Hizi hapa ndege za Fokker 28 na fokker 50 ndege za Rais TZ Magufuli

Mwaka jana niliandika uzi humu nikishaur ndege za rais zitumike kibiashara kama hazitumiki. Maana magufuli hatumii hizi ndege. Ila moods wakafuta. Waliona sijui ni wazo la kishenzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna nyuzi nililetaga humu miaka ya nyuma nikishauri "Trafiki wafungiwe mashine za EFD", mods wakafuta, labda walihisi ni wazo la kishenzi, haikupita mwaka tukaanza kuona EFD zikitumika kupiga faini badala ya notification za barabarani, nadhani kuna haja ya kuweka viwango elekezi vya elimu vya mtu kuajiriwa juwa mod.
Pia hata hii ya ndege niliileta humu jf, naona amefanyia kazi ushauri
Ndege iliyotulisha nyasi Watanzania na kupokelewa na Lowassa miaka ile inaendeleaje? - JamiiForums
 
A
Ila Magufuli pamoja na mapungufu yake lakini anapiga mzigo. Hakuna aliyetegemea ndani ya miaka mitatu kufanya haya. Sasa atoe uhuru wa siasa, bunge live na katiba mpya amalize kazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Akifanya hayo unayosema hata haya makubwa hataweza kuyafanya kwa sababu beberu atatumia uhuru wa siasa, bunge live na katiba mpya kutu-sabotage!
 
Uzuri hazibebi watu wengi hivyo hata kuwahamishia kwenye vipanga boi na dreamliner ni rahisi
Ratiba lazima itagomba sana. Hata ya watu kukalishwa Airport saa nyingi na inapoteza maana nzima ya kupanda ndege kuokoa muda.
 
Nafikiri ni suala la vipa umbele tu. Wale wengine baada ya Mwinyi sidhani kama wangeshindwa.

Pia waliogopa kudumaza uchumi wa ndani. Kuna foundation waliiweka pia iliyopelekea kuweza kutimiza malengo ya sasa. Mfano mkapa kuanzisha TRA, ndio inamuwezesha JPM atimize ya kwake. JK na barabara, nakifiri kwa kipindi chake asinge eleweka kama angekimbilia ndege.
yes nakubaliana na wewe kabisa bila ya foundations za waliomtangulia isingekuwa kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Nijuavyo Ndege wanacharge bei kubwa ili hata wakikosa Abiria iweze kuruka kwa wakati hata kama imejaza nusu.
Kwa kuwa Dar, Kilimanjaro, Mwanza na Kigoma bila kusahau ARUSHA na pengine Dodoma kuna Abiria wengi; Nawashauri waweke bei rafiki ili ndege ijae muda wote.
Nashauri wasijekusubiri hadi ije ndege Shindani ndio washushe bei. Biashara katika ulimwengu wa tatu kwa kiasi kibubwa huendesha na bei ndio vingine viangaliwe ...
 
nadhani kuna haja ya kuweka viwango elekezi vya elimu vya mtu kuajiriwa kuwa mod.

Kigezo cha elimu sawa lakini sidhani kama elimu ile ya vyeti itasaidia.

Kuna mifano mingi tu tunaona wateule maDr na PhD zao vitu wanavyofanya na hoja zao zinashangaza hadi msukuma akasema bora hata CPE holder ni bora kuliko wao (CPE =Certificate of Primary Education)

Kama @Maxence Mero angekua msomi wa viwango hivyo basi jf ingeishajifia siku nyingi au ingekua kama media nyingine za sasa.

Kujielewa na kujiamini katika imani yako ndio kigezo kikuu.

Kusoma wakati mwingine ni kama kuwa computerised au programmed kwamba huwezi fikiri nje ya box. Uko limited to 1+1=2 basi.

Lakini hebu fikiria kama sehemu nyingine ya dunia watu wakafundishwa 1+1=11 toka utoto wao. Siku mkikutana nani ataamini mwenzie ni sahihi??
 
Hizi ndio ndege za Rais kama ulikuwa huzijui, Rais Magufuli kasema zipakwe rangiView attachment 992019View attachment 992019View attachment 992020View attachment 992020
Pelek hizi kitu Songea na Mtwara haraka Mkuu....unachelewa sana...endelea kusikiliza watu wanasema nini,Mwisho tutakuzomea hujafanya kitu,Fanya Businesses analysis, kama inalipa oeleka Songea Mtwara ikalete Pesa....Endelea kusikiliza Wapinzani wako kwenye hili kama utafika.,..
Rais.Dr.John Pombe Magufuli...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom