Hivi zile ajira elfu 13 za waalimu wa msingi na sekondari zimeishia wapi?

mbutamaseko

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
735
1,050
Ni muda kidogo umepita toka ajira hizi zitangazwe kwa mbwembwe sana.

Nilishuhudia wasaka ajira walizipokea kwa matumaini sana japo wengi walihisi ni suala la kisiasa zaidi kutokana na ajira hizo kutangazwa ghafla katikati ya kampeni.

Vipi kuna mtu anamjua mtu aliyeajiriwa kupitia ajira hizo? Mnadhani baada ya uchaguzi wataajiriwa kweli?

Hitakuwa Kama kumpa samaki chambo baada ya kumvua? Kwa yeyote mwenye lolote juu ya hili.
 
Kwa haraka , kwa dhalura na kwa mbwembwe Kama zilivyotangazwa. Unadhani kwa nini hazijatoka mpaka Sasa?
Unatakwimu za watu walioomba hadi sasa? Unajuaje kama wanachambua? Unadhani hapa wanatumia utaratibu au kanuni ya FIFO (first in first out). Wakati wa kutangaza hukuwashauri, sasa subiri wakati ukifika watatangaza.
 
Unatakwimu za watu walioomba hadi sasa? Unajuaje kama wanachambua? Unadhani hapa wanatumia utaratibu au kanuni ya FIFO (first in first out). Wakati wa kutangaza hukuwashauri, sasa subiri wakati ukifika watatangaza.
Mbona umepanic pimbi? Kwa kupanic huku unadhani kuna ajira hapo? FIFOOOOO
 
Samahani kama ntawakwaza baadhi ya watu lakini nacho weza sema.

Atoe asitoe, Ila kila kijana aliyemaliza au aliyopo bado chuoni, inabidi ajiulize, je yupo tayari kuendelea na utaratibuu huu kuwa inapofikia wakati wa kampeni ndyo ajira zitangazwe?

Kama jibu ndiyo, basi tar ile chagua bwana yule lakini kama jibu hapana, basi chagua upande wa pili ambao unaonekana kuwa na utaratibu tofauti katika jambo hili la ajira.

Neno langu siyo sheria.
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku). Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Ataajiri kwa hela ipi? Aache kununua ndege na kujenga flyovers!! Hivyo ndivyo anavyowaza muda wote.

Halafu wakati huo huo unapewa porojo za majukwaani eti tunatoa bilioni 19 kila mwezi kwa ajili ya Elimu Bure! Elimu bure bila Walimu wa kutosha na wanaolipwa stahiki zao kwa wakati?

Bora Wapiga Kura wamchague Tundu Lissu. Huenda akayarudisha matumaini yaliyopotea kwa Watanzania walio wengi.
 
Mmeshachagua mnataka nini Tena, hakuna ajira miaka hii mitano. Kama huamini kasome Ilani ya CCM
 
Back
Top Bottom