Hizi gharama za mawaziri kuishi hotelini zitalipwa na nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi gharama za mawaziri kuishi hotelini zitalipwa na nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Feb 20, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Baadhi wanaishi Ubungo Plaza ambako gharama ni dola za Marekani 105 kwa siku wengine wanaishi Protea ambako kwa siku ni kati ya dola za Marekani 155 na 180.

  Sababu wanazotoa,
  1. Nyumba walizopangiwa bado zinafanyiwa ukarabati
  2. Nyumba walizopangiwa bado zinakaliwa na mawaziri waliomaliza muda wao
  3. Nyumba za mawaziri zina masharti mengi ikiwemo kutolima bustani na kuweka mifugo(kwani huko mahotelini wanaruhusiwa kuweka mifugo?)
  4. Nyumba walizopangiwa ni ndogo n.k nk.

  Swali langu; ni kwanini mawaziri wakose uzalendo kiasi hiki kwa kuridhia matumizi makubwa wakati wengine wana nyumba zaidi ya mbili hapo hapo Dar?

  Na kwa nini serikali iendelee kupoteza mamilioni kwa siku pasipo na sababu za msingi haioni kuwa hayo pia ni matumizi mabaya ya kipato cha Taifa.

  Inauma na inakera sana kuona vitendo hivi vinafanywa na viongozi wa nchi masikini kama Tanzania ilhali serikali ikiangalia, tuseme wao si sehemu ya jamii kuwa kubana matumizi ni kwa watu wa kipato cha chini tu wao haiwahusu.

  Soma zaidi Nipashe Jumapili Home
   
 2. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #2
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu tutalipa mimi na wewe, tukigoma tunapigwa mabomu kwani ndio sera yao mpya japo inakuja kwa kisingizio cha ajali!
   
 3. M

  Mavunja Member

  #3
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nchi hii ni ajabu kweli kweli. Inawezekanaje tunaweza kuvumlilia uozo kama huu? Ukienda hospitali ya umma si ajabu ukaambiwa dawa hii au ile hakuna. Kisa bajeti ya kununua dawa ndogo. Na unaweza hata kufa kwa kukosa dawa. Lakini wafujaji wa fedha za walipa kodi wanapeta hata baada kupanga mpango mchafu wa awamu ya tatu ya CCM kuuziana wakubwa nyumba za serikali. Wale ambao bado wanawapta CCM benefit of doubt na kuendelea kuwapigia kura wajue wanachangia tuangamie nchi hii. Way forward tuhamasishane kuiongoa CCM, haifai.
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Luteni hao mwaziri unadhani wanaishi Blue Pearl au Protea?

  Thae fact is wanaishi kwenye "nyumba zao" halafu hiyo invoice ikilipwa wanagawana na wenye ma-Hotel pasu kwa pasu!
   
 5. Mageuzi

  Mageuzi Member

  #5
  Feb 21, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aibu na kichefu chefu cha JK na mawaziri wake,hana nia ya dhati kuokoa uchumi wa nchi yetu,
   
 6. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hili nalo ni jinamizi lingine linalochangia umasikini kwa watanzania. At the first place kwanini waliuziana nyumba za Serikali? na baadaye waje kupangiwa kwenye mahotel. Kuna siku isiyokuwa na jina nyumba hizo zitarudishwa hata kama itachukua muda gani
   
 7. Rugas

  Rugas JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,053
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135  ukweli mtupu huo mkuu!
   
 8. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Sintochangia hii thread mpaka unipe hayo majina ya Wateule walio katika hizo Hotel.Vinginevyo utakuwa uzushi kwani upelelezi tena wa usiku mpaka kujua ubavu wao unalala wapi ni issue si ya kitoto,lazima unawajua kwa sura na majina.Yalete tafadhari!
   
 9. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Makubwa haya.

  Nchi inajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.
   
 10. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ninyi mnawaita mawaziri, lakini kwa matumizi haya inaonesha wazi kwamba hawa ni waasi. Wameasi nchi na hawana maana yoyote. Pia vyama vya upinzani wapo wapi kuwasema watu hawa?
   
 11. B

  Bobby JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Grethinkaz sometimes tuna vituko sana sisi. Luteni katoa source ya hiyo taarifa yake kwanini umshushue hivyo? Si uplay part yako na wewe kwa kuitafuta hiyo source ili ujithibitishie? Otherwise kama huna huo muda si ungekaa kimya tuuuu?
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Feb 21, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Jamani..this is too low..
  Sitaki na siwezi kuamini
   
 13. K

  Kamuzu JF-Expert Member

  #13
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 998
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  maswali mengine muwe mnakaa nayo tu jamani, maana majibu yake ni dhahiri mno so ili kuepusha kuwaumiza wadanganyika moyo kauka, tusije tukafa kabla ya wakati wetu.

  kwa sasa tujikite katika kutafuta suluhu ya haya yote yanayotusibu, sababu tunazo za kutosha.... uwezo tunao wa kutosha.... tunachopungukiwa ni kimoja tu - UTHUBUTU!


  Amani yetu inatumiwa vibaya.
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  Feb 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Amini usiamini - Mawaziri hata sufuria za kupikia nymbani kwao zinanunuliwa na Serikali!
   
 15. B

  Bobby JF-Expert Member

  #15
  Feb 21, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,683
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Luteni kwanza nikushukuru kwa post nzuri inayojali maslahi ya nchi. Posts zako nyingi ziko kwenye mtazamo chanya wa kuipenda nchi yako-big up sana.

  Mbili nimehilight maneno hapo juu ya serikali na mengine yenye kufanana nayo. Binafsi huwa napenda sana matangazo ya USAID redioni, kwenye tv, magazeti na kwingineko. Kikubwa ambacho kinanigusa ni kile kibwagizo cha "Kwa hisani ya Watu wa Marekani-From American People" Ni ukweli kabisa kwamba hizo pesa huwa zinakuwa zimetolewa na serikali ya Marekani lakini source ya hizo pesa ni walipa kodi wa Marekani ndio logic behind. Mimi nadhani ifike mahali tuwe hivyo sisi pia. Badala ya kusema serikali inapoteza pesa tuseme kodi za watanzania zinapotea. Kuna watu ambao kwa sisi kuendelea kutumia neno serikali kunawafanya wadhani sio wao wenye hizo pesa so wanakosa uchungu nazo. Nitafurahi sana siku moja nikiona bango la ujenzi wa barabara linasomeka "Barabara hii inajengwa kwa kodi za watanzania" na serikali ya Tanzania kama ilivyozoeleka.

  So ni sisi tutakaolipa hayo madola huko kwenye hizo 5 star hotels ili hao wajinga na familia zao waendelea kuenjoy huko ilihali wahanga wa mabomu hawana hata sukari ya uji. Ni kodi zetu ndizo zitakazopotea na si pesa za serikali. Na ni wajibu wetu sisi kama watanzania kuzilinda hizo pesa pamoja kwamba kwa bahati mbaya hatufanyi hivyo.
   
 16. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #16
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu umenena vizuri,
  Tatizo kubwa tulilonalo watanzania wengi ni kutokujali au kukosa uchungu na kodi zetu tunazolipa, hatuna uwezo wa kukemea kwa kauli moja matumizi mabaya ya kodi zetu yanayofanywa na wale tuliowapa(japo wengine wamejipatia) dhamana ya kutuongoza pamoja na marafiki zao.

  Watanzania tufikie mahali tusimame pamoja pasipo kujali itikadi zetu tuwawajibishe tuliowaajiri kwa yale ambayo hatukuwatuma baadala ya kuandanama kuunga mkono hotuba ya kiongozi fulani aliyotoa, bali tuandane kukemea ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, milipuko ya mabomu na membo mengine yanayofanana na hayo. Nchi yetu tutaijenga wenyewe na si watu wa Marekani.
   
 17. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #17
  Feb 21, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mama,
  Pamoja na kwamba hutaki na huwezi kuamini, elewa kwamba nchi hii tunachezewa michezo michafu na serikali yenyewe!
   
 18. s

  salisalum JF-Expert Member

  #18
  Feb 21, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Unauliza anus ya kuku kwenye upepo? Au unauliza mawe wakati uko kwe milima?
   
 19. t

  tbetram Member

  #19
  Feb 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hali hii haiwezi kuvumilika.
  Matokeo ya uchaguzi ya 2010 yalionyesha watu wengi waishio mijini walipigia kura vyama vya upinzani.
  I believe watu walioandama na kuwaondoa madarakani marais wa Misri na Tunisia ni wakazi wa mijini. Hivyo hata katika Tanzania watu waishio mijini wanaweza kufanikiwa kuikomboa nchi hii kutoka mikononi mwa sisiemu bila ya kuwahusisha watu wa vijinini ambao ndio nguzo ya sisemu. Time for action​
   
 20. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #20
  Feb 21, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  KWANI ALIYEUZA NYUMBA ZA SERIKALIKIBABE NA KUWAGAWIA MAHAWALA ZEK NYMBA ZA SERIKALI HUMJUI, AU NDIO WOGA WA KITANZANIA KUMUOGOPA MTU KWA KUWA NI MAARUFU. hUYO NDIO ANASTAHILI KULIPA HIZO BILI
   
Loading...