Hivi wewe ni Raia kamili au Raia nusu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi wewe ni Raia kamili au Raia nusu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by platozoom, Sep 24, 2012.

 1. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,298
  Trophy Points: 280
  Nchi ikiwa masikini kila mtu atashikwa uchawi.............Mtashikana uchawi wa Ukabila, Dini, Kanda, Jinsia, Kuna wengine watamshambulia Bashe kwa mujibu wa rangi au wajihi wake kana kwamba wao wako salama sana............

  Kuna wengine watakishambulia chama fulani kwa mujibu wa hisia za ukanda au ukabila ambacho kimsingi hakina dola ya kuyatimiza matakwa ya kimaendeleo...

  Kuna watakaomshambulia mtu kwa sababu ya imani yake pengine wakifikiri matatizo yao yamesababishwa na wenye imani tofauti na yao.

  Au tumesahau ile dhana ya ukila nyama ya mtu................................

  Kwa nini tuwaandame watu wenye Imani, rangi na kabila tofauti na yetu?
  Ni wangapi mpaka wako majeshini na wana wazazi au jamaa zao upande wa pili wa mpaka?
  Ni wangapi ambao wana mizizi ya ukoo toka upande wa pili wa mpaka?

  Hivi watu hawaoni cartel za wizi wa mali na rasilimali za umma kutoka kwa Weusi wenzetu....Au walio wengi wenye akaunti Uswisi wana rangi ya Kijani?

  Bashe, Patel, John, Said (kwa maana ya hayo hizo tofauti hapo juu) si waliyoleta umasikini katika nchi hii..Tushughulike na ya msingi la sivyo kama Taifa tutapiga "marktime" kila uchao.


  Na hii inanikumbusha jinsi Waluo Kenya wanavyohasimiana na Wakikuyu na kufikia kuuana wakifikri matatizo yao yamesababishwa na Wakikuyu kama kabila....kuumbe kuna Waluo matajiri wanapiga deals na Wakikuyu matajiri wenzao.

  ..... nguruvi 3 Mchambuzi Mag 3 Mwanakijiji na wengineo mnaweza kutupa tafsiri ya hiki kizungumkuti?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu Platozoom,

  Nashukuru kwa kunishirikisha katika mjadala huu muhimu. Kama ulivyojaribu kubainisha, huu ni mchezo unaochezwa na wanasiasa wachache kwa maslahi yao binafsi, hasa ya kisiasa; ni dhahiri kwamba Watu wenye interest kuona Taifa letu linameguka kwa misingi ya kikabila, kidini n.k huwa SIO WANANCHI, bali WANASIASA/VIONGOZI ambao ndio huchochea na kupenyeza agenda zao katika misingi hii ndani ya Jamii kwa ustadi mkubwa sana. Na ni viongozi hao hao ambao pia ni mabingwa wa kuja na maneno matamu na ya kuvutia kila kukicha juu ya AMANI, UMOJA, KUVUMILIANA MA UTULIVU, kwamba vitu hivi vimechangia sana mafanikio yetu kama watanzania; Lakini ukitizama kwa ndani, pamoja na ukweli huu, wengi wa viongozi hawa huwa ni wanafiki na hawamaanishi wanachokisema, kwani hutumia maneno kama haya kwa ajili tu ya kujijenga kisiasa au kulinda maslahii yao fulani fulani; Sio vinginevyo;

  Suala la Hussein Bashe sio geni katika siasa za nchi yetu kwani hizi zimekuwa ni political games played around citizenship kwa miaka mingi sana, na sio Tanzania tu bali Afrika kwa ujumla. Hakika hii ni kejeli kubwa sana kwa uafrika wetu, lakini muhimu zaidi, our Panafricanism Vision; Nje ya Bashe, kama tunakumbuka vizuri, miaka ya nyuma Watu kama Arcado Ntagazwa, Jenerali Ulimwengu na wengineo kadhaa pia walichezewa mchezo huu; Kwa mfano, kwa Ntagazwa ilikuwa kwa nia ya kumwondolea sifa za kuwa Mbunge huko Kigoma na kwa Jenerali Ulimwengu, For Wielding His Pen Against POWER!!!

  Historia inatufundisha kwamba wanasiasa wote wanaocheza mchezo huu wa kipuuzi huishia pabaya, ingawa inawezekana ikatokea wakafanikiwa kisiasa in the short to medium term. Kwa mfano, Iddi Amin mwaka 1972 declared wahindi wote waliozaliwa vizazi vitatu nyuma (1972=>) kwamba sio Rais wa Uganda, hivo wengi walifukuzwa nchini, wengine waliuawa, huku Iddi Amin akijizolea umaarufu na mtaji mkubwa wa kisiasa miongoni mwa walala hoi; Lakini sote tunaelewa hatima yake kwa taifa la Uganda ikaja kuwa nini;

  Mwaka 1981, Mobutu Seseseko wa Zaire nae – declared kabila la BANYAMULENGE kwamba sio Raia wa Zaire; Hii jamii originally ilitokea Rwanda na walihamia Zaire karne ya kumi na saba na kumi na nane, kabla hata ya ukoloni haujaingia Zaire, au Taifa la Zaire kuzaliwa; Kabila hili chini ya Mobutu likateswa na kuuwa kwa wingi sana, na machafuko yakaendelea hadi miaka ya 1990s ambapo ikapelekea kwa taifa jipya la DRC kuzaliwa; Licha ya hayo, mpaka leo hali ya DRC sio shwari;

  Mwaka 2002, Rais Gbagbo wa Ivory Coast nae declared mpinzani wake - Alassane Ouattara (Rais wa sasa) na wafuasi wake kwamba sio Raia wa Ivory Coast; matokeo yake ni kwamba Ivory Coast ikaishia kugawanyika kati ya North and South, huku upande wa North ukimuunga Mkono Alassane Ouattara, na ule wa South wakimuunga mkono Gbagbo; hatima ya hili sote tunaijua;

  Nchi jirani na sisi hapo Zambia pia, Kaunda na wenzake wakaja kuwa declared na Rais Chiluba kwamba sio Raia, na kidogo ipelekee nchi kwenye machafuko kama sio juhudi za Nyerere na jumuiya ya kimataifa; Lakini sote tunajua hatima ya Chiluba ilikuwa nini, na jinsi gani familia yake inavyoteseka sasahivi;

  Kwa mtazamo wangu ambao unaweza usiwe sahihi sana ni kwamba, waasisi wa nchi nyingi za Afrika (the likes of Nyerere) walifanya uamuzi wa busara sana kuja na resolution kwamba mipaka iliyowekwa na Wakoloni wakati wa scramble and partition for Africa iendelee kuwa ile ile baada ya uhuru ili kuepuka machafuko siku za usoni. Actually, hili lilikuwa ni pendekezo la Nyerere kwa OAU ambalo lilipitishwa kwa kura karibia zote; Tumeona faida ya resolution hii kwa afrika, ingawa bado tunaona wachokozi wachache kama Mama Banda wa Malawi ambae pia hili suala ni msukumo wa kisiasa zaidi ili kujitafutia mtaji wa kisiasa kwani ni vigumu sana kwake kupita kwenye uchaguzi mkuu ujao kama Rais wa kwanza mwanamke wa Malawi; Lakini all in all, uamuzi wa kurithi mipaka ya ukoloni ulikuwa wa busara sana; Lakini kwa mtazamo wangu, waasisi wetu walisahahu pia kuja na resolution nyingine muhimu sana ambayo ingeangalia suala la Uraia, sio mipaka tu, kwa mfano kwa kutumia vigezo vya generations fulani fulani n.k; Nadhani kama tukidhamiria, tunaweza kulianzisha hili nyumbani (Tanzania) sasahivi before it becomes too late;
   
 3. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,298
  Trophy Points: 280
  Asante Mchambuzi.

  Na hili la kuwinda watu kisiasa ndilo huwa linanipa shida sana. Kwa mfano unapomsema mtu sio raia kama silaha ya kisiasa au kumziba mdomo wale wenye asili kama yake wanakuwa wanafikiri nini? Hivi kweli watajihisi wako salama ndani ya nchi yao?

  Namkumbuka Waziri Gregory Awori aliyekuwa kwenye baraza la mawaziri la Yoweri Museveni wakati huohuo upande wa pili nchini Kenya Kaka yake Moody Awori ni Makamu wa Rais. Pamoja na wakenya kubaguana kikabila sikuwahi kuwasikia mahasimu wa Moody Awori wakimwita Mganda kwa sababu ya asili ya wazazi wake.

  Labda tuseme uwanja wa kisiasa si mkubwa kiasi hicho.......kwamba kwenye duara la kisiasa kuna idadi kubwa ya wanasiasa wasiokuwa Wanasiasa kwa maana halisi ya "Uanasiasa" ? Kwa hiyo lolote linaweza kufanyika............

  Au tuseme "waungwana" wanakuwa kama simba aliyejeruhiwa na kuchanganyikiwa linapofika suala kinyang'anyiro cha madaraka au kulinda himaya yao? na pale vumbi linapotulia wanarudisha akili yao vizuri (Kama ishu ya Bashe na Ulimwengu ilipokwisha kwa namna ya kushangaza)
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na hoja zako nyingi kimsingi, lakini iliyonigusa zaidi ni hiyo hapo juu; ukipata muda naomba utembelee uzi wangu mwingine ambao nimejaribu kuwajadili wanasiasa wetu katika mazingira ya uongozi; nasita kujadili tena humu kwani katika majibu yangu kwako, nahisi kama kwa kiasi kikubwa nitayarudia yale yale niliyoyajadili huko nyuma; link ya uzi huo ni hii ifuatayo: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/293844-lowassa-na-tatizo-la-uongozi-ccm.html
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,298
  Trophy Points: 280
  Asante. Bila shaka nitapata muda wa kuupitia kesho na pengine kutafuta angle nyingine muhimu ya mjadala

  Usiku mwema
   
Loading...