Hizi Faini Mahakamani badala ya kifungo,ni sawa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi Faini Mahakamani badala ya kifungo,ni sawa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Kellei, Jul 23, 2011.

 1. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Wakuu,nimekua nikifuatilia kwa muda mrefu hizi adhabu za mahakama,lakini napata tatizo kidogo.Kwa mfano gazeti la leo la mwananchi ukurasa wa 8 wameandika habari ya Raia watatu wa China ambao wamehukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja kwa kosa la kuajiri watu wasiokua na vibali vya kuishi nchini na kufanya kazi za ujenzi bila kibali cha uhamiaji.
  Kinachonitatiza hapo ni kwamba wanatakiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini.
  Swali langu ni kwamba,jela miezi sita =na shilingi elfu hamsini?
  Je hizi faini zinakokotolewaje ili kuwatendea haki?
  Kama mtu anaingiza kwa saa zaidi ya elfu 50 iweje hiyo ndiyo iwe faini ya miezi sita?
  Kwanini kipato cha mtu kisikokotolewe kwa mwezi then wazidishe kwa idadi ya hiyo miezi?
  Je mahakama zetu zinazingatia hali halisi ya maisha au wanatoa faini kulingana na sheria za miaka ya sitini?
  Msaada tafadhali.
   
Loading...