Hivi watumishi waliofukuzwa kazi hawawezi kusamehewa??

Fall Army Worm

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
19,332
14,255
Heshima zenu wakuu. Kama kichwa kinavyojieleza, leo ktk sherehe za uhuru mheshimiwa rais ametoa msamaha kwa wafungwa waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa lakini pia wafungwa wa makosa mengine.

Na kwa namna ya pekee akina babu seya na wanawe. Sasa kwa kuwa mheshimiwa kaonyesha moyo wa huruma na kwamba hata mungu anatusamehe madhambi yetu makubwa kabisa, basi nilikuwa ninamuomba mheshimiwa rais awafikirie hawa ndugu wa vyeti feki, si kwa maana ya kuwarudisha kazini, hapana, bali kwa kuwapa hata kifuta jasho kidogo maana walitumika ktk kulijenga taifa pamoja na vyeti vyao kuwa feki,

Wapo waliokuwa wauguzi baadhi yao wamenitibu hata mimi na nilipona kabisa, wapo waliokuwa katika fani nyingine km hizi za kuhudumia jamii, nao walifanya kazi kwa bidii kabisa tena bila kujibakiza. Hawa pia wangeweza kutazamwa kwa jicho la tatu. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom