Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,213
- 1,638
Kanuni: Ikiwa A = B na B = C; siyo kosa kusema A = C. Kuhusu watu kutoka nje kuwa Wazanzibar, hilo halipo ila liliopo na kwa mujibu wa Sheria ya Mzanzbari, kuna Uzanzibari wa aina mbali kama vile: Watu wote waliokuwa raia wa sultani tarehe 12/1/1964 ni Wazanzibari. Watu wote ambao mmoja wa wazazi wake ni Mzanzibari huyu ni Mzanzibari wa kuzaliwa. Uzanzibari mwingine ni wa kujiandikisha na mwingine tena ni ule unaopatikana kwa Mtanzani yeyote kukaa Zanzibar kwa miaka mitatu mfululizo na akaomba kuwa Mzanzibari. ili uwe Mzanzibari unapaswa kwanza kuwa Mtanzania. Tatizo ni wale waliopewa dhamana kutumia dhamana zao kwa maslahi binafsi (rushwa).