIDA, ilikuwa ni rahisi kupata hiki cha mpiga kura. Hizi kauli za kusema wapinzani hawajajiandikisha, wapinzani hao ni kina nani? Au wanaishi porini wasipohitaji huduma kama benki?

Hili swali nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakisema,je wamepita kwenye daftari la mpiga kura na kuchunguza wakagundua kuwa wapinzani hawajajiandikisha? Wanawezaje kujua huyu ni mpinzani na huyu siye? Au kutokuwa na kadi ya CCM ndiyo upinzani?

Kwa taarifa yenu, wapo wafanyabiashara wengi wana kadi za CCM, Chadema, na ACT. Wanafanya hivi kwa kuogopa usumbufu ambao wangeweza kupata kwa kutokuwa CCM, ila mioyo yao iko mbali kabisa na CCM.

Pia wapo wenye kadi za vyama vya upinzani kama akina Mrema, Cheyo na wengine kama hao walioshirikishwa keki ya taifa, mioyo yao ipo CCM ila ni vile tu wakijiunga huko watamezwa na wanaweza wasionekane.

Nashauri propaganda zisizo na lengo zuri ziachwe na kila mtu apewe Uhuru wa kuchagua.Vyama vingi vipo kwa mujibu wa sheria na msivichukulie kama vikundi vya waasi.
Ni mbinu za wizi wa kura hizo tujiandae kulinda kura zetu.
 
Back
Top Bottom