Hizi "flyover" zetu tunazoambiwa zitadumu kwa miaka 100 kwa jiji kama Dar, nikiwa Rais wa nchi naziondoa

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Kwanza kimuonekano, njia panda ya TAZARA na njia panda ya Ubungo zote zipo sawa (Zime cross njia mbili kila moja). Ila moja ina flayover moja na nyingine ina mbili. Hii design ilitakiwa kuwa kitu tunaita "typical design" . Kwa kile walichofanya ni kama kuchafua tu mji kwa kuweka mazagazaga.

Mimi sipo kwa hilo any way. Shida yangu kubwa ni umbali zilioenda hizo flyover kutokea "Centre" yaani zinapokutana. Ni kichekesho kwa mji unaokuwa kwa kasi kama Dar.

Ile ya TAZARA ambayo ilizinduliwa nadhani haina miaka miwili imeshaanza kuelemewa na foleni ya magari ambayo yanatakiwa kuchepuka (Kwenda Buguruni n.k. Yanajikuta yanabana magari ambayo yalitakiwa kupita juu moja kwa moja. Flyover ambayo kutokea Centre haiendi hata umbali wa Km 1 si kichekesho hicho?

Kwanini Rais wetu aliondoa zile "designs" alizoacha JK? Hii kuharakia mambo ndiyo yale yale ya Dodoma kujenga ikulu kisha inakuwa chini ya kiwango kupita kiasi then unaamua kujenga nyingine. Ha ha ha!

Sasa Flyover inaenda umbali wa mita kadhaa kutokea centre kisha unatuambia eti itadumu zaidi ya miaka 100 ikiwa effective. Mfugale muogope Mungu ujue!

Hii design ya vi-flyover vifupi kama mbilikimo imepelekea pale Ubungo kutokea kituko cha aina yake badala ya barabara ya viwango. Siku za mbeleni watakaolaumiwa ni sisi wahandisi wakati kiukweli yupo anayeingilia mambo.

101478028_607591769847744_6068200760835505548_n.jpg

Picha: flyover ya Ubungo katika muonekano wake. Cheki kutokea centre flyover inaenda umbali gani?

Hapa si ni sawa na kutupa hela tu jamani!

Hapa kitakachotokea ni magari yanayochepuka kutokea upande wa Morogoro kwenda Mwenge na kuelekea barabara ya Mandela yatajikuta yakianza kuyabana yale yanayotakiwa kwenda na barabara ya Morogoro kuelekea mjini na vise versa yake hivyo hivyo.
 
Mwenge - moroko inafumuliwa au inapanuliwa boss?
Unapanua barabara bila kuitumia? Ile hela bora wangekula kwenye sherehe za uhuru kuliko alipoenda kuitupa pale Mwenge ona sasa miaka mitatu tu wamefumua tena!
 
G Sam,

Nilijua utawaza kuhamisha mji

Mji unaweza kuhama ndugu, acha uzezeta

Unaziangusha 200b Tsh za kodi na unaandika ujinga hapa?

Old city can remain as it is na unahamisha mji kwingine

Mnawazaga nini?
 
Akili za ufipa zimechanganyikana na kinyesi cha popo.

Nyinyi hata ofisi tu ya chama mmeshindwa kujenga eti mnaanza kujadili miradi na miundombinu ya nchi inayoboreshwa?
Mwambieni mbowe arudishe bil8.9 alizoiba mjenge hata ofisi kuu ya Chama
 
Back
Top Bottom