Hivi wimbo wa nyegezi umepigwa marufuku wapi?

ngonyango

JF-Expert Member
Aug 7, 2017
1,836
2,000
Ukienda kwenye mabaa , shoo za promotions mbalimbali , disco , pubs ..kila mahali ni nyyegezi kwenda mbele.. mitaani watoto wanauimba kama wote......hata waheshimiwa wakiusikia huwa wanatingisha vichwa kwa furaha kama siyo kuruka ruka mfano Mhe. Naibu Spika , naona hata BASATA wenyewe huko mtaani watakuwa wanaukubali....sasa najiuliza huu mwimbo umepigwa marufuku kwenye matamasha ya Wasafi Festival tu au?? nimekumbuka hii ishu sababu niko hapa Nyerere square Dodoma kuna promotions ya Tigo inaendelea..wanashindana kucheza Nyegezi...Hongereni WCB kwa kutoka video chap chap kabala ya ban manake duh iko hewani sana kila mahali...ifike mahali tuache unafiki wadau
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,957
2,000
Taifa la Tanzania limejaa viumbe binadamu wanafiki!!

Tuliambiwa huo wimbo umejaa matusi! Sasa kama unayosema ni kweli; how come tena Tigo wanaachwa kumwaga mitusi tena bila shaka wakisaidiwa na maspika?!

Ina maana eneo lote hilo hajapita askari akashuhudia matusi yakisambazwa waziwazi tena kwenye halaiki?! Ikiwa wimbo ni full matusi, how come tena hata raia wa kawaida wanawaacha Tigo waki-promote matusi?!
 

alibaaliyo

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
537
500
Ni jambo la kuhuzunisha sana wimbo huu kuendelea kupigwa kwenye hadhara na walinzi wa amani wakiwa kimya.
 

ngonyango

JF-Expert Member
Aug 7, 2017
1,836
2,000
Nafikiri hivyo vyombo vya kusimamia sheria vimeona kuwa hauna matusi ...ni kama kampa papa wa Gigy money nk
 

Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
191,391
2,000
*KIBURI* ni kati ya tabia ngumu sana kujigundua kama unayo au la. - Na kwa sababu ya ugumu wa kujigundua, ndio maana imeliza watu wengi - - *Naweka hapa mambo kadhaa TUJIPIME SOTE KAMA TUNA DALILI ZA KIBURI AU LA:-* - *1. UKIONA, KILA UKIONYWA UNAKASIRIKA NA KUNUNA AU KUSUSA, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.* - - Yaani unaona karipio au onyo badala ya kuona tatizo lako, au hata ukiona tatizo lako huwezi kujizuia KUKASIRIKA AU KUNUNA UKIONYWA. - - *2. UKIONA, KILA MKIKOSANA NA MTU, HUONI KOSA LAKO, UNAONA MAKOSA YA MWINGINE TU, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.* - - Kiburi siku zote NI KIDOLE KUKUONYESHA KOSA LA MWINGINE. - - Nilichojifunza, kwenye kila kwenye wawili au zaidi kukosana na kutokuelewana, kila mmoja ana mahali pa kujirekebisha, hakuna asiye na jambo la kujirekebisha - *3. UKIONA, KILA UNALOFANYA, UNATAKA KUJILINGANISH NA WENGINE, AU KILA WANACHOFANYA UNAJILINGANISHA NAO, HIYO NI DALILI KUBWA SANA YA MTU MWENYE KIBURI.* - Kiburi siku zote KINATAKA WEWE UJIONE UKO JUU YA WENGINE.... Wewe mzuri zaidi ya wengine... Msomi zidi ya... Una pesa zaidi ya... Unafundisha zaidi ya... Unahubiri zaidi ya... Unaomba zaidi ya... - Siku zote "Wahesabu wengine kuwa bora..." - - *4. UKIONA, KILA UNALOFANYA UNAFANYA KWA LENGO LA KUSHINDANA.* - - - Unafanya jambo zuri ndio, lakini Adhma (Motive) yako ni mashindano, hata kama hujasema hivyo... - - Unafanya ili kumshinda fulani hata kama fulani hajui, yaani utoshelevu wako wa ndani sio kutimiza jambo fulani, bali ni kugundua KWA KUTIMIZA HILO UMEMSHINDA FULANI - *5. UKIONA, UNAPENDA KUSIFIWA KWA KILA UNALOFANYA, kwa lugha nyingine kuwa RECOGNIZED AND APPRECIATED.* - - Kutambulika na kushukuriwa (to be recognized and appreciated) si jambo baya kabisa, lakini ukiona ukikosa hicho kitu unakosa amani kabisa na unatumia gharama yoyote utambulike na kushukuriwa, HICHO NI KIBURI KINAKUSUKUMA

*6. UKIONA, KILA ZURI UNALOLIFANYA SIRINI, UNATAKA LIJULIKANE NA WATU HATA KAMA SI MUHIMU KWAO na si kwa lengo la KUJIFUNZA, hiyo ni dalili ya KIBURI.* - - Ukiomba, hauridhiki mpaka watu wajue uliomba, UKIFUNGA, mpaka watu wajue ulifunga au huwa unafunga, UKIFANYA JAMBO ZURI KWA MUNGU WAKO, mpaka watu wajue ndio unasikia kuridhika... Kinachokusukuma ndani ni KIBURI. - *7. UKIONA, HAUKO HURU(COMFORTABLE) KABISA KUTUMIA LUGHA YA PAMOJA(tuta.., tume..) UNAPENDA ZAIDI KUTUMIA LUGHA YA BINAFSI (Nita.., nime.. ) UNAPOONGELEA MAMBO AU UMILIKI WA VITU, hiyo yaweza kuwa dalili ya KIBURI.* - - Hupendi kutumia lugha kama, vitu vyetu, jambo letu, huduma yetu... Sisi... nk, unapoongelea jambo ambalo na wengine wana mchango hata kama ni mdogo sana, hasa kama mwewe ni muanzilishi wa jambo au una mchango mkubwa juu ya jambo. - Kumbuka *"KIBURI HUTANGULIA ANGUKO"* - Lakini pia, *"KIBURI HUTANGULIA MAUTI"*
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,889
2,000
Taifa la Tanzania limejaa viumbe binadamu wanafiki!!

Tuliambiwa huo wimbo umejaa matusi! Sasa kama unayosema ni kweli; how come tena Tigo wanaachwa kumwaga mitusi tena bila shaka wakisaidiwa na maspika?!

Ina maana eneo lote hilo hajapita askari akashuhudia matusi yakisambazwa waziwazi tena kwenye halaiki?! Ikiwa wimbo ni full matusi, how come tena hata raia wa kawaida wanawaacha Tigo waki-promote matusi?!
Huo wimbo wa Taifa,Naibu spika nauimba mwanzo mwisho
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,729
2,000
Ngoja nicheze kidogo kama naibu spika, eeh nyege nyegezi, nyege nyegezi..................................
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom