Hizi kadi ni za kurudisha huduma au ni siasa tu?

mirindimo

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
827
1,358
Waugwana habarini za kusoma uzi jamiini.Naona sasa kila huduma inawekewa kadi kwa sasa,kuna mwendokasi,sasa naona hospitali za serikali kama za wilaya ya Kinondoni wamekuja na kadi. Tusubiri kidogo mkuu wetu wa jiji anaweza sema na tuwe na kadi za nooniiino.

Hoja yabgu hapa, kwanini usiangaliwe mfumo wa kuunganisha hizi kadi zote kukawa na kadi moja itakayotumika kuanzia sehemu za kupata huduma za msingi za kijamii mpaka sehemu za biashara?

Sasa utakuta wallet inajaa kadi tu.

Ni wazo tu!

Nawasilisha
 
Kadi sahihi itakayofaa kwa huduma takribani zote, ni kile kitambulisho cha Uraia.

Kina taarifa nyingi sana kile, naamini serikali ikijipanga, wakakitumia kile tu, huduma zetu zitaenda poa.

Hatutalazimika tena kuwa na kadi nyingi mifukoni mwetu.

Tatizo serikali haijashtukia sijui, ama ni urasimu tu? Japo changamoto ni, bado wengine tena wengi tu bado hawajapata.

Ahsante!
 
Mkuu safi sana kwa kumkumbusha jamaa jaman wallet sio lazma uwek kadi zote tatioz Wabongo tunajaza Kadi hata hatuzitumii
Sasa ikitokea unataka kutumia na hujaibeba? Kwa sababu Bongo maisha bado hayajawa straight wote tunaishi maisha ambayo unaeza pata janga anytime na kama huna hizo kadi usipewe msaada.
 
Back
Top Bottom