Hivi Wazungu wao wanajisikiaje katika Dunia yenye 'Miafrika Ndivyo Ilivyo'? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Wazungu wao wanajisikiaje katika Dunia yenye 'Miafrika Ndivyo Ilivyo'?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Oct 9, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Katika tafakuri zangu za kujiandaa kurudi kubeba maboksi kwa wazungu nimejikuta tena nikiitafakari nadharia tata ya 'Miafrika Ndivyo Ilivyo'. Ila leo nimeiangalia kwenye upande wa pili wa thumni. Hivi hawa wazungu ambao mwananadharia wa 'Miafrika Ndivyo Ilivyo' anadai wamependelewa na Mungu kuwa na vichwa vya kuvumbua sana wao huwa wanajisikiaje?

  Kwa mfano, yanapotamkwa majina ya Galileo Galilei, Isaac Newton, Abraham Lincoln, Marie Curie, William Shakespear, Albert Einstein, Bill Gates na wazungu wengineo je mzungu anajisikiaje? Je, anajisikia kuwa hayo ni mafanikio ya Kizungu tu? Au anakubaliana na Frantz Fanon kuwa mafanikio hayo ni ya watu wote duniani ikiwamo Miafrika/Mitanzania?

  Kama kuna mzungu humu ndani au mtu anayewaelewa vizuri wazungu basi naomba anisaidie kuelewa hili suala maana nadhani lina jibu la matatizo yetu Miafrika. Ningependa kujua mtu kama Jim Sinclair anajisikiaje hasa anapotoa yale matangazo yake kuhusu jinsi wanavyochota madini ya Mitanzania. Je, na yeye anajisikia kama yule Paul Mooney wa Makuadi wa Soko Huria? Kwa ujumla, je, wanajisikiaje kuhusu 'Miafrika ndivyo Ilivyo'?
   
 2. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  M-PM Nyani aka Julius

  Hahahahaha.....miafrika imeanza kushtuka sasa inauliza maswali...hahaha...
   
 3. m

  mzanganyika JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 257
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Charles Darwin aliamini kwamba akili ya Mzungu iko more advanced and sophisticated kuliko ya Mwafrika.

  Baadaye wanasayansi walithibitisha kwamba hiyo nadharia yake haikuwa sahihi.
   
 4. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jamii ijuayo uwiano thabiti kati ya dharau, ubinafsi, chuki na ustaarab dhidi ya jamii nyingine na baina ya watu wake ni jamii yenye maendeleo. Isiyojua ni dumazi.

  Kwa ujumla, wanajua ni kwenye mambo gani wanaizidi na yepi hawaizidi 'Miafrika'. Wanaangalia mambo ya kuisaidia na mambo yasiyohitaji kuisaidia wakihakikisha kwamba, haiangamii yote na wakati huo huo hawaiendelezi kwa kasi na kujikuta 'wao ndiyo wamelala' na kuanza kuitegemea 'Miafrika' kwa kila jambo.
   
 5. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  SteveD vipi kaka, habari ya Iringa.

  Umeshajiandikisha kupiga kura za Serikali za mitaa.

  MJ
   
 6. Companero

  Companero Platinum Member

  #6
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo sasa wazungu wanaamini kwamba hiyo nadharia yake haikuwa sahihi?


  The Bell Curve

  Originally prepared by: Brian Beatty
  Revised:


  [SIZE=+2][​IMG][/SIZE]
  The Bell Curve, published in 1994, was written by Richard Herrnstein and Charles Murray as a work designed to explain, using empirical statistical analysis, the variations in intelligence in American Society, raise some warnings regarding the consequences of this intelligence gap, and propose national social policy with the goal of mitigating the worst of the consequences attributed to this intelligence gap. Many of the assertions put forth and conclusions reached by the authors are very controversial, ranging from the relationships between low measured intelligence and anti-social behavior, to the observed relationship between low African-American test scores (compared to whites and Asians) and genetic factors in intelligence abilities. The book was released and received with a large public response. In the first several months of its release, 400,000 copies of the book were sold around the world. Several thousand reviews and commentaries have been written in the short time since the book's publication.

  Source: http://www.indiana.edu/~intell/bellcurve.shtml
   
 7. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Kumbe dili lako lote la kwenda Bongo "kujenga nchi" ulifanya tu sababu ulijua muda wowote maisha yakiwa magumu Bongo ungeweza kurudi tena huko ulipokuwa ukiishi Ughaibuni?

  Baya zaidi ulikuwa mstari wa mbele kusihi wenzako warudi "kusukuma mbele gurudumu la maendeleo" nyumbani bila kujali kama wana vibali/uraia huko Ughaibuni au la. Ni woga na unafiki mtupu!
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu rejea kwenye mada. Hilo unalolisema lina mahali pake. Nyani haoni...
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huku kutoka toka nje ya mada husika ndio kunasababisha Miafrika tubaki kama tulivyo. Jadili mzungu - na si Compa - anajisikiaje. Alafu mnaongea kana kwamba mtoa Visa za kwenda kubeba maboksi ni mimi mwenyewe!
   
 10. K

  Koba JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  Tukifuata sheria na kuacha rushwa na wizi tutawazidi hata wazungu!
   
 11. Companero

  Companero Platinum Member

  #11
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Wazungu wanajisikiaje kuhusu hilo tamko?
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...hapo ukiongezea swala zima la kuwa watafiti ili kumudu mazingira yetu na kuyaendeleza kwa kutumia elimu iliyopo na ile tutakayojifunza, tutawazidi hata Wajapan!!
   
 13. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tamko lipi hilo unalong'ang'ania?!!
   
 14. Companero

  Companero Platinum Member

  #14
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Linalosema tutawazidi!
   
 15. p

  p53 JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  Hivi wewe hujajua jinsi wabongo tulivyo wanafiki?Hapa watu wanabwabwaja tu kwa kutumia nick names lakini dhamira ya dhati zero.
  Wewe cha msingi wasomeee ukiona kuna la kufaa katika maisha yako lichukue,ukiona wamemwaga upupu waachie wenyewe uwawashe
  Akili mkichwa mkulu usifuate maneno ya mtu!
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Oct 9, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hawana hofu nalo. Kwa mwendo tulionao wanajua hatutaweza kuwazidi. Katika huu mwendo wametuacha nyuma zaidi ya miaka 350! Hata hivyo tukiamua kubadilika na kuanza kufuata sheria, kuacha rushwa, kuwa watafiti, kuweka jamii kwanza kabla ya ubinafsi, na mengineyo mengi yenye misingi ya kuleta maendeleo huku tukijihami na yale yote yanayoweza kutudumaza (both external and internal); basi tunaweza tukafanya mengi ndani ya miaka hata 20 tu na kuweza kupunguza kwa kasi kubwa umbali waliotuacha, kwani tutakuwa tunakimbia badala ya kujikokota ili kuwafikia.
   
 17. Companero

  Companero Platinum Member

  #17
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,474
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sijui siku hizi wanajisikiaje kuhusu hilo ndio maana nimeuliza ila zamani hivi ndivyo baadhi ya vinara wao walivyokuwa wanafikiri:

  The very image of an enlightened leader, Smuts opposed slavery and celebrated the 'principles of the French Revolution which had emancipated Europe,' but he opposed their application to Africa, for the African, he argued, was a 'a race so unique' that 'nothing could be worse for Africa than the application of a policy' that would 'de-Africanize the African and turn him into a beast of the field or into a pseudo-European.' - Citizen and Subject: Decentralized Despotism and the Legacy of Colonialism
   
 18. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #18
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  swali zuri sana,nilitaka kupost hii lakini umeniwahi,ngoja nikale boksi kesho ntakujibu
   
 19. m

  mpangwa1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 9, 2009
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 279
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  miafrika siyo mibunifu all the time copying from wazugu kwa hiyo wazugu anasikia proud unless we change our altitudes tunaendelea tu kuomba hela za ujenzi wa barabara zetu.
   
 20. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #20
  Oct 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  Hii chakula ya Raj Patel. Akiingia humu kuwapa vidonge vyenu mtaanza "kutoka nje ya mada" na kuanza kumwita mdosi.
   
Loading...