Hizi hapa hatari tano(5) anazoweza kukutana nazo mwanao mtandaoni...

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Mara kadhaa kupitia wasaa huu tumezungumza juu ya matumizi ya mtandao na athari zake, chanya na hasi. Leo tunakutanabaishia aina tano kuu za hatari anazoweza kukutana nazo mwanao awapo mitandaoni na namna bora ya kukabiliana nazo ili kupafanya mtandaoni mahali salama kwa mwanao.

Maudhui yasiyofaa. Mtandaoni kuna maudhui chungu nzima kuanzia nyimbo za ibada hata filamu za utupu. Ingawa waandaaji wa maudhui wanaweza kuweka maangalizo juu ya umri wa nani anapaswa kuona nini – mtandao haubagui na mara nyingi hasa hapa kwetu watoto wetu wanatumia ama simu zetu, kompyuta na pengine ‘tablets’ zetu wazazi kuingia mtandaoni. Namna hii wanaweza kuangalia mambo tunayotumiwa na watu wazima wenzetu ama mambo ambayo tumekwisha yafungua wakaendelea ‘kufurahia.’

Kufanya mawasiliano na watu wasiofaa. Mtandaoni wapo marafiki – tunaowafahamu vyema na tusio-wafahamu hata chembe. Sisi wenyewe watu wazima kila uchao tunapokea maombi ya marafiki wapya. Mtoto vilevile awapo mtandaoni hili halikwepi. Wapo watu wasio-waaminifu ambao kutwa wanatafuta watoto wadogo kuwalaghai ama kuwarubuni kupitia picha za ngono ama hata kuwaibia ‘pocket money’ ambayo sisi wazazi tunavuja jasho kuwatimizia. Je unajua utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kuwa mtoto mmoja wa kitanzania anao marafiki mpaka zaidi ya 5,000 kwa wastani katika mitandao ya kijamii?

Mitandao inaweza kumuharibia mwanao sifa. Watoto, kama ilivyo sisi watu wazima, wanapenda kuwa maarufu. Umaarufu wa mitandaoni umewafanya watoto wapige picha wakiwa watupu, wakiogelea ama hata wakipata kumbato, mabusu na mambo kama hayo huku wenzao wakiwachukua filamu ama picha. Yote haya hupakiwa katika mitandao ya kijamii kwa minajili ya kupata ‘likes’ na maoni (comments). Bahati mbaya mtandao hausahau. Picha na filamu hizi zitadumu mitandaoni hata watakapohitimu elimu na wakawa ‘watafuta ajira’ ama hata viongozi katika jamii.

Matumizi yalopitiliza hadi kuleta athari za utegemezi wa mtandao. Upo usemi unaoibuka kwa sasa kuwa maisha hayawezekani pasi na mtandao. Hii kwa watoto ina maana kuwa wataathirika kimakuzi, masomoni, kiroho na hata kimahusiano. Itakuwa nadra kwao hata kujenga hoja wanapokuwa na marafiki hata kwetu sie wazazi wao. Marafiki wao takribani wote watakuwa penye ‘screen’ za kompyuta, n.k.

Athari za kibiashara. Upo ushahidi wa mzazi mmoja aliyeikuta picha ya mwanaye aloipakia mtandaoni katika mabango ya matangazo barabarani (billboards) alipokuwa safarini nchi jirani. Makampuni kwa sasa yamehamishia ‘vita’ ya masoko mtandaoni. Kila unapoingia kuperuzi unaulizwa ulipo (location), umri na hata mawasiliano yako binafsi. Yote haya ni mambo ambayo mtoto kamwe hawezi kuyakabili. Mara nyingi atagawa taarifa hizi kama njugu na mwishowe atakuwa ‘soko-mjinga’ la bidhaa lukuki hata zenye kuhitaji matumizi ya watu wazima pekee.

Ufanyeje? Badala ya kumnyima mtoto mtandao mpe mafunzo ya matumizi bora ya mtandao. Wewe ndiye mlinzi nambari moja wa mtoto wako. Mpe nyenzo ili kwazo ajikinge na majahili toka kote duniani mtandaoni. Anza kwa kujifunza wewe namna bora ya kutumia mtandao kwa miongozo chungu nzima inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano hapa kwetu Tanzania.

Vilevile makampuni mengi makubwa mtandaoni sasa yametia saini makubaliano ya kumlinda mtoto mtandaoni. Facebook, YouTube, Google na mengine. Soma sehemu ya vigezo na masharti ya mengi ya makampuni haya ili kuziba mianya ya wewe na mwanao kuingia katika tovuti zisizofaa hasa kama unatumia kifaa chako hicho na mwanao uwapo nyumbani.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
 
Nadhani njia sahihi ni kuwa na PG kila sehemu.

Kwenye TV fanya setup decoder za siku hizi ni rahisi kuset. Kwenye simu kuna app nyingi za kuwasaidia wazazi kujua mwanao anacho tazama.

Lakini mwisho wa siku hayo yote hayatasaidia kama hautajenga tabia njema kwa mtoto ajue kipi afanye hata kama haupo alipo.
 
Ila watoto wa saa hivi hatari wanajua mambo ya teknolojia kuliko watu wazima mfano mzuri Mimi na masister kipindi tulipokuwa wadogo tulikuwa tukichezea television ya nyumbani isionyeshe chaneli za taarifa habari ili tuangalie maigizo hiyo inadhihirisha namna gani tulikuwa tukijua teknologia kuliko wazazi wetu
 
Hakika mitandao ya kijamii imekuwa changamoto sana kwa watoto na jamii nzima kwenye maadili na kuiga tamaduni mbalimbali zisizo faa
 
Mkuu sana Sema Tanzania, nakubaliana nawe kwa asilimia 100. Tukiwa kama wazazi, tuna wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanakua katika kustawi kuliko kudumaa au kuharibika; kung'aa kuliko kuchafuka na kuwa na mema mengine. Hakika,watoto wetu wanakua kwenye dunia yenye changamoto nyingi kuliko hata wakati wetu.
Udai utahakikisha, hivi kama saizi upo hapo ulipo na mwanao ana simu yake chumban kwake, unajua anachokifanya?!!

kuna vitu vingine ni vya kumuachia mungu mwenyewe ndio anajua suruhisho lake, kwa akiri za kibinadam ukweli hauwezi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila kitu kuntu,Kazi ni kwa wazazi na walezi kuwaelewesha watoto njia sahihi ya kupita.
 
Hakika malezi yamekuwa magumu zaidi baada ya kuingia kwa utandawazi..Lazima tuingie ndani kabisa ktk kujua malezi na kuyatekeleza. Tatizo kubwa ni kwa wazazi kujiita wa kisasa..huu ndio ulimbukeni unaoangamiza familia zetu. Asanteni Sema Tanzania kwa jitihada hizi japo niwaombe muongeze juhudi ziadi kwani kizazi kijacho kiliza wengi.
 
Mara kadhaa kupitia wasaa huu tumezungumza juu ya matumizi ya mtandao na athari zake, chanya na hasi. Leo tunakutanabaishia aina tano kuu za hatari anazoweza kukutana nazo mwanao awapo mitandaoni na namna bora ya kukabiliana nazo ili kupafanya mtandaoni mahali salama kwa mwanao.

Maudhui yasiyofaa. Mtandaoni kuna maudhui chungu nzima kuanzia nyimbo za ibada hata filamu za utupu. Ingawa waandaaji wa maudhui wanaweza kuweka maangalizo juu ya umri wa nani anapaswa kuona nini – mtandao haubagui na mara nyingi hasa hapa kwetu watoto wetu wanatumia ama simu zetu, kompyuta na pengine ‘tablets’ zetu wazazi kuingia mtandaoni. Namna hii wanaweza kuangalia mambo tunayotumiwa na watu wazima wenzetu ama mambo ambayo tumekwisha yafungua wakaendelea ‘kufurahia.’

Kufanya mawasiliano na watu wasiofaa. Mtandaoni wapo marafiki – tunaowafahamu vyema na tusio-wafahamu hata chembe. Sisi wenyewe watu wazima kila uchao tunapokea maombi ya marafiki wapya. Mtoto vilevile awapo mtandaoni hili halikwepi. Wapo watu wasio-waaminifu ambao kutwa wanatafuta watoto wadogo kuwalaghai ama kuwarubuni kupitia picha za ngono ama hata kuwaibia ‘pocket money’ ambayo sisi wazazi tunavuja jasho kuwatimizia. Je unajua utafiti wa hivi karibuni ulionyesha kuwa mtoto mmoja wa kitanzania anao marafiki mpaka zaidi ya 5,000 kwa wastani katika mitandao ya kijamii?

Mitandao inaweza kumuharibia mwanao sifa. Watoto, kama ilivyo sisi watu wazima, wanapenda kuwa maarufu. Umaarufu wa mitandaoni umewafanya watoto wapige picha wakiwa watupu, wakiogelea ama hata wakipata kumbato, mabusu na mambo kama hayo huku wenzao wakiwachukua filamu ama picha. Yote haya hupakiwa katika mitandao ya kijamii kwa minajili ya kupata ‘likes’ na maoni (comments). Bahati mbaya mtandao hausahau. Picha na filamu hizi zitadumu mitandaoni hata watakapohitimu elimu na wakawa ‘watafuta ajira’ ama hata viongozi katika jamii.

Matumizi yalopitiliza hadi kuleta athari za utegemezi wa mtandao. Upo usemi unaoibuka kwa sasa kuwa maisha hayawezekani pasi na mtandao. Hii kwa watoto ina maana kuwa wataathirika kimakuzi, masomoni, kiroho na hata kimahusiano. Itakuwa nadra kwao hata kujenga hoja wanapokuwa na marafiki hata kwetu sie wazazi wao. Marafiki wao takribani wote watakuwa penye ‘screen’ za kompyuta, n.k.

Athari za kibiashara. Upo ushahidi wa mzazi mmoja aliyeikuta picha ya mwanaye aloipakia mtandaoni katika mabango ya matangazo barabarani (billboards) alipokuwa safarini nchi jirani. Makampuni kwa sasa yamehamishia ‘vita’ ya masoko mtandaoni. Kila unapoingia kuperuzi unaulizwa ulipo (location), umri na hata mawasiliano yako binafsi. Yote haya ni mambo ambayo mtoto kamwe hawezi kuyakabili. Mara nyingi atagawa taarifa hizi kama njugu na mwishowe atakuwa ‘soko-mjinga’ la bidhaa lukuki hata zenye kuhitaji matumizi ya watu wazima pekee.

Ufanyeje? Badala ya kumnyima mtoto mtandao mpe mafunzo ya matumizi bora ya mtandao. Wewe ndiye mlinzi nambari moja wa mtoto wako. Mpe nyenzo ili kwazo ajikinge na majahili toka kote duniani mtandaoni. Anza kwa kujifunza wewe namna bora ya kutumia mtandao kwa miongozo chungu nzima inayotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano hapa kwetu Tanzania.

Vilevile makampuni mengi makubwa mtandaoni sasa yametia saini makubaliano ya kumlinda mtoto mtandaoni. Facebook, YouTube, Google na mengine. Soma sehemu ya vigezo na masharti ya mengi ya makampuni haya ili kuziba mianya ya wewe na mwanao kuingia katika tovuti zisizofaa hasa kama unatumia kifaa chako hicho na mwanao uwapo nyumbani.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org

Kutokana na Uchunguzi wangu niliofanya kwa muda mfupi ni kwamba asilimia kubwa ya watanzania ikiwemo watu wazima hawajui matumizi sahihi ya mitandao .. watu wengi wanaitumia mitandao vibaya kwa kuweka hata mambo yao ya ndani /binafsi kwenye mitandao bila kufikiria madhara ya baadae kutokana na taarifa ulizoweka mitandaoni ....

pia niseme tu wazazi wanaweza kuwaelimisha watoto juu ya matumizi sahihi ya mitandao kwa maana sio kila kitu kwenye mitandao ni kabaya kwa watoto kuna application nzuri za watoto kwa ajili ya kujisomea, kupata taarifa za masuala ya afya ..na hata historia ya mambo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom