Hizi Hapa Faida za Bangi ikitumiwa ipasavyo

sumu-ya-panya

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
628
570
Mmea wa bangi una matumizi mengi ya matibabu, ujenzi, kutengenezea dizeli oganiki na pia hufumwa nyuzi zinazotumika katika ushonaji. Utafiti kuhusu mbangi unaendelea kufumbua matumizi mengine zaidi. Shida yake kubwa ni kusababisha uraibu.

Majani ya mmea wa kike wa Mbangi hutumika kutengeneza bangi. Bangi hutumika katika dawa ya kulevya kwa sababu inasababisha namna ya ulevi.
Mbangi ni mmea wa nyuzinyuzi ambazo hufumwa nyuzi zinazotumika katika ushonaji wa vitu tofautitofauti.
Mbangi, hasa spishi ya Cannabis sativa, hupasuliwa mbao, fito na vikingi za ujenzi.

Mbegu za Mbangi, hasa Hemp iliyo katika spishi ya Mbangi-mwitu, hutumika kama chakula
. Mbegu hizi zina proteini, madini, vitamini E na hata mafuta ya Omega-3 na Omega-6 yenye manufaa makubwa kwa mwili.
Mbegu za Mbangi aina ya Hemp ni halali kwa matumizi ya chakula katika nchi nyingi ikiwemo Uingereza.[6]

Kimatibabu sehemu tofauti za Mbangi hutumika kwa shughuli tofauti za tiba.
Mbegu za Hemp hutumika kupunguza ugonjwa wa moyo kwa vile hutoa nitriki oksidi inayopumzisha mishipa ya damu na kushusha shinikizo la damu.
Mafuta yatokayo kwa mbegu hizi za mbangi hutumika kutibu magonjwa ya ngozi.
Mbegu za Mbangi Hemp pia zina asidi aina ya GLA (Gamma-Linolenic Acid) inayotumika kupunguza athari za prolactini inayosababisha dalili za kabla ya hedhi (Premenstrual Syndrome) wakati wa kukatika uzazi (menopause).
Magonjwa mengine ambayo Mbangi una uwezo wa kutibu ni kama vile pumu, ugonjwa wa Parkinson, umbugiaji wa pombe kupindukia, woga wa kula (anoreksia nevosa), unyogovu, ugonjwa wa maungio ya mifupa (athritisi), gliomas, kifafa, shida ya kupumua usingizini (apnea) na glaukoma.
Mafuta ya CBD inayotolewa kutoka kwa mbangi yanauwezo wa kutibu wasi wasi (anxiety) na huzuni (depression).
Mbegu za mbangi pia zaweza kutolewa mafuta au dizeli oganiki inayoweza kutumika kwa jenereta au kuendesha injini nyingine za dizeli.
Utafiti unaendelea kuhusu uwezekano wa kutumia mbangi katika utengenezaji wa karatasi za kuandikia na kuhusu madhara yake kwa afya


Bangi si Mbaya sijui Serikali.Haijaona.faida zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom