Hivi watumishi wa serikali Bonus Yao ipo vipi?

MKATA KIU

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
2,350
2,000
Heshima kwenu wadau..

Tunashukuru mwaka unaelekea ukingoni tukiwa wazima wa afya na wengine ofisi zimeshafungwa hadi january, mambo ya holiday season kwenye ma kampuni ya kigeni..

So ni mwendo wa kushinda viti virefu tu, unaunguza Bonus uliyopewe na mwajiri huku unajiliwaza na maji ya mende kupunguza stress za mwaka mzima..

Sasa bwana nina rafiki yangu yupo serikalini daily analia njaa tu hadi december hii analia njaa tu, imebidi nimuulize hujapata hata ka Bonus kidogo ndugu, anasema hajapata zaidi ya mshahara..

Wadau hii ni kweli au jamaa ananipiga changa la macho ili nisimkope bali yeye tu ndio anikope mimi?

Cc wafanyakazi wa serikali nchi nzima wa jamii forums
 

Daddo

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
1,408
2,000
Serikali haijawahi kutenga fungu la bonus za wafanyakazi.
 

BALAKI

JF-Expert Member
Dec 28, 2012
371
0
Ukitaka bonus serikalin unajilipa mwenyewe, in terms of kitu kidogo ndo mana rushwa will stand forever
 

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
6,588
2,000
Haijawahi kutokea kwa serikali hii tangu izaliwe! Yenyewe ndo huhitaji sisi tuipatie bonus kwa kuikopesha hadi mishahara yetu na posho mbalimbali kama wafanyavyo walimu kwenda likizo kwa gharama zao na hata ukidai hulipwi.
Hili dubuana linaloitwa serikali ni dhulmati sana!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom