Nondoh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2016
- 298
- 478
Kila siku huwa najiuliza hivi hawa werevu wanakuwaga wapi hadi yule wanayemuona mjinga/mpumbavu anachukua hatua ambazo wanaziona hazifai, na kuanza kumshambulia. Je wangekuwa wanakemea na kutoa njia sahihi ya kushughulikia matatizo hivi huku kote tungefika?
Kuna matukio mengi sana yametokea na yanaendelea kutokea lakini hakuna hata mwerevu mmoja aliyejitokeza mbele kukemea na kutoa suluhisho nini serikali au jamii ifanye ili kutatua kuliko kusubiri mpumbavu achukue hatua then kuanza kumshambulia.
Mfano mpumbavu alijaribu kuchukua hatua zidi ya shisha na changudoa werevu wakaibuka kama inzi msimu wa maembe wakamshambulia personal hadi akashindwa. Mimi nilizani sasa wao watalivalia njuga suala la shisha na dada/kaka poa kwa njia stahiki kuhakikisha serikali inalitokomeza lakini hadi leo wamekaa kimya na serikali imekaa kimya.
Sasa kimbembe ni hiki cha sasa, toka afariki amina chifupa hakuna mtu aliyetanua mdomo hadi former prezidaa alistaafu na orodha yake mfukoni... Leo hii kaibuka mtu kulikemea na kuchukua hatua kila mtu anamshambulia ndani ya chama chake na nje ya chama chake.
Sasa najiuliza hawa werevu wanakuwaga wapi? Na wanapoteleaga wapi baada ya tukio?