Hizi habari za francis cheka zina ukweli gani??

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
16,615
38,588
Habari zinazosambaa hadi hivi mjini Morogoro ni hofu ya kupotea kwa bondia maarufu nchini mkazi wa Morogoro Francis Cheka.

Kwa mujibu wa watoa habari na marafiki wa karibu wa Bondia huyo ni kwamba eneo ilipotokea ajali ya lori la mafuta hapo msamvu ni jirani kabisa na “ofisi” yake iliyokuwa ikijihusisha na ununuzi wa chupa na madumu ya plastics yaliyokwisha tumika!

Habari zaidi zinasema bondia huyo alionekana katika eneo la ajali wakati wananchi wakipigania kuchota na kuzoa mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tanker hilo la mafuta ya petrol; Baada ya kutokea mlipuko wa moto kufuatia mafuta kushika moto hakuna aliyemuona Francis Cheka tena!!!

Mpaka sasa hivi ninapoandika taarifa hii Bondia Francis Cheka hapatikani nyumbani kwake, wala simu yake au mwili wake!! Huku marafiki zake wakiwa katika majonzi makubwa sana kwani inasemekana alienda katika koki iliokuwa ikitoa mafuta ili kuwazuia watu wasihatarishe maisha yao kabla Moto haujalipuka.

Sisi wapenzi wa Bondia huyu tunaliomba jeshi la polisi kusaidia kupata ukweli wa taarifa hii ya kusikitisha sana!!!
 
Wenahisi unaupungufu wamawazoyako weunahisi sisi tunaweza jua alipo au unatupima akili kwakuandika vituvisivyo vyamaana
 
NIMESIKILIZA KIPINDI CHA MICHEZO JANA USIKU CHA CLOUDS...NDUGU YAKE AKIWA KAMA MSEMAJI WA FAMILIA AMESIKITISHWA SANA NA HIZO TAARIFA ZINAZOENEA NA KUSAMBAZWA KUWA NDUGU YAO AMEFARIKI KWENYE HIYO AJALI...TAARIFA ZENYE USAHIHI NI KWAMBA CHEKA YUPO HAI MZIMA WA AFYA NA YUPO MSUMBIJI KWA SHUGHULI ZAKE BINAFSI ZA KIKAZI.....KWAHYO HIZO TAARIFA ZIPUUZWE
 
Habari zinazosambaa hadi hivi mjini Morogoro ni hofu ya kupotea kwa bondia maarufu nchini mkazi wa Morogoro Francis Cheka. Kwa mujibu wa watoa habari na marafiki wa karibu wa Bondia huyo ni kwamba eneo ilipotokea ajali ya lori la mafuta hapo msamvu ni jirani kabisa na “ofisi” yake iliyokuwa ikijihusisha na ununuzi wa chupa na madumu ya plastics yaliyokwisha tumika! Habari zaidi zinasema bondia huyo alionekana katika eneo la ajali wakati wananchi wakipigania kuchota na kuzoa mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye tanker hilo la mafuta ya petrol; Baada ya kutokea mlipuko wa moto kufuatia mafuta kushika moto hakuna aliyemuona Francis Cheka tena!!! Mpaka sasa hivi ninapoandika taarifa hii Bondia Francis Cheka hapatikani nyumbani kwake, wala simu yake au mwili wake!! Huku marafiki zake wakiwa katika majonzi makubwa sana kwani inasemekana alienda katika koki iliokuwa ikitoa mafuta ili kuwazuia watu wasihatarishe maisha yao kabla Moto haujalipuka. Sisi wapenzi wa Bondia huyu tunaliomba jeshi la polisi kusaidia kupata ukweli wa taarifa hii ya kusikitisha sana!!!
kwani inasemekana alienda katika koki iliokuwa ikitoa mafuta ili kuwazuia watu wasihatarishe maisha yao kabla Moto haujalipuka
 
Mungu mkubwa
Screenshot_20190814_183203_com.instagram.android.jpeg
 
Afadhali aise
NIMESIKILIZA KIPINDI CHA MICHEZO JANA USIKU CHA CLOUDS...NDUGU YAKE AKIWA KAMA MSEMAJI WA FAMILIA AMESIKITISHWA SANA NA HIZO TAARIFA ZINAZOENEA NA KUSAMBAZWA KUWA NDUGU YAO AMEFARIKI KWENYE HIYO AJALI...TAARIFA ZENYE USAHIHI NI KWAMBA CHEKA YUPO HAI MZIMA WA AFYA NA YUPO MSUMBIJI KWA SHUGHULI ZAKE BINAFSI ZA KIKAZI.....KWAHYO HIZO TAARIFA ZIPUUZWE
 
Wosia wa Mengi ndio wa kujadiliwa.. imekaaje awaweke kina Regina out
 
Back
Top Bottom