”Hiyo ndiyo serikali ya Magufuli, Serikali nitakayoiunda”

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,169
Mara nyingi Dr Magufuli amekuwa akitumia jina lake kama sehemu ya kampeni. Yaonekana kisha gundua kwamba neno CCM haliuziki kama jina lake la Magufuli. Wapambe pia wanalitumia jina na mafanikio yake, na mara nyingi sana wanakwepa kutumia jina la CCM ili kuonyesha mafanikio ya chama. Hatimaye Magufuli anatoa ahadi kama zile za J.K Nyerere Desemba 9, 1961. Leo hii Magufuli anaahidi kujenga viwanda bila maelezo tunayofahamu kwamba viwanda vilishajengwa vikafa!

Katika hali hii ya sasa, Nape naye kisha toweka kabisa ktk kampeni za uchaguzi. Yawezekana kakimbilia jimboni kujitetea lakini ktk kipindi hiki, ni aibu kwa chama ’kizee’ kama CCM kujivunia amtendo ya waziri mmoja tu badala ya mafanikio ya chama ktk miaka zaidi ya 50 ya utawala. Hii inaonyesha tuendako kwa utawala wa chama hiki ni matatizo tupu.

Nashauri wana CCM kama ilivyofanya KANU, hameni chama. Ingieni vyama vingine na kuachana na jina la CCM. Hili jina haliuziki tena.
 
mara nyingi dr magufuli amekuwa akitumia jina lake kama sehemu ya kampeni. Yaonekana kisha gundua kwamba neno ccm haliuziki kama jina lake la magufuli. Wapambe pia wanalitumia jina na mafanikio yake, na mara nyingi sana wanakwepa kutumia jina la ccm ili kuonyesha mafanikio ya chama. Hatimaye magufuli anatoa ahadi kama zile za j.k nyerere desemba 9, 1961. Leo hii magufuli anaahidi kujenga viwanda bila maelezo tunayofahamu kwamba viwanda vilishajengwa vikafa!

Katika hali hii ya sasa, nape naye kisha toweka kabisa ktk kampeni za uchaguzi. Yawezekana kakimbilia jimboni kujitetea lakini ktk kipindi hiki, ni aibu kwa chama 'kizee' kama ccm kujivunia amtendo ya waziri mmoja tu badala ya mafanikio ya chama ktk miaka zaidi ya 50 ya utawala. Hii inaonyesha tuendako kwa utawala wa chama hiki ni matatizo tupu.

Nashauri wana ccm kama ilivyofanya kanu, hameni chama. Ingieni vyama vingine na kuachana na jina la ccm. Hili jina haliuziki tena.

nasikia nape atapewa uwaziri wa mambo ya nje kama magufuli akishinda,kitu ambacho hadi sasa ni kigumu,ati kwa kuwa ni mropokaji sana,ili kulitembeza bakuli vizuri
 
ccm ilifia mikonon mwa makamba mbna

Yes! Nadhani forum kama hii ingetumika vizuri, mengi yangeokolewa. Binafsi sina uadui na CCM, lakini sitegemei kushabikia chama kisichotaka kukubali ukweli.

Haiingii akilini chama kizee kama CCM kupoteza umaarufu bila kujifahamu. Tatizo ilikuwa ni kuwa na katibu mkuu ambaye hakujua majukumu yake. Katibu mkuu ndiyo ubongo wa taasisi na siyo kufanya kazi kama mwenezi. Kuwa mtu wa vijembe na mipasho. Ofisi yake ilistahili ifanye kila aina ya utafiti na kuona mbele.
 
Ni aibu kubwa kwa chama kutembelea ndoto ya waziri - nyota ya mtu. Ni aibu na fedheha sana.
Je ataunda serikali na malaika kama Gabreli, n.k?
 
1. Lowassa anatumia jinalake au la ukawa?
2. Kwahiyi kama viwanda vya kipindi cha ujima vili fail, inamaanisha tusijaribu tena?
3. Mbona chadema wanajivunia jasho la mtu mmoja (Dr Slaa) kwenye kuimarisha chama?
4. Tatizo likowapi kama Nape akiwa waziri wa mambo ya nje? Au una wivu wa kike?
 
nasikia nape atapewa uwaziri wa mambo ya nje kama magufuli akishinda,kitu ambacho hadi sasa ni kigumu,ati kwa kuwa ni mropokaji sana,ili kulitembeza bakuli vizuri
Kiingereza chenyewe hajui kuongea labda uwaziri wa jinsia na watoto
 
1. Lowassa anatumia jinalake au la ukawa?
2. Kwahiyi kama viwanda vya kipindi cha ujima vili fail, inamaanisha tusijaribu tena?
3. Mbona chadema wanajivunia jasho la mtu mmoja (Dr Slaa) kwenye kuimarisha chama?
4. Tatizo likowapi kama Nape akiwa waziri wa mambo ya nje? Au una wivu wa kike?

Tuache mapenzi, tushabikie na ukiona unayemshabikia kashindwa, hama haraka.
Ni kweli mabango yote sasa yanasomeka Chagua Magufuli. Miaka yote yaliandikwa Chagua CCM. Huwezi kumuleta mtu kama Makamba eti asidie kampeni.

Unatoa ahadi ya kuanzisha viwanda wakati miaka michache uliuza viwanda na kusema serikali imejiondoa ktk kuendesha viwanda. Sasa imerudi tena? au kujenga maana yake nini?
 
nasikia nape atapewa uwaziri wa mambo ya nje kama magufuli akishinda,kitu ambacho hadi sasa ni kigumu,ati kwa kuwa ni mropokaji sana,ili kulitembeza bakuli vizuri

Waziri kama huyo atupeleke wapi jamani! Bora tuhame sayari hii.
 
Tuache mapenzi, tushabikie na ukiona unayemshabikia kashindwa, hama haraka.
Ni kweli mabango yote sasa yanasomeka Chagua Magufuli. Miaka yote yaliandikwa Chagua CCM. Huwezi kumuleta mtu kama Makamba eti asidie kampeni.

Unatoa ahadi ya kuanzisha viwanda wakati miaka michache uliuza viwanda na kusema serikali imejiondoa ktk kuendesha viwanda. Sasa imerudi tena? au kujenga maana yake nini?

huo Ni utapeli mkuu, kama ilivyozoea CCM
 
Back
Top Bottom