Walimu wapya 6000 kuajiriwa ifikapo Juni, kuanza na waliojitolea kwanza

Feb 9, 2021
6
16
Naibu Waziri wa TAMISEMI mh Silinde amewataka maafisa elimu nchini kupeleka majina ya walimu waliojitolea mapema ili wapewe kipaumbele katika ajira 6000 alizotangazwa Rais Samia hivi majuzi.

Akijibu swali bungeni Naibu Waziri Silinde amesema kigezo cha kwanza itakuwa wale wote waliojitolea na amewataka maafisa elimu kutuma majina kwanza ya walimu waliojitolea kufundisha.

----
Serikali imesema walimu wapya 6000 wa shule za msingi na sekondari wataajiriwa ifikapo mwezi juni, mwaka huu ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi na walimu waliofariki au kustaafu kazi.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia elimu Mhe.David Silinde kwa niaba ya Waziri wa Nchi wa Ofisi hiyo ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Njombe Mhe. Deodatus Mwanyika aliyetaka kujua serikali inachukua hatua ipi kumaliza tatizo la upungufu wa walimu nchini hasa katika shule za vijijini.

Mhe Silinde ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana na Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia katika kukamilisha jukumu hilo.

Mapema Naibu Waziri amesema kati ya desemba mwaka 2015 na septemba 2020 serikali imeajiri walimu 10666 wa shule za msingi na walimu 7515 wa shule za sekondari ili kukabiliana na upungufu unaojitokeza hususani kuwapanga katika maeneo yenye uhitaji mkubwa.

Aidha ameongeza kuwa kuanzia mwezi desemba mwaka 2015 hadi septemba 2020 halmashauri ya mji wa njombe imeajiri walimu 21 wa shule za msingi na walimu 111 wa shule za sekondari.

Mhe Silinde amesema vilevile Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia ofisi za wakuu wa mikoa imekuwa ikifanya uhamisho wa ndani kwa kuwahamisha walimu waliozidi hasa kwenye maeneo ya mijini na kuwapanga kwenye shule zenye uhaba mkubwa wa walimu ambazo nyingi ipo maeneo ya vijijini.
 
Anawadanganya tu huyo muunga juhudi silinde.

Hata ajira za mwisho walisema hivyo, lakini wengi sana hawakuajiliwa.

Usiwaamini sana CCM, waongo sana.

Kama walimsujudu, kumsifu na kimwabudu bwana maguguli, hata hajadekompose wamenza kusema alikuwa mwizi, dikteta na fisadi. Iweje kwa mwalimu wa kujitolea?

Ajira zitatoka kwa connections, rushwa, walemavu, masomo ya wachache, elimu maalumu na wachache kwa bahati

Kwa sasa usiwaamini CCM.
 
Hapo sasa ndo tunapokosea,zamani walikuwa wanatoa post moja kwa moja, kwa sasa kila field ya serikali walimu wapo wanajitolea mfano kwenye majeshi wapo na hata Halmashauri nyingi walimu wapo wanakusanya mapato na kupewa posho tu kuendeshea maisha yao; je walimu hawa hawatapata ajira?
 
Naibu Waziri wa TAMISEMI mh Silinde amewataka maafisa elimu nchini kupeleka majina ya walimu waliojitolea mapema ili wapewe kipaumbele katika ajira 6000 alizotangazwa Rais Samia hivi majuzi.

Akijibu swali bungeni Naibu Waziri Silinde amesema kigezo cha kwanza itakuwa wale wote waliojitolea na amewataka maafisa elimu kutuma majina kwanza ya walimu waliojitolea kufundisha.
Yote kheri
 
Huyu silinde kwa kauli hiyo inabidi aachie ngazi, izi kauli ndo zinazoleta mianya ya Rushwa kwa nini wasie wanapita mashuleni kutake note na kunakili majina ya walimu wanao jitolea, kuliko kuliko kuwambia maafisa elimu wapeleke.
 
Siasa mbele taaluma nyuma, kwani kazi ya CV ni nini au watu wanagushi CV. CV huonyesha mtu anafanya nini amepita wapi.
Silinde ni kama hajasoma shule vile.
 
Huyu silinde kwa kauli hiyo inabidi aachie ngazi, izi kauli ndo zinazoleta mianya ya Rushwa kwa nini wasie wanapita mashuleni kutake note na kunakili majina ya walimu wanao jitolea, kuliko kuliko kuwambia maafisa elimu wapeleke.
Yaani huo mwanya,utatumika vizuri sana na waalimu wakuu ambao wataandika majina ya walimu,kwasababu wale ambao hawakua mashuleni,watataka nao majina yao yaandikwe kwa kutoa chochote.
Huu utaratibu ni wa hovyo sana.JK alikua bora kwenye hili.
 
Huu ni ujinga kabisa.

Kigezo cha kupata ajira ni kujitolea?

Kama ni hivi watoe tamko tanzania ijue ,watu wakimaliza vyuo wakajitoleee ndio waajiriwe.

Vinginevyo huo ni uhuni tu
Kujitolea huwa ni sifa ya Kwanza kuajiriwa sehemu nyingi duniani
 
Mmmh ninavyojua mimi wengi waliojitolea hiyo taaluma hawana ila kwakuwa wanajua kusolve math basi walipewa chaki wafundishe

Kiukweli asilimia kubwa ya walimu wa shule za kata hawakusomea ualimu wengi wao walipachikwa tuu ninayo mifano iliyo hai kwa hili ninaloliandika

Serikali ingewaajiri waliihitimu wa vyuoni na siyo kuangalia waliojitolea ama sivyo wadai na vyeti vya taaluma ya ualimu
 
Back
Top Bottom