Hivii, "Mchawi" wa Bilioni 1 atakuwa na CAG au Musiba???

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,466
2,860
1 Bilioni TZS mkopo kwa ajili ya SACCOS mara hii mmoja wa wajumbe wa cabinet kawa implicated kwa namna moja au nyingine.

Wakati mmoja Humphrey Polepole alieleza vyema kuwa mahakamani wana-deal na legality. Kisiasa wana-deal na legitimacy.

Legality ni ngumu sana kuwakamata watu, ndiyo maana kuna wazee wetu hapa walificha vijisenti visiwa vya watu huko, wakavuta mgao tena wa akina Seth, bado wako "kitaa" na huenda isiowe rahisi taasisi ya kupambana na mlungura kuwa “implicate”.

Legitimacy hapo ni namna gani maji safi yanaweza kutupiwa taka mtu akawa implicated. Au pengine “hapo zamani za kale” kuna namna mtu bila kujua kesho alihusika kwa namna moja au nyingine kuchafuka, bila kujua kesho nuru itakuja na mambo ya kizani hayatafichika tena.

Siko hapa kumtetea mtu au kumlaumu mtu. Kuna siku Yesu aliletewa mwanamke aliekutwa kwenye actual act ya “lile tendo”. Wale wanaume wakampeleka yule mama kama mkosaji wakitaka atoe hukumu. Mnazareth yule, akijua hawa jamaa wote sio wasafi kiviileee, akatumia falsafa rahisi, yule ambae hajawahi kutenda dhambi, basi awe wa kwanza kutupa jiwe. Wale wanaume wote mioyo ikawachoma, wakalala mbele.

Story zinazoendelea kwenye vichwa vya Watanzania, ni maswali mengi na pengine majibu yanatabirika.
Je, mjumbe wa cabinet “ataliwa kichwa”? Au anaweza kuachwa aendelee na utumishi katika huku akitembea na gari lenye kupepea bendera ya Taifa? Sisi tulio kitaa, hatuna cha kusema zaidi ya kusubiri mamlaka ya uteuzi ifanya maamuzi. Kama atabaki ewaaa. Itakuwa ka-save. Vinginevyo Gerson Msigwa “atatupia” breaking news yenye “letterhead ya magogoni” mtaa wa Rais wa Marekani mwenye nasibu na Kogelo.

Huenda SACCOS toka jimbo la mjumbe wa cabinet kama wangekuwa na good business/investment model, bila shaka mkopo wanajimbo wangekuwa washarudisha na riba juu. Madhambi yao yangeweza kusamehewa. Ila kama fedha ilizama kwenye kukopa na kukopeshana, dah… sijui itakuwaje, maana "mfalme wetu" hataki kabisa kuona fedha zinapotea hovyo.

Ushauri kwa mifuko na mabenki. SACCOS haitawatoa Watanzania kwenye umasikini kama zilivyo fedha za 10% ya collection za halmashauri. Sio rahisi kama inavyodhaniwa kuwa na biashara endelevu bila organized systems za kibiashara/uwekezaji.

Nwashauri mtafuteni Watanzania wenye akili na wenye business/investment models ambazo zishakuwa proven ndani na nje ya Tanzania. Ikiwezekana wawe na consultant (toka huko nje sio hapa) ambae anaweza kusimamia uwekezaji au biashara yao. Fedha zenu za mkopo zitarudi na mtapata wanachama wanaochangia kila mwezi. Ila hii ya mikopo ya vikundi toka imeanza, inasaidia watu wasukume siku kuwa busy na biashara ya “hand to mouth”.

Mkiwa fair, toeni call for proposal. Ila mkitegemea Watanzania waje na collateral au bank statement yenye 50% ya wanachokusudia kukopa, hata wakileta fedha zitazama maana wanafanya biashara za kujikimu.

Kwa mahitaji ya soko la Tanzania na kusini mwa jangwa la sahara, mifuko ya pensheni ingesaidia sana kuwa hata bila mdhamini kwa kampuni kuanzisha uwekezaji ambao wanaotaka kuanzisha wana mkakati wa kibiashara na wana wadau wanao ambao wapo kwenye game ya hiyo biashara au uwekezaji ambao watanzania wanataka kuanzisha. Tumpeni fursa "Mfalme wa magogoni" awe busy kufungua viwanda ili kodi iongezeke, collection za pensheni nazo zitaongezeka na hata wala bataa pia waongezeke.

Tunahitaji fikra mbadala ili tukue kiuchumi/kibiashara arithmetically kwa kuanzia and then twende exponential growth Vinginevyo, kuna hela zipo, hata wastaafu wakipewa bado kuna zingine zitabaki zinakuwa zimekaa tu kwenye mabenki na account zinasoma. Kwa kuwa menejimnet zilizopita hawakuwa more creative, wao wakadhania majengo ni habari ya mjini.

Kumbe kuna watu wanaweza kuanzisha kampuni hata wasipopewa hela mkononi, wangeweza kukaa na nyie ili fedha zikawa kwenye uwekezaji ambao soko lake lipo ndani ya TZ na SADC kwa kuanzia ili kukuza mzunguko na kutanua wigo wa ajira sio mikopo ya SACCOS. SACCOS toka zimeanza watu wanakopa kusomesha watoto, kujenga nyumba na sio kuwekeza kwenye biashara zenye kuzalisha ili kurejesha mtaji na riba kwa mwenye hela.

Kama NSSF au PSSPF mna utayari tutafufatene walau kwenye brainstorming mpate kujua nini namaanisha. Japo sitashangaa kupata jibu, taasisi zetu hizi hazifanyi kazi na mitandao ya kijamii. Wakati huo huo ukiandika barua, it take time kujibiwa. Msiogope start-up, kama ziki well organized. Mbona TANROAD, TARURA, EWURA, SUMA JKT zilianza na zinakwenda. Kimsingi walianza kwenye right set-up.

Tumsaidieni mfalme wetu walau awe busy kufungua maviwanda, maana mrejesho wake kwenye uchumi na biashara una +ve ripple effect hususan kwa Watanzania wengi na taasisi za kodi, mifuko ya pensheni, mifuko ya bima ya afya... the list goes on.
 
Back
Top Bottom