Hizi Cheki hizi zina matatizo gani.. miye sitaki..

funny people. topical indeed. hawa jamaa kweli wanastahili kuoana! very comical kwa kweli
 
Inawezekana ni ugonjwa wa familia kwenye tarakimu labda ndiyo sababu hata mtoto wao hajui kwanini wanamwita bilionea wakati yeye anasema ni milionea tu.

carelessness.jpg



leo mtaniuwa na kicheko. hiyo picha ya juu watu walisema ime-fotoshopiwa.
 
Nimelitafuta hili neno "cheki" kwenye kamusi yetu halimo. Ni tofauti kidogo na huo mfano wako. Tusonge mbele na mada yetu. Kosa kama lile sio Salma wala JK peke yao wanaweza wasiligundue. Vifijo, nderemo na shamrashamra zinazokuwa pale hazimpi nafasi mgeni rasmi kuliona hilo. Na wala halina madhara pande zote.

Kujipendekeza na kuwa puppet kuna viwango vyake, ila wewe mwenzetu umevuka viwango, nashindwa kuelewa unachokitetea wewe ni kitu gani! nenda kwenye website ya ccm ndio ya viwango vya mawazo yako.
 
This cheque will definetly be reffered to drawer! (kichekesho)!
Hii 'Salma Kikwete Saccos' ni tofauti na WAMA?

Kwani hujui ametafuta njia bora ya kuhamisha na kutorosha fedha za NGO WAMA kwenda kwenye saccos yake ni ufisadi tuu ,anajua kuna siku watataka kuhakiki mahesabu ya WAMA hawa mpaka waondoke watakuwa wamevuna fedha nyingi kuliko kawaida
kuhamisha kutoka hapa kuingia kwenye mifuko yao,tumeliwa hii ni familia ya viwavi
 
Originally Posted by Arafat
Swali la kizushi samahani sana wakuu!

Salma R. Kikwete; R stands for what?

Hiyo R inasimama km jina la BABA yake mzee Rashid wa Mkuranga

Nashukuru sana Mkuu? Salama Rashid Kikwete!! ajabu na kweli katika Afrika.

Mambo ya Mkuranga hayo! swali lingine tena la kizushi

Kwanini watu wanajadili mapungufu ya hundi hii kwa itikadi na tofauti ya vyama vyao?

Myt: Members wote wa JF ambao hutetea CCM kwa pamoja haoni upungufu wowote katika hundi hiyo hivyo wanaitetea na wale wa CDM wanaona tofauti kadhaa na wanaziainisha! Je tofauti ya vyama inaweza kuwa tofauti ya uwezo wa kuelewa na hata ikawa tofauti katika maono ya kitu kilichopo mbele ya mtu? Nilidhani tofauti inaweza kuwa katika Itikadi tu!

Mnataka kusema kwa mfano: swali 2x2 linaweza kuwa na jibu tofauti kutokana na chama cha mtahiniwa!

Hili nalo ni tatizo kubwa kwa nchni yetu
 
kaaah!! kumbe na cheki ya ujenzi wa shule ya mbweni nayo ni vituko? ha ha ha haaaa!! sihami tz ng'ooo....shubutuuuuu... nihame niende wapi ntakapopatia burudani nzuri km hiii??
 
Kujipendekeza na kuwa puppet kuna viwango vyake, ila wewe mwenzetu umevuka viwango, nashindwa kuelewa unachokitetea wewe ni kitu gani! nenda kwenye website ya ccm ndio ya viwango vya mawazo yako.
Wengi wetu humu ni hadi pale unapompopoa JK na familia yake, uikandie CCM na viongozi wake ndipo unaonekana uko huru, haujipendekezi sio puppet na sifa nyingine nzito kama hizo. Binafsi nitaitii dhamira yangu, nitausimamia ukweli hata kwa kupewa jina na sifa gani humu.
 
Wengi wetu humu ni hadi pale unapompopoa JK na familia yake, uikandie CCM na viongozi wake ndipo unaonekana uko huru, haujipendekezi sio puppet na sifa nyingine nzito kama hizo. Binafsi nitaitii dhamira yangu, nitausimamia ukweli hata kwa kupewa jina na sifa gani humu.

Wachina wanamsemo wao usemao a photo can speak a thousands words.

View attachment 29688
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom