Hizi Cheki hizi zina matatizo gani.. miye sitaki..

Mawaziri Hawa Ghasia na Malima wapo pia kwa nyuma wanafurahia maigizo!
 
Nimelitafuta hili neno "cheki" kwenye kamusi yetu halimo. Ni tofauti kidogo na huo mfano wako. Tusonge mbele na mada yetu. Kosa kama lile sio Salma wala JK peke yao wanaweza wasiligundue. Vifijo, nderemo na shamrashamra zinazokuwa pale hazimpi nafasi mgeni rasmi kuliona hilo. Na wala halina madhara pande zote.

WildCard not from you!

Kwamba "wala halina madhara"???? Mkuu week-end ilikuwa na nini mpaka usione hilo halina madhara??
Ni ujumbe gani mama Salma anautuma kwa jamii kwa kukabidhi hundi ambayo haieleweki??

Katika makosa ya kihasibu hili tutaliitaje??

Kama viongozi wetu wana wasaidizi waliochoka kiasi hiki ndio kusema Tanzania haina watu makini??
 
Si unaona hata wewe umekosea! Umeandika "Signaory" badala ya signatory.

nashukuru umekiri kwamba Mama Salma kikwete siyo makini na amekosea kama mimi nisivyo makini na nikagundua amekosea na wewe uliye makini ukaunga mkono hajakosea
 
Originally Posted by Arafat
Swali la kizushi samahani sana wakuu!

Salma R. Kikwete; R stands for what?

Hiyo R inasimama km jina la BABA yake mzee Rashid wa Mkuranga
 
WildCard not from you!

Kwamba "wala halina madhara"???? Mkuu week-end ilikuwa na nini mpaka usione hilo halina madhara??
Ni ujumbe gani mama Salma anautuma kwa jamii kwa kukabidhi hundi ambayo haieleweki??

Katika makosa ya kihasibu hili tutaliitaje??

Kama viongozi wetu wana wasaidizi waliochoka kiasi hiki ndio kusema Tanzania haina watu makini??
Jamani, huu ni mfano tu wa hundi. Sio hundi yenyewe ilookabidhiwa! Tunakomaa nalo hivi kweli? Kiuhasibu labda tuliite "Errors in amounts, such as recording one or more amounts incorrectly". Mifano hii ya hundi inaweza isiandikwe na wahasibu.
 
Nchi hii (Nnji hii) ya ajabu kweli kweli... yani mpaka mzee wa kaya ni mchakachuo tu
 
View attachment 29649

Hizi cheki zina matatizo yake.. Toka kwa Mjengwa Blog

hahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

mama weeeeeeeeeeee njooooo mwanao navunjika mbavuuuuuu!!

kwanza hakukuwa na haja ya kuandika neno shilingi.

kali zaidi: ni pale alipoandika 3, 800, 00 akimaanisha milioni tatu na laki nane. Mweeeeeeeeeeeeee mwalimu huyu Salma Ridhwani Kikwete. Mwalimu salma. duh, jamani mwalimu!
 
1.jpg

Hii ndo kibongo bongo mke wa muheshimiwa nae hayupo makini.

Kwa maneno ni shilingi milioni tatu na laki nane kule pembeni wamempiga changa la macho imeandikwa 3.800,00/= vitu vya kushangaza kama hivi utaviona bongo tu.
Kikosi cha intelenjisia na protocali sijui kimemdanganya mke wa rais?
Kwa hisani ya MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo

Naona Yupo Na dada yake ..waziri wa utumishi ..Ghasia...kweli familia ipo kazini..occation ya kukabidhi shilingi laki 380,000 ..inapata ugeni wa waziri wa utumishi ,mbunge ,first lady ..kweli kazi tunayo ..siasa at its best ..nadhani hayo mafuta tu kwenye magari yao ...ngoma,sherehe za makabidhiano na logistics zote ....ni bora tu wangeoka ili wawape msaada unaoeleweka...
 
Inawezekana ni ugonjwa wa familia kwenye tarakimu labda ndiyo sababu hata mtoto wao hajui kwanini wanamwita bilionea wakati yeye anasema ni milionea tu.

carelessness.jpg

Mi sina swali hapo, ngoja niitafute ile ya Exim Bank yenye maandish ya "Two hundred thousand" na tarakimu za "300,000/=. tehe tehe teheeeee
 
Hivi huko magogoni kuna shida gani? Kama wanashindwa kusoma cheque moja tu inakuwaje kwa mambo makubwa?

Nawaone Hawa Ghasia na Malima. Yaani viongoze wote hawa wamesafiri toka Dar kwenda kupokea cheqeu ya 3,800,00? huku si ndio kuuza ng'ombe ili ushinde kesi ya kuku?
 
Jamani, huu ni mfano tu wa hundi. Sio hundi yenyewe ilookabidhiwa! Tunakomaa nalo hivi kweli? Kiuhasibu labda tuliite "Errors in amounts, such as recording one or more amounts incorrectly". Mifano hii ya hundi inaweza isiandikwe na wahasibu.
Nafikiri huelewi watu wanachojadili hapa hawajadili cheki iliyopelekwa benki wanajadili kinachoonekana na umakini wa mtu mwenyewe na wasaidizi wake.
 
nashukuru umekiri kwamba Mama Salma kikwete siyo makini na amekosea kama mimi nisivyo makini na nikagundua amekosea na wewe uliye makini ukaunga mkono hajakosea
Kosa la Mama yetu Salma ni kutoisoma kabla hiyo hundi mfano kabla ya kupiga picha. Hakuiandika yeye.
 
Nafikiri huelewi watu wanachojadili hapa hawajadili cheki iliyopelekwa benki wanajadili kinachoonekana na umakini wa mtu mwenyewe na wasaidizi wake.

Nakubali. Kwa nini linataka kukuzwa hivi? Kwa kuwa huyo ni Mama Salma? Kosa la namna ile wangapi tungeliligundua na kushangiliwa koote kule?
 
Kosa la Mama yetu Salma ni kutoisoma kabla hiyo hundi mfano kabla ya kupiga picha. Hakuiandika yeye.

a dummy cheque is drafted from a template .... a template is a real cheque leaf attended by the cheque bearer.... usipotoshe... pumba ni pumba tu haziwezi kuwa choroko
 
Nakubali. Kwa nini linataka kukuzwa hivi? Kwa kuwa huyo ni Mama Salma? Kosa la namna ile wangapi tungeliligundua na kushangiliwa koote kule?
Anayelikuza siyo JF ni yeye anayetafuta publicity bila kuwa makini na vitu kama hivi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom