Hizi hotuba za kisiasa za Rais Magufuli zitatuponza. Tuchague mambo ya kusema hadharani

robinson crusoe

JF-Expert Member
Oct 22, 2020
740
1,214
Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi Rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka.

Ni vibaya kwa rais kutoonesha imani na chanjo ya COVID-19 hadharani. Baadhi ya wasiwasi aliyonayo rais alistahili ibaki moyoni mwake na vyombo husika na siyo kulitangazia taifa. Yaweza kuwa yuko sahihi lakini ni vibaya kuweka uhakika mkubwa kiasi hicho kwa wananchi. Siyo wa kwanza, maana Afrika yupo rais wa Gambia aliwahi jidai kuoteshwa dawa ya UKIMWI, lakini ilikuwa ni gumzo la dunia juu ya kituko hicho.

Kwa nini Tanzania tuwe kituko cha Dunia kwa kukataa mawazo ya wanasayansi waliotangulia mbele yetu? Tutakapozidiwa tutakwenda wapi? Ni vibaya kumiliki sifa. Kama mwanzo tumebahatisha, tusizidishe imani kwamba Tanzania ni kiboko. Wengine wakiizuia wakati sisi tunabeza mbinu zao, tutakwisha.

Washauri munaosikilizwa na rais, jipangeni. Tunakoelekea miaka hii mitano ya kujiamini ni pabaya sana. Rais aandikiwe hotuba na kupunguza michapo ya pembeni na utani majukwaani, mengine yanatia aibu taifa. Siyo vizuri pia kuendelea na mifano ya ndoa, wanawake weupe, sijui nini tena.
 
Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka...
Kwani tuna Rais? nani kamchagua? Unadhani watanzaniawenye akili wanaweza kumchagua Rais wa hivyo?
 
Kwani tuna Rais? nani kamchagua? Unadhani watanzaniawenye akili wanaweza kumchagua Rais wa hivyo?
Tuache siasa za CHADEMA na CCM. Hata ujitoe kichwa huyo ndo rais. Rais yupo Boss! Upende usipende huyo ndo rais anayesaini kwa niaba ya nchi: Hata Uganda. Amin ndo alikuwa rais.
 
Tunaweza tukasikilizwa au hapana, ukweli ni kwamba rais anatakiwa kusaidiwa jinsi ya kuchagua maneno ktk majukwaa ya kisiasa. Tunaona jinsi rais anavyotumia jukwaa na kujisahau kwamba maneno ya rais hutafsiriwa na ofisi zote nchini na kuvuka mipaka...
Magufuli ni Raisi wa aina yake, siyo mtu wa kumumunya maneno kuogopa mabeberu watamfikiriaje. Kwa Africa hadi sasa sijaona Rais mwenye uthubutu Kama huo, maraisi wengi wa Africa ni wanafiki wanaojipendekeza kwa mabeberu wakiogopa kusitishiwa misaada.

Kuhusu hii chanjo ya Covid kusema ukweli ina walakini mkubwa kuhusu effetiveness yake. Ukiangalia muda uliotumika kutengeneza chanjo hii ni mfupi mno kuweza kufanya majaribio na kupata data za kutosha kujiridhisha kuhusu ubora na usalama wake.

Kitu kingine wakati hii vaccine inatengenezwa hapakuwa na aina mpya ya kirusi ambacho ni hatari zaidi kuliko aina ya kwanza.
Kwa hiyo unaona kabisa kutumia vaccine hii haitakuwa na matokeo mazuri Sana.

Kwa hiyo JPM alichosema ni kuwa tusiamini kila chanjo inayotengenezwa na wazungu.

Waafrika tuna tatizo moja hata Kama tumesoma hatuna confidence ya kuchallenge kazi zinazofanywa na wazungu kwa sababu ya Imani potofu kuwa kila wanachokifanya ni sahihi.

Kwa taarifa yako huu msimamo wa leo wa Magufuli umekuwa gumzo Afrika in a positive way, watu wengi wamekubaliana na msimamo wa Magufuli.
 
Uzuri wa Magu sio mnafiki. Ni vizuri ukaonesha your true colour na msimamo iwe upo sawa au umekosea. Watu design ya magu wanawavuruga sana wazungu kwani huwa hawakwepeshi maneno.
 
Back
Top Bottom