Hizi Home theatre zinatengenezwa kwa teknolojia gani?

Mkuu hiyo ni ni LG Home Theater? Kelele zinatoka wapi sasa
pale unapoona una kinu halafu wajuba wanakwambia unasikiliza nyenze.

jf jaman ah,inaweza kukujenga na kukuvunja vunja moyo.
hiyo ni kinu bana,sasa mtu ukute anataka akupambanishe na hili jini hapa chini,lazima yako ionekane ni kituko wakati sio kweli
Screenshot_20210113-195200__01.jpg
 
Hiyo ya 5.1 ni home theatre sio soundbar unaweza kupata kuanzia 1.2 mpk 1.5m ila uende na mtaalam wasije kukuuzia mdosho (fake). Kwenye hizi kitu tafuta original. Mie nina radio Sony nilinunua nikiwa Chuo Kikuu 2002 mpk leo inadunda kwa quality ile ile nilinunua duka la Sony (enzi hizo) Posta wenzangu walinicheka wao walikuwa wamenunua laki 300,000 aina hiyo hiyo Kariakoo mie nilinunua laki tano na wale jamaa wa Sony wakaniambia zao ni orijino hizo za Kkoo ni feki. Kweli mpk leo ni miaka 18 kitu kinadunda vile vile yamekufa yale madude ya DVD tu ila radio na tape inafanya kazi na nimeongezea kifaa cha bluetooth na flash imekuwa kama za kisasa tu
Kifaa cha kuunga Bluetooth kikoje na TSH ngap nakiihitaj
 
Mkuu nakubaliana na wewe kabisa , Ila baadhi ya watu wanaweza wasiielewe,
Music is about details ya kinachopigwa sio mdundo tu
Nilikuwa mpenzi sana wa earphone za soundmagic e10 , kwa wakati huo nilikuwa ndio chaguo langu bora , sasa Katka pilikqpilika za mtu mweusi Siku moja nikakutana na jamaa ana earphone za Shure , akaniazimisha !!! Ebana nilichoka playlist ni Ile ile yangu ya kila Siku, Ila details zilikuwa za kutosha na nilikuwa napata kila kitu katika half the volume niliyokuwa naitumia na earphone zangu. Kuna nyimbo moja jamaa Kama anakohoa flan huku akiimba nilikuwa Sijawahi kumsikia Siku zote Ila kwenye zile earphone nilisikia kila kitu

Nakubaliana na wewe mkuu , unaweza kudhani unasikiliza music kumbe unapigiwa makelele na mbaya zaidi usijue hilo
Umenena mkuu , music is good all the time ujue tunakosa vionjo vingi kwa SBB ya vifaa visivyo na ubora,
 
Back
Top Bottom