Makusudically
JF-Expert Member
- Feb 3, 2014
- 2,203
- 1,235
Nimelazimika kuuliza hili swali, baada ya Mh. Waziri mmoja baada ya kutenguliwa uteuzi wake, yeye alilazimisha kuongea na Wandishi wa habari kwa lengo La kuwaaga wale aliokuwa akiwaongoza, na alipozuiliwa alizua uongo kuwa eti katishiwa bastora, lakini tumefuatilia clips zote hatukuweza kuiona hivyo bastora wala mtu aliyedaiwa kumtishia bastora Mh. Waziri huyo. Historia inatukumbusha kuwa wapo mawaziri kadhaa waliowahi kutenguliwa uwaziri lakini hatukuwahi kuwaona wakiitisha wandishi wahabari kuwaaga au hata kutaka kuwaeleza au kutaka kuwashukuru, nisafari hii tu maajabu haya yamejitikeza, laba Katiba pendekezwa inavipengele vinavyoruhusu jambo hili, na Waheshimiwa mawaziri wameanza taratibu kulifanyia mazoezi. Prof.Muhongo hakuaga, Tibaijuka, Diallo, Kagasheki, Werema, Yona, Mramba, Kitwanga, n.k. Labda hawa hawakuwa na uelewa zaidi.