Hizi aibu zitaisha lini tz???ebu angalieni hii imekaaje....miss universe tz aibu...tupu..

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
4,208
3,097
Ikiwa imebaki siku moja tu kufanyika kwa shindano la miss universe kule Brazil(jtatu) imenibidi nikate tamaa kwa mwakilishi wetu kule (yaani Nelly Kamwelu).Nikiwa mmoja wa mdau na mkereketwa wa sifa nzuri kwa taifa letu ambaye nimekuwa nikifatilia maandalizi haya kule Brazil kwa kweli imenisikitisha baada ya kumfatilia mwakilishi wetu kule miss.Nelly Kamwelu.Nimekuwa nikimfatilia yeye na wawakilishi wetu wa africa haswa majirani zetu Angola na Botswana ambao kwa kweli wamepeleka vitu vya uhakika wajameni. Kwanza sijui ilikuwaje watanzania tukampeleka mrusi kutuwakilisha, hivi kweli tumekosa mweusi mwenzetu jamani??nawaambia safari hii tena tz imefanya kama walivopeleka muhindi Richa kipindi kile,tena safari hii ni mbaya zaidi kwani huyu mdada Nelly anaonekana kuiwakilisha urusi na wala si tz, hii ni fedheha kubwa jamani.Kilicho nifanya niumie sana ni kuona kuwa katika kuwakilsha vazi la taifa, wengine wote wamewakilisha mavazi yao kama waafrica wengine wamevaa nguo zao za taifa lakini cha ajabu huyu Nelly kapiga picha ya ajabu nawawekea hapa, hili vazi wanavaaga urusi na wala halina hadhi ya ki nchi ni aibu kubwa...yaani hata nguo za kanga wameshindwa kumpa huyu akavaa angalau kuonyesha anatoka Africa (Tanzani)?hata Richa kipindi kile alivaa nguo za vitenge, huyu mrusi safari hii ametuua kabisa wajameni.Pia hana mvuto hata chembe ukilingalisha na wadada toka majirani zetu hapa Angola na Botswana ni vitu adimu vya nguvu, safari hii kweli sitashangaa kusikia miss Angola au Botswana kashinda kwani ni watoto adimu na wakali kiyama.Kwa kuwaonyesha tu picha ebu angalieni hizi picha za huyu mrusi wetu Nelly alafu tumlingalishe na wenzake Leila (miss Angola) na Larona (miss Botswana) alafu muone aibu tuliyopeleka kule. fatilieni link hii kujua zaidi kinachojili kule miss universe brazil
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom