robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 740
- 1,214
Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi Rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka.
Ni vibaya kwa rais kutoonesha imani na chanjo ya COVID-19 hadharani. Baadhi ya wasiwasi aliyonayo rais alistahili ibaki moyoni mwake na vyombo husika na siyo kulitangazia taifa. Yaweza kuwa yuko sahihi lakini ni vibaya kuweka uhakika mkubwa kiasi hicho kwa wananchi. Siyo wa kwanza, maana Afrika yupo rais wa Gambia aliwahi jidai kuoteshwa dawa ya UKIMWI, lakini ilikuwa ni gumzo la dunia juu ya kituko hicho.
Kwa nini Tanzania tuwe kituko cha Dunia kwa kukataa mawazo ya wanasayansi waliotangulia mbele yetu? Tutakapozidiwa tutakwenda wapi? Ni vibaya kumiliki sifa. Kama mwanzo tumebahatisha, tusizidishe imani kwamba Tanzania ni kiboko. Wengine wakiizuia wakati sisi tunabeza mbinu zao, tutakwisha.
Washauri munaosikilizwa na rais, jipangeni. Tunakoelekea miaka hii mitano ya kujiamini ni pabaya sana. Rais aandikiwe hotuba na kupunguza michapo ya pembeni na utani majukwaani, mengine yanatia aibu taifa. Siyo vizuri pia kuendelea na mifano ya ndoa, wanawake weupe, sijui nini tena.