Hiwezekani tukawa na bunge lenye zaidi ya nusu ya wabunge waliochagua kuwa wajinga hivi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hiwezekani tukawa na bunge lenye zaidi ya nusu ya wabunge waliochagua kuwa wajinga hivi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Jun 30, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 23,757
  Likes Received: 1,388
  Trophy Points: 280
  Kwa anayesikiliza bunge ataona jinsi wabunge wa walivyoamua kuwa wajinga.wabunge wengine wanatukana matusi,wawaitana kuwa wenzao hawana maadili sijui maadili gani?Ukishakuwa mbunge umeenda fanya kazi, na katika kazi ni kama katika ndege,hakuna kusimama kupisha wakubwa.bunge limekuwa na umbea na uzushi usiokuwa na fikra.Wanasimama akina wazee, wamekuwa ktk serikali bila ukomavu.Wanasifia na kusalimu mlolongo mrefu wa ndugu, jamaa, marafiki?mahawara halafu na waume zao.Spika haoni hilo ila akisimama mpinzani mama anang`aka ,anaongea hata kitu kisicho husu mwongozo.wabunge wanawarukia wenzao wenye busara.bado mwishowe anahukumiwa aliyerukiwa.

  Haiwezekani hili likafanyika na raia tukabaki na mashaka tuu bila kujiaminisha kuwa hawa wabunge hasa wa CCM wamekuwa vichaa.hawajui haki za binadamu, hawana uzalendo,wala hawajui madhara ya matendo na maneno yao.Haiwezekani mawaziri wote wasijue kuwa Pinda alipaswa jiudhulu hapa.Migogoro ya madaktari tangu mwanzo alichemsha mara 2 wakawatoa kafara wengine,Pia kadanganya bunge kuhusu Arusha.bado wabunge wote wa CCM wanamshukuru na kumsifu wa kuwaongoza.
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 26,314
  Likes Received: 4,756
  Trophy Points: 280
  Ndo hivyo sasa tutafanyaje!! unashikwa hasira mpaka unataka lia..
   
 3. paty

  paty JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,196
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  tujilaumu wenyewe kwa kuwachagua hao wana sisiemu, tujilaumu wenyewe kwa kushindwa kulinda kura zetu , kwa sasa nadhani inabidi tutumie pressure groups kuwa challenge hawa mafisadi kwenye majimbo yetu , labda itasaidia kubadili mitazamo yao hawa vitambi kutoka kwenye uchama mbele kwenda kwenye utaifa kwanza, ingawa akili zao haziwezi kuongezeka kwani washachokaa, wanasinzia tu na kuongea kama hawana normal IQ
   
 4. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,660
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kiini cha udhaifu wa wabunge ni ninyi watanzania wenyewe!! Mnapiga kura kama vipofu, kisha mnalalama kama vichaa!! Hao si mliwachagua ninyi wenyewe?? Mliendekeza ushabiki wa Yanga na Simba kwenye siasa bila kuangalia uhalisia wa mambo!!

  Mlipodanganywa kwa chumvi, kanga na vikofia vya kijani mkakodoa macho na kuduwaa mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango!! Akili zikawaishia mkawapa kura vibaka!! Sasa tulieni mnyooshwe vizuri hadi hapo mtakapopata mang'amuzi mwaka 2015.
   
 5. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,964
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  wanaopoteza muda kwa kuomba miongozo huwaoni? Danganya wijinnga wenzi
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,605
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Wengi wao ni wakatoliki ,sasa sijui tusemeje zaidi ya mnavyowaponda, nashangaa !!
   
 7. kelvito

  kelvito JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe msengerema!
   
 8. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mentally Castrated na Udini.
   
 9. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,790
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Ukatoliki umeingiaje hapo?ukinyamaza ni busara pia
   
 10. l

  lebabu11 JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2010
  Messages: 1,322
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 180
  Mfumo wetu wa kuwapata viongozi umesababisha kuwapata wenye IQ za chini ya kiwango, na kwa bahati mbaya sana wanaendelea na wataendelea kurithisha uongozi kwa watoto na jamaa zao wenye viwango hivyo hivyo kama hatua muhimu hazitachukuliwa na jamii kudhibiti hali hiyo!
   
 11. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,500
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  We nahisi umepungukiwa na akili mbili.
  WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
   
Loading...