Hivi zaidi ya uhakiki, Angela Kairuki hana kazi nyingine anayofanya?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,784
Maana kila siku namsikia tu yupo kwenye uhakiki...
Hana jipya analofanya kama kushughulikia mazingira safi ya ufanyaji kazi, maslahi ya wafanyakazi na hata wastaafu...
Kuna watu kibao wanateseka kufatilia madai yao mbali mbali kama pension, kuhamishwa vituo vya kazi nk.

Huyu mama sijawahi hata kumsikia akishughulika na mambo kama hayo...
Sema za ukweli hawa wakina Kairuki, ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa uasherati kwa kuwa wameshindwa kutumia nafasi zao kuwaunganisha wana ndoa waliotenganishwa na ajira.
Wewe kama mtu mzima, hivi kweli unashindwa kufikiria mfanyakazi wako yuko mbali na mwenzi wake kwa zaidi ya mwaka anatimiza vipi haja zake za kiutu uzima kama sio kuchepuka? Na wewe waziri uko hapo tu unafurahia kulipwa mshahara?
 
Unahakiki watumishi mwaka, ! hahahah tunafanyana watoto hakika, nipo mbali na familia na gharama za maisha zimepanda kwa kuhudumia kaya mbili plus makorokoro mengne, HALAFU ETI WANATETEA WANYONGE! SIJUI LABDA KUNA MAANA NYINGINE YA WANYONGE AMBAYO MIMI SIJUI, Yaaani duu
 
Maana kila siku namsikia tu yupo kwenye uhakiki...
Hana jipya analofanya kama kushughulikia mazingira safi ya ufanyaji kazi, maslahi ya wafanyakazi na hata wastaafu...
Kuna watu kibao wanateseka kufatilia madai yao mbali mbali kama pension, kuhamishwa vituo vya kazi nk.

Huyu mama sijawahi hata kumsikia akishughulika na mambo kama hayo...
Sema za ukweli hawa wakina Kairuki, ndio wamechangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kwa uasherati kwa kuwa wameshindwa kutumia nafasi zao kuwaunganisha wana ndoa waliotenganishwa na ajira.
Wewe kama mtu mzima, hivi kweli unashindwa kufikiria mfanyakazi wako yuko mbali na mwenzi wake kwa zaidi ya mwaka anatimiza vipi haja zake za kiutu uzima kama sio kuchepuka? Na wewe waziri uko hapo tu unafurahia kulipwa mshahara?
Tatizo hapa ni kwamba vyombo vya habari vinatoa zile habari za ku capture attention na kuuza magazeti. Hizo habari nyinginezo ambazo ungependa kuona Waziri Kairuki anazitoa kuhusu mazingira safi ya ufanyaji kazi, maslahi ya wafanyakazi na hata wastaafu...sio NEWS, haziuzi Magazeti hizo. Yapo mambo mengi yanafanyika katika wizara ile ambayo kwa tasfiri ya media yetu they are not newsworthy. kama ukiangalia kipindi cha TBC cha Tunatekeleza au kipindi cha dakika 45 utapata kufahamu mambo mengine mengi yanayofanyika mbali na uhakiki.
 
ndio kazi aliyopewa afanye uhakiki hadi 2020 ili mukose haki zenu amesema mwisho march mosi ataongeZa two weeks
 
Kazi nyingne hana kama IPO haina manufaa kwa umma, vitu vinavyolenga umma ni Ajira, maslahi watumishi, uhamisho, pension, kupanda madaraja, nyongeza mshahara, je haya kafanya hata 1?

Atasema anaimarsha wizara je ndo inaanza au ina zaidi ya miaka 50? Je hivyo vitu vngne ndo atumie mwaka mzma kuvifanyia marekebsho huku mambo yote yamesimama? Mawazo finyu na uwezo mdogo wa viongoz wetu, ukiamn serikali hii ya awamu 5 umepotea,

Maana imejaa ubaguz, majungu, visa, uchama, visasi, chuki nk, muda wa siasa umeisha viongoz wafanye kaz kwa ajiri ya umma na sio kulenga matumbo yao tu,

WATU WAKISEMA MNAWAITA WACHOCHEZ WAKATI MNACHOFANYA SIO RAFIKI, MNATAKA MPEWE SIFA TU HATA PASPOSTAHILI, PUNGUZENI MIHEMUKO HAPO MNAPTA TU NA MAISHA YA WATANZANIA YATAENDELEA HATA BILA UWEPO WENU, MAISHA MLIYONAYO KTK HIZO NAFASI NI YAMPITO TU, MSIJFANYE MIUNGU WATU NA MTAKE KUABUDIWA KWENYE HAMNA!
 
Tatizo siyo yeye bali wafanyakazi wenyewe. Kuna vyama vya kutetea wafanyakazi je vimeungana na kupinga vinavyoendelea ndani ya wizara zao? Sababu hivi vyama viko kwa mujibubwa sheria kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi.ambapo wanaweza kuibana wizara kisheria.

Tukubali watanzania wengi bado hatutaki kubadilika na tunakubali kuwa watumwa kwa wakubwa zetu/ viongozi wetu. Hata hivyo vyama vipo tu kama majina lakini si kwa kusaidia wafanyakazi
 
Back
Top Bottom