Hivi weupe ndio urembo au?

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,409
119,014
Habari zetu warembo na watanashati.

Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi? tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.

Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote?

Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
CREAM+ORIGINAL+NA+ZA+UHAKIKA+KWAAJILI+YA+KUNG%27ARISHA%2C+KUSOFTISHA%2C+NA+KUPENDEZESH.jpg
 
Ndiyo maana wachina, wazungu, waarabu wanatucheka sana kwa kutuletea kemikali zilizo oza huku Afrika. Pia inashangaza unaweza ona mwanamke mweusiiii amevaa wigi la kijani, nyekundu, njano, sielewi wanaona uzuri gani. Yaani baada ya kuonekana mzuri anakuwa anatisha kuwa a zombie.
 
Ndiyo maana wachina, wazungu, waarab wanatucheka sana kwa kutuletea kemikali zilizo oza huku Afrika. Pia inashangaza unaweza ona mwanamke jeusiiii limevaa wigi ya kijani, nyekundu, njano, sielewi wanaona uzuri gani. Yaani baada ya kuonekana mzuri anakuwa anatisha kuwa a zombie.
ulivyoweka msisitizo jeusiii mwenyewe akikusikia si ndo mwanzo wa kwenda kujichubua
 
Ndiyo, kwenye jamii nyingi, hususan za watu weusi [walio na asili ya Afrika] rangi nyeupe ya ngozi huhusishwa na urembo.

Naamini ni ukweli ambao watu wengi hatuupendi, lakini ndo hivyo tena. Ukweli mara nyingi huwa ni mchungu na tulio wengi huwa tunajitahidi kuukataa waziwazi.

Hapo juu umezungumzia watu kujichubua ili kujibadili rangi ya ngozi na wawe weupe zaidi. Vipi kuhusu nywele bandia zilizonyooka? Ina maana nywele asilia za kipilipili ni mbaya, siyo?

Na vipi kuhusu majina ya kigeni siku hizi?

Unakuta mtu anaitwa Anthony Francis wakati baba ni Mgogo na mama ni Mnyiramba!

Au Maxwell John wakati baba ni Mmakonde na mama ni Mzaramo!

Hiyo mifano inanileta kwenye hoja ya kuhusisha Uafrika na uduni na Uzungu na ubora.

Hata watu wenye tabia za kishenzi huwa tunawaita 'waswahili'. Halafu tabia flani flani zinazoonekana au kudhaniwa kuwa ni za kistaarabu ndo zinaonekana ni za 'kizungu'.

Ni ndivyo tulivyo tu.
 
Hapo kwenye majina pananikera sana, unakutana na mtu mzima bila aibu eti anaitwa Peter Paul au Mohammed abdallah, seriously!! Hii ipo zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile Africa. Nigeria ni aibu mtu kuwa na jina la kigeni hata mnigeria azaliwe wapi ataitwa Babatunde, Yemi na majina yao ya asili hali kadhalika South Africa wanatumia sana majina yao, wakenya pia ni sisi tu ndo tumekengeuka.

Kuna mtoto mtanzania toka Mwanza mwaka jana alienda UN kuhutubia anatumia majina mawili yote ya kigeni hadi wale watu walimshangaa. Nilikua naangalia TV ila niliona aibu peke yangu.

Ni wabongo tu ambao wakienda mbele kama anaitwa Musa atajiita Moses, Hashimu Thabiti kawa Hasheem Thabeet. Tumekuwa whitewashed hadi aibu
 
Aibu mno!

Tena sasa hivi nadhani huo mtindo ndo umeshika kasi sana.

Zamani walau moja ya majina ya mtu lilikuwa lazima liwe lile la ukoo.

Lakini siku hizi sivyo kabisa.

Ukitaka kuliona hilo kwa wingi basi angalia matokeo ya mitihani ya wanafunzi wa shule za sekondari au angalia orodha ya wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.

Yaani mtu unayasoma hayo majina hadi unaanza kuona aibu kabisa.
 
Habari zetu warembo na watanashati.
Hii tabia imeota mizizi sasa sijui kwa nini wanawake tunakuwa hivi...tena siku hizi vipodozi vya kubadilisha rangi vinatangazwa hadharani kabisa afadhali siku za nyuma watu walikuwa wanajichubua kwa kujificha.
Hivi ni kweli hivi vipodozi vya kubadilisha ngozi havina madhara kiafya? Kama vina madhara mamlaka zinazohusika zimeshindwa kuwashughulikia wanaofanya biashara hizi? Kwa kweli nashindwa kuelewa hivi huyu dada ukimuangalia picha yake ya kushoto na kulia kuna tofauti yoyote? Ipo inayovutia kuliko nyingine? Mimi naona mtu ni yule yule tu nothing more nothing less. Naombeni maoni yenu wadau
View attachment 526690
Best habari za masiku! Hii ni tiba ya vidonda na mabaka ya ngoma. Ukiona hivyo anao
 
Hapo kwenye majina pananikera sana, unakutana na mtu mzima bila aibu eti anaitwa Peter Paul au Mohammed abdallah, seriously!! Hii ipo zaidi Tanzania kuliko nchi nyingine yeyote ile Africa. Nigeria ni aibu mtu kuwa na jina la kigeni hata mnigeria azaliwe wapi ataitwa Babatunde, Yemi na majina yao ya asili hali kadhalika South Africa wanatumia sana majina yao, wakenya pia ni sisi tu ndo tumekengeuka.

Kuna mtoto mtanzania toka Mwanza mwaka jana alienda UN kuhutubia anatumia majina mawili yote ya kigeni hadi wale watu walimshangaa. Nilikua naangalia TV ila niliona aibu peke yangu.

Ni wabongo tu ambao wakienda mbele kama anaitwa Musa atajiita Moses, Hashimu Thabiti kawa Hasheem Thabeet. Tumekuwa whitewashed hadi aibu
Hapo sasa unakuwa unatuonea let's say mi naitwa Josephine na baba yangu anaitwa Goodluck, nifanyeje? Nichukue jina la jirani?
 
Best habari za masiku! Hii ni tiba ya vidonda na mabaka ya ngoma. Ukiona hivyo anao
Nzuri best za wewe? nimecheka ila siku hizi hakuna ngoma ya hivyo wananona tu mwisho wa siku wanakufa kama shinikizo la damu
 
Hapo sasa unakuwa unatuonea let's say mi naitwa Josephine na baba yangu anaitwa Goodluck, nifanyeje? Nichukue jina la jirani?

Hmm? Ni kweli haujui inavopaswa kuwa au..?

Kikawaida jina la pili huwa ni lile jina la ukoo.

Huyo Goodluck hana jina la ukoo?

Tuseme anaitwa Goodluck Msambichaka...wewe kama unaitwa Josephine basi jina lako la pili litakuwa Msambichaka na si Goodluck.

Hivyo utaitwa Josephine Msambichaka.

Hivyo ndivyo ilivyo...ila siku hizi imeanza kuwa tofauti.
 
Hapo sasa unakuwa unatuonea let's say mi naitwa Josephine na baba yangu anaitwa Goodluck, nifanyeje? Nichukue jina la jirani?
Sio kosa lako sababu ni nje ya uwezo wako ila nawalaumu wote ambao walitangulia bila kuona athari za hili. Hivyo na wewe, kwa mfano, ukimuita mtoto wako Innocent basi mwanao ataitwa Innocent Josephine Goodluck, mwanao kwa hakika amepoteza identity yake milele.

Aidha watanzania wengi wanajua majina ya Koo zao ila wanachagua kutoyatumia makusudi, simjui mtu hata mmoja ambaye hajui jina lake la asili ila huwa yanafichwa.
 
Hmm? Ni kweli haujui inavopaswa kuwa au..?

Kikawaida jina la pili huwa ni lile jina la ukoo.

Huyo Goodluck hana jina la ukoo?

Tuseme anaitwa Goodluck Msambichaka...wewe kama kama unaitwa Josephine basi jina lako la pili litakuwa Msambichaka na si Goodluck.

Hivyo utaitwa Josephine Msambichaka.

Hivyo ndivyo ilivyo...ila siku hizi imeanza kuwa tofauti.
Sawa mkuu ila huwezi kujua mtu ana sababu gani za kutotumia jina ukoo
 
Sio kosa lako sababu ni nje ya uwezo wako ila nawalaumu wote ambao walitangulia bila kuona athari za hili. Hivyo na wewe, kwa mfano, ukimuita mtoto wako Innocent basi mwanao ataitwa Innocent Josephine Goodluck, mwanao kwa hakika amepoteza identity yake milele.

Aidha watanzania wengi wanajua majina ya Koo zao ila wanachagua kutoyatumia makusudi, simjui mtu hata mmoja ambaye hajui jina lake la asili ila huwa yanafichwa.
Wengine hawataki kufahamika makabila yao mfano ukiona Sanga unajua tu ni nani
 
Sijawahi kusikia sababu yoyote ile iliyo na mashiko.

Nyingi ambazo huwa nazisikia huwa hazina mashiko kabisa.

Naweza kusema nyingi ya hizo sababu zinatokana na ujinga [ignorance] tu.
Wewe hujawahi kusikia ila zipo. Na mashiko yangu mimi wewe unaweza kuona ni upuuzi...ndo hivyo tunatofautiana
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom