Hizi akili za vijana wengi wa leo ningekuwa nazo miaka ile nadhani sasa ningekuwa nauza mkaa au naokota makopo

Mukulu wa Bakulu

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
4,052
12,906
JF bwana ina watu wana vituko sana. Ukiwa ni mtu wa kufuata mambo ya watu alafu uko humu basi unaweza kuishia kukata tamaa na kua masikini sana.

Humu kila mtu kwao wana pesa, kila mtu ana kazi nzuri mshahars mzuri, humu kila mtu ana gari nzuri na anaishi kwake, ana mke au girlfiend mzuri na humu kila mtu anapiga goli 5. JF is a place of perfect people, watu ambao wame-'make' kwenye maisha.

Tukirudi kwenye hoja yangu, unakuta vijana wengi humu wanaponda sana mtu kuishi kwa shemeji yake(mume wa dada yake), as if humu kila mtu anatokes kwenye family background iliyo vizuri. Mimi binafsi hapa nilipo ni kwa mkono wa shemeji yangu, miaka ile naamka kwetu hatukua na kitu cha maana ila bahati nzuri sister wetu akaolews na jamaa mmoja aliekua msomi na mwenye uwezo, hivyo ndugu zangu wengi ambao sasa wana nationalwise recognition walipitia kwake.

Jamaa ana moyo mzuri sana, ndugu zangu wakubwa waliokua shule kipindi hicho jamaa aliwasapoti kwa moyo mmoja na kuwa-encourage kusoma sana. Baadae mimi sister akanifuata hom nikaenda kusihi kwa mshikaji, jamaa ana moyo safi hakuwahi kum-mistreat sister mbele yangu wala kunitamkia jambo lolote baya, alinisapoti kwa kila kitu na mbaya zaidi miaka ile wanaanzisha bodi ya wanabadili mfumo wa mikopo vyuoni nikakosa mkopo, wakanishauri nibadili course nisome yenye mkopo ila jamaa akasema haina maana kumlazimisha mtu asome masomo asiyoyapenda kisa mkopo, jamaa akalipa.

Kiukweli hatutokei familia zenye uwezo sawa na hakuna mtu anaependa kwenda kuishi kwa shemeji yake bila sababu.

Hii JF ya leo ingekuwepo miaka ile na nikawa na mawazo ya kitaahira kama ya vijana wa leo labda nisingeenda kuishi kwa shemeji alafu sasa ningekua nauza mkaa au naokota makopo.

Mimi binafsi naona niseme nimeishi kwa shemeji yangu na sehemu ya mafanikio yangu na ya baadhi ya ndugu zangu yamechangiwa kwa kiwango kikubwa sana na shemeji yetu. Leo hii silipi deni la bodi ya mkopo, nina kazi inanilipa mshahara mkubwa na mambo kadhaa kwa sbaabu ya mchango wa shemeji yangu.

Bila mkono wa shemeji yangu labda ningekua mtu mwingine kabisa. Hebu tuwapongeze mashemeji zetu wote wanaopenda mafanikio ya ndugu wa mke wake.
 
Namuona shemeji anakuelekeza namna ya kula usimletee fujo kwake
Safi Sana muheshimu Sana
IMG-20170712-WA0022.jpeg
 
HUU NI UZI WA KIBWEGE SANA HUU TANGU JF IANZE.

LENGO LA MTOA MADA NI KUHAMASISHA WATU WAKAISHI KWA SHEMEJI ZAO KAMA YEYE-

MASELA PAMBANENI,
MSISADIKI HUU UJINGA.

KUSOMESHWA, KUPATA KAZI NA MSHAHARA MKUBWA
SIO JUSTIFICATION KUWA YEYOTE ATAPATA HIVYO KUPITIA MUME WA DADA'AKE!!!
 
HUU NI UZI WA KIBWEGE SANA HUU TANGU JF IANZE.

LENGO LA MTOA MADA NI KUHAMASISHA WATU WAKAISHI KWA SHEMEJI ZAO KAMA YEYE-

MASELA PAMBANENI,
MSISADIKI HUU UJINGA.

KUSOMESHWA, KUPATA KAZI NA MSHAHARA MKUBWA
SIO JUSTIFICATION KUWA YEYOTE ATAPATA HIVYO KUPITIA MUME WA DADA'AKE!!!
Dunia yote ya wasomi wanajua mtu anaeandika herufi kubwa hua ni taahira na ana matatizo ya mtindio wa ubongo.

Sass kama mtu unaandika kwa herufi kubwa, niseme nini tena?
 
1. Mtu kupigia kura ccm ni haki yake kikatiba, kama wewe ulivyo na haki ya kuchagua mwanaume wa kukuvua chupi.

2. Ulimchagua Lowassa, sasa yuko wapi?
Mtu timamu na akili zake kujisifu hadharani kwamba kuipigia kura ccm ni haki yake kikatiba ni ishara kwamba amepungukiwa akiba ya busara.
 
Humu kila mtu kwao wana pesa, kila mtu ana kazi nzuri mshahars mzuri, humu kila mtu ana gari nzuri na anaishi kwake, ana mke au girlfiend mzuri na humu kila mtu anapiga goli 5.


Mimi binafsi naona niseme nimeishi kwa shemeji yangu na sehemu ya mafanikio yangu na ya baadhi ya ndugu zangu yamechangiwa kwa kiwango kikubwa sana na shemeji yetu. Leo hii silipi deni la bodi ya mkopo, nina kazi inanilipa mshahara mkubwa na mambo kadhaa kwa sbaabu ya mchango wa shemeji yangu.

Bila mkono wa shemeji yangu labda ningekua mtu mwingine kabisa. Hebu tueapongeze mashemeji zetu wote wanaopenda mafanikio ya ndugu wa mke wake.

Kuhusu kila mtu kuwa na mke sio sahihi, JF wote hawataki kuoa ni wanazalisha tu singo mamas.... hapo mwishoni mshukuru sana dada yako.
 
2. Ulimchagua Lowassa, sasa yuko wapi?[/QUOTE]

Ha ha ha ha
 
Mleta mada inaonesha kuna mahali jiwe lilitupwa gizani likakupata, leo umeona uje u revenge!

Hata Tanzania inaitwa Nchi ya Ujamaa na Kujitegemea japo tunaenda kuomba kondom Marekani.
 
Kuna shemeji yangu naishi naye kwangu, ni graduate na mjanja tu nahisi yuko humu pia sema sijui ID yake.... usiwe na hofu shemeji utaishi kwangu hadi akili zikukae sawa.
 
Kwa hiyo wewe unataka kuturazimisha na sisi tukubaliane na akili zako za kimama ?
Mimi nasema hivi dume zima kulelewa na shemeji yako ni umama.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom