Hizi kampeni za Serikali ya JK za nini? Kizuri chajiuza... Mwenye macho haambiwi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi kampeni za Serikali ya JK za nini? Kizuri chajiuza... Mwenye macho haambiwi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ibrah, Jan 19, 2009.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Wadau, hivi karibuni kumezuka kampeni za kuisifia Serikali ya awamu ya 4. Mwezi Desemba TRA walitoa makala kwenye gazeti wakisema "Mafanikio ya awamu ya 4 katika ukusanyaji wa kodi. Wakatoa na takwimu lukuki kuwa kwa mara ya kwanza Serikali ya awamu ya 4 kupitia TRA imefanikiwa kukusanya kodi kubwa zaidi kuliko ilivyowahi kutokea!

  Mimi nakubaliana nao lakini mbona hatuoni matokeo ya ongezeko hilo kwa uchumi na maisha ya Watz? Au ni kama vile fedha hizo zaingia katika mifuko iliyotoboka? Pili, TRA watueleze ikiwa ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa tax base au ndo hizo kodi tunazokamuliwa sisi walala hoi huku Wafanyabiashar wakubwaa na makampuni yakikwepa? Kwangu mimi haiingii akilini kwa Kampuni mfano ya Coca cola, Pepsi Cola na Bia (TBL) kutopandisha bei za vinywaji ikiwa wameongezewa kodi.Labda wachumi mniabie inawezekanaje Makampuni hayo kuongezewa kodi halafu bei za vinywaji zisiongezeke maana ongezeko la kodi linapandisha gharama za uzalishaji ambazo lazima zifidiwe kwa mtumiaji wa mwisho kuongezewa bei, vinginevyo kodi wanazoilipa TRA si sahihi, wanatuibia!

  Pili, nnachokiona mimi ni TRA na Serikali kuendelea kutuumiza sisi Wafanyakazi kupitia PAYE maana kodi ya PAYE zimeongezeka na kwangu mimi kodi ninayokatwa inafikia karibu 25% ya mshahara! Sasa TRA watuambie ni mafanikio gani hayo ya kuzidi kutuumiza walipa kodi? Nadhani mafganikio halisi ni kama wangefanikiwa kuongeza idadi ya walipa kodi na si kuangalia kuwango cha ukusanyaji kwa kuwakamua walipa kodi ambao ni haohao waliotwisha mzigo wa mafanikio ya TRA. Wizi mtupu!

  Wiki ilopita TANROADS nao wakatuchapia kwneye magazeti juu ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya 4. Wakatoa na takwimu juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara iliyokamilika,iliyosainiwa na ambayo uilitakiwa iwe imekamilika mwaka jana na ile ambayo itaanza mwaka huu; ajabu ni kuwa iliyokuwa ikamilike mwaka jana ilikuwa bado!.

  Jana Waziri mmoja alikaririwa akisema Serikali ya awamu ya 4 imefanikkiwa kutoa ajira milioni moja! Yaani ni vioja; mbona hatuoni hayo ilia tunaaminishwa tu kwa kuambiwa na kulishwa takwimu ambazo hatajathibitisha?

  Sipingi wala sikatai kuwa kuna mafanikio lakini kinachonishangaza ni hizi kampeni za magazetini kutuambia juu ya mafanikio ya Serikali ya awamu ya 4 ila kinachonishangaza ni jitihda za kampeni zinazofanywa na viongozi wetu kujaribu kuifagilia Serikali.

  Msimamo wangu ni kuwa hawna sababu ya kutumia nguvu nyingi kutulisha takwimu na kutushawishi kwa habari na takwimu kwani MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA! Pia: CHEMA CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA! Watanzania tuna macho ya kuona na tunajua kilicho chema, hawana haja ya kupiga panda.
   
 2. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hawa jamaa nadhani hawaelewi kwamba language ya layman ni kuona sio statistics. Swali je hayo yanayosemwa yanaonwa?????????
   
 3. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukweli ni kwamba, mafanikio yanayosemwa na TRA yanatokana na ongezeko la kodi mbali mbali. Mfano ni ongezeko la kodi kwenye Road license. Sidhani kuwa wameongeza vyanzo vya mapato hata kimoja.

  Kuhusu PAYE, serikali imepunguza kwa kiasi kidogo sana (maximum 30,000/-) hasa kwa wale wa kiwango kikubwa cha mishahara.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  ....hawa TANROADS ndio wakae kimya kabisaaa.........maana miradi mingi ni hasara tu.

  Dr. Kawambwa if you are serious na TANROADS....ondoa huyo Mrema......maana toka aingie hasara tuliyokula ni unthinkable billions......
   
 5. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nafikiri serikali yetu inahitaji watu ambao ni creative and wanaoweza kufikiri zaidi katika kucreate sources mpya za kodi na sio kuongeza kwenye kodi zilizopo.

  kama tutaendelea na mtindo huo huo wa kuongeza kodi kwenye sources tulizonazo tu tutahua biashara za wadau. Maana mji kama mbeya ulirudi nyma kimaendeleo kutokana na TRA kuwakamua wafanyabiashara kuliko uwezo wa kulipa.
   
 6. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Moja;
  It is unfortunate kwamba kuna vitu unalazimika uonyeshe kwenye takwimu... mfano ujenzi wa barabara, hapo ulipo usiposafiri kwenda sehemu ambazo barabara zimejengwa wewe utajua je?

  Mbili;
  Utaratibu wa wizara na idara kutoa takwimu za mafanikio zilianza tangu mwaka wa Kwanza wa JK... kwa hiyo mimi naona ni muendelezo tu.

  Tatu;
  Kuna sehemu wamefanikiwa, lakini kuna sehemu tumeona kabisa hawajafanikiwa... mfano bandari, reli, ndege etc... kwa hiyo ni vyema kwa kweli tuwasikilize.

  Nne;
  Nakubaliana na wewe kwamba wafanyakazi wanakiona cha mtema kuni,wanalipa mara nyingi zaidi kuliko walipakodi wengine wote, kibaya zaidi wafanyakazi wa sector binafsi ndio zaidi kwa kuwa wao hawana marurupu lukuki yaliyo nje ya mishahara yao kama wale wa serikali.

  Tano;
  Hizo ndio zinaitwa siasa... unapamba kitu hata kama hakuna la zaidi... hata bila uongozi wowote ule kodi inatakiwa iongezeke kila mwaka kwa kuwa shughuli zinapanuka etc. etc.
   
Loading...