'Hiyo Internet Ndio Kitu Gani, Mie Hata Sikijui' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Hiyo Internet Ndio Kitu Gani, Mie Hata Sikijui'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 12, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Bibi mwenye umri wa miaka 75 wa nchini Georgia ametiwa mbaroni kwa kuzikosesha nchi za Armenia na Georgia internet baada ya kuzikata nyaya kuu zinazopeleka internet kwenye nchi hizo, alipoulizwa kwanini amefanya hivyo alijitetea kuwa hajui hata hiyo internet ndio kitu gani.
  Katika gumzo la kesi ambayo imewavutia watu wengi duniani, bibi Hayastan Shakarian mwenye umri wa miaka 75 huenda akahukumiwa kwenda jela miaka mitatu iwapo atapatikana na hatia ya kuzikata nyaya kuu zinazopeleka internet nchini Armenia na Georgia.

  Bi Shakarian huku akiangua kilio alijitetea kuwa hajui hata hiyo internet ndio nini na kwamba yeye alikuwa porini akikata kuni wakati alipozilima nyaya za fibre optic zinazosafirisha internet kwenda nchini Armenia.

  Tukio hilo lililotokea machi 28 mwaka huu, lilipelekea asilimia 90 ya watumiaji wa internet nchini Armenia kukosa internet kwa masaa 12.

  Bi Shakarian ambaye anaishi kwenye kijiji cha watu masikini chenye maendeleo duni cha Armazi kilichoko kilomita 15 toka mji mkuu wa Georgia, Tbilisi, alijitetea kuwa yeye ni mwanamke fukara ambaye hana uwezo wa kutenda kosa hilo kubwa la jinai.

  "Sijui hata hiyo internet ndio kitu gani", alilalamika bibi huyo wa miaka 75.

  Bi Shakarian amefunguliwa mashtaka ya kuharibu mali na kama atapatikana na hatia huenda akahukumiwa kwenda jela miaka mitatu.

  "Mama yangu hakuzikata nyaya za internet makusudi, anaangua kilio wakati wote anaiogopa sana kesi aliyofunguliwa", alisema Sergo Shakarian, mtoto wa kiume wa bi Shakarian.

  Ingawa kampuni inayosambaza internet imedai kuwa nyaya zake za internet zilikuwa zimelindwa vizuri ili zisiharibiwe, hii si mara ya kwanza Georgia kukosa internet baada ya nyaya kukatwa kwani mwaka 2009 kibaka mmoja alizikata nyaya hizo za internet katika dili lake la kuiba nyaya za umeme.


  5594094.jpg
   
 2. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Hilo ndio tatizo la matabaka. Wengine wanaishi maisha ya juu sana, wengine kwenye ufukara ulio topea.
  Bibi huyo angekuwa na uwezo wa kupikia gesi hayo yote yasingetokea.
   
 3. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Maskini wamsamehe bibi wa watu
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,473
  Likes Received: 4,130
  Trophy Points: 280
  Kumbe na huko nao wanapikia kama huku kwetu Kavifuti?
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaaaaa wanazagaa kuni!!ila mpaka supermarket unakuta kuni zinauzwa ila kitu ambacho sijakiona ni mkaa
   
Loading...