Hizi bahasha wanazopewa waandishi habari baada press release ni mafuta tu au ni takrima?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,979
Nimefanya utafiti kuhusu namna waandishi wa habari wanavyouza weno wao kwa makundi ya watu wenye fedha na taasisi mbalimbali. Mtanisaidia kukosoa ila Hali ipo hivi kwa kifupi.

1. Kila Waandishi wahabari wanapoitwa kwenye tukio lazima uone wakisaini bahasha za kaki na waandika majina, wanacholipwa wanakiita fedha ya mafuta na elfu 30,000 hadi laki tatu 300,000 kulingana na uzito wa habari na namna Mambo yanavyotakiwa yawe.

2. List wanayosaini waandishi hasa katika taasisi za umma na serikali haiwekwi kwenye kumbukumbu, fedha wanazolipwa uandikiwa au kuombwa kwa matumizi mengine. Nadhani hakuna fungu la mafuta ya waandishi wa habari.

3. Kwa Sasa waandishi wengi wanatumika kimkakati aidha kulinda pale kiongozi anapolinda ajira au anapotaka aonekane amefanya kazi. Hi imepelekea taarifa za eneo flan kurushwa kwa pamoja wakati mmoja, Mfano tukio linatipotiwa kwenye habari na vyombo vyote ila ukiliangalia haikuwa hot news kwa siku husika.

4. Hii tabia inatoka kwenye sekta za umma na Sasa imehamia kwenye NGO na baadhi ya taasisi za kimataifa hasa pale wanapotaka wafadhili waone kazi wanayofanya au kushawishi wapate fedha zaidi.

Kabla ya kuweka picha za waandishi wakisaini katika baadhi ya maeneo hasa wale wa nje ya Dar napenda kujua hii pesa ya mafuta ni malipo halali au Ni takrima?
 
Ngoja ninunue Mike yangu na kitambulisho nijidai muandishi nikale hizo pesa
 
Posho mkuu, bila hiyo kitu tungeishije mjini, media malipo yake madogo
 
Posho mkuu, bila hiyo kitu tungeishije mjini, media malipo yake madogo
 
Zinaitwa Brown envelope mzee..izo anakupa aliekualika uje usikilize press yake, huwa kuna posho
 
. Kila Waandishi wahabari wanapoitwa kwenye tukio lazima uone wakisaini bahasha za kaki na waandika majina, wanacholipwa wanakiita fedha ya mafuta na elfu 30,000 hadi laki tatu 300,000 kulingana na uzito wa habari na namna Mambo yanavyotakiwa yawe.

2. List wanayosaini waandishi hasa katika taasisi za umma na serikali haiwekwi kwenye kumbukumbu, fedha wanazolipwa uandikiwa au kuombwa kwa matumizi mengine. Nadhani hakuna fungu la mafuta ya waandishi wa habari.
Very soon itaitwa sanitizer
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom