Hivi zile pesa za tahadhari tunazolipa shuleni au vyuoni huwa zinarudishwa ukimaliza?

donlucchese

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
17,040
21,513
Nakumbuka tangu nikiwa sekondari, A-levo mpaka chuoni huwa kuna pesa ya tahadhari (caution money) ambayo tuliaminishwa hutumika pale endapo mwanafunzi anaweza akawa amecause damage kwenye property ya taasisi husika.

Swali ni kwamba je, endapo mwanafunzi amemaliza bila tatizo lolote lile si ni jukumu la uongozi wa taasisi husika kurudisha fedha ile?

Kwangu mimi binafsi kote nilipopitia sijawahi kurudishiwa fedha ile. Sijui kwa nyie wenzangu Wakuu.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiomba zinarudi..baada ya kumaliza shahada ya uzamili pale mlimani, nliomba nkarudishiwa, though kwa kuchelewa Sana.
 
Baadhi ya vyuo wanarudisha, mfano MU bàada ya kujaza clearance form unashikishwa 50k yako, utaamua ufanye nauli au ukapige mtungi ukijipongeza kumaliza chuo.
 
Back
Top Bottom