Hizi herufi (R) au (TM) humaanisha nini kwenye bidhaa?

Troublemaker

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
19,881
38,508
Habari zenu wakuu.

Kuuliza si ujinga. Kuna hizi herufi huwa tunakutana nazo kwenye bidhaa. Kama za electronic, vyakula n.k. Huwa zinakuwa ndogo kuliko maandishi husika, mara nyingi huwa kumezungushiwa kaduara ndani inakuwa "R" au "TM"
 
Trademark (TM) inamaanisha jina la bidhaa limesajiliwa kisheria huwezi kulitumia kwenye bidhaa yako. Ukilitumia ni kosa utashitakiwa, TM huwa mara nyingi kwenye brand maarufu ambayo iko kwenye soko sana hivyo kuepuka wajanja kupiga pesa kwa mgongo wa jina la brand wanapiga Trademark. R nadhani ni Registered, hiyo mara nyingi hutumika kuonyesha kuwa hilo jina limesajiliwa kibiashara so ni hatari kukopy ukalitumia kivyako example, BlueBand, etc
 
asanteni nyote mlioshiriki kunielimisha.

Na mimi nina swali kidogo.
Kwa nini makampuni mengi yanaishia na LIMITED...
Mfano: chapamaandazi limited
 
Na mimi nina swali kidogo.
Kwa nini makampuni mengi yanaishia na LIMITED...
Mfano: chapamaandazi limited
Neno limited msingi wake ni limit, weka mipaka, zuia. Sasa kampuni inapikua limited maana yake ni kua adhabu au makosa yanayofanywa na kampuni hayahusiani na wamiliki wa kampuni. Maana yake ni kua wamezuia, wameweka mipaka mambo ya kampuni yasiwahusu wamiliki wa kampuni. Mfano kampuni ikifilisika msije kwenda kuwadai wamiliki wa kampuni mkachukua vitu vyao hivyo wanaweka mipaka ya kampuni na vitu vyao binafsi.

Sijui kama utakua umepata mwangaza kidogo
 
Back
Top Bottom