Hivi watumishi mnawezaje kuishi kwa kima cha chini cha 300k bila marupurupu yoyote kwa maisha ya sasa?

Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,512
2,000
Poleni sana watumishi, ni mwaka mwingine wa machungu tena kwenu..., nimeshangaa nilivokuja likizo nakutana na mtu analipwa 300k na ni mtumishi wa umma tena kwa mwezi, serious?

mnawezaje kuishi kwa mshahara wa 300k bila allowance nyingine yeyote kwa mwezi?, mnahudumiaje familia zenu, kulipa bill za nyumba, chakula na usafiri kwenda na kurudi makazini mnamudu vipi?.

huyu mke wangu namuachisha hii kazi ya ualimu mda si mrefu aisee

huu mshahara wa basic ya 300k mnawezaje kuishi huku kila siku mkitakiwa muwe kazini, mnajenga vipi au mpaka mstaafu? na mkiistaafu mnakutana na nssf na psssf mnachokutana nacho huko kwa taasisi hizi za mafao mnakijua wenyewe, kwa wale mlio ajiriwa na mnao tamani ajira kwa awamu hii jiandaeni kufa kwa msongo wa mawazo.
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
5,521
2,000
Wewe unaongelea laki tatu yote hiyo! Wakati kuna watumishi wengine wanapokea mpaka laki na 80 kwa mwezi! baada tu ya bodi ya mikopo kuongeza makato kutoka 8% hadi 15% ya basic salary huku wakiwa na mikopo kutoka kwenye mabenk na pia taasisi nyingine za kifedha!

Bora ukafungia tu hivyo vyeti vyako aisee! Miaka 4 sasa, hakuna madaraja kwa watumishi walio wengi, hakuna nyongeza ya mshahara, incriment haieleweki, nk. Hela zinajengea miundombinu na kununulia ndege.
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,228
2,000
Ukisoma ili uje kuwa tajiri kwa kulipwa mshahara mzuri basi bora usisome tu.

Kusoma ili uajiriwe na upate utajiri unajiumiza..!!!!!!!

Watu wanaishi na 150K wewe unasema laki tatu..?
Poleni sana watumishi, ni mwaka mwingine wa machungu tena kwenu..., nikiwa shamba napambana na hali yangu huku kijijini japo mazingira ya utafutaji na kilimo yamekuwa magumu nimejikuta nawahurumia watumishi wa serikali hii.

mnawezaje kuishi kwa mshahara wa 300k bila allowance nyingine yeyote kwa mwezi?, mnahudumiaje familia zenu, kulipa bill za nyumba, chakula na usafiri kwenda na kurudi makazini mnamudu vipi?.

binafsi kwenye mihangaiko yangu kuna mda huwa nakwama naenda kugongea daywaka ya bajaji, kwa mfano nikiichukua bajaji toka saa12 jioni mpka saa5 usiku nikirudisha natakiwa nipeleke na elfu15, hapo mimi nitakuwa nimetengeneza si chini ya 25k nitakayobaki nayo maisha yanaendelea kwa siku hiyo.

huu mshahara wa basic ya 300k mnawezaje kuishi huku kila siku mkitakiwa muwe kazini, mnajenga vipi au mpaka mstaafu? na mkiistaafu mnakutana na nssf na psssf mnachokutano nacho huko kwa taasisi hizi za mafao mnakijua wenyewe, kwa wale mlio ajiriwa na mnao tamani ajira kwa awamu hii jiandaeni kufa kwa msongo wa mawazo.

acha nifungie vyeti kabatini nipambane nijuavyo
 
Parabora

JF-Expert Member
Jul 6, 2019
1,512
2,000
Ukisoma ili uje kuwa tajiri kwa kulipwa mshahara mzuri basi bora usisome tu.

Kusoma ili uajiriwe na upate utajiri unajiumiza..!!!!!!!

Watu wanaishi na 150K wewe unasema laki tatu..?
kuna sehemu nimezungumzia utajiri mkuu?
 
tuusan

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
13,543
2,000
Poleni sana watumishi, ni mwaka mwingine wa machungu tena kwenu..., nikiwa shamba napambana na hali yangu huku kijijini japo mazingira ya utafutaji na kilimo yamekuwa magumu nimejikuta nawahurumia watumishi wa serikali hii.

mnawezaje kuishi kwa mshahara wa 300k bila allowance nyingine yeyote kwa mwezi?, mnahudumiaje familia zenu, kulipa bill za nyumba, chakula na usafiri kwenda na kurudi makazini mnamudu vipi?.

binafsi kwenye mihangaiko yangu kuna mda huwa nakwama naenda kugongea daywaka ya bajaji, kwa mfano nikiichukua bajaji toka saa12 jioni mpka saa5 usiku nikirudisha natakiwa nipeleke na elfu15, hapo mimi nitakuwa nimetengeneza si chini ya 25k nitakayobaki nayo maisha yanaendelea kwa siku hiyo.

huu mshahara wa basic ya 300k mnawezaje kuishi huku kila siku mkitakiwa muwe kazini, mnajenga vipi au mpaka mstaafu? na mkiistaafu mnakutana na nssf na psssf mnachokutana nacho huko kwa taasisi hizi za mafao mnakijua wenyewe, kwa wale mlio ajiriwa na mnao tamani ajira kwa awamu hii jiandaeni kufa kwa msongo wa mawazo.

acha nifungie vyeti kabatini nipambane nijuavyo
Mtumishi anaruhusiwa kufanya kazi zingine muda ambao sio wa kazini...
Laki tatu Ni ndogo kama hana kitu kingine anachokifanya!!
 
safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
7,228
2,000
Na ndo mleta mada kauliza wanaishije watumishi..?

Jawabu amelipata kwamba wanaishi,kuhusu pesa kutotosha hata huyo ambaye unatamani uwe kama yeye pesa hazimtoshi pia..
Kwa maisha ya sasa ukizubaa utakuwa umejifunga minyororo ya umaskini wa kutupwa nimejipa miaka mitatu ya kujitathimin ila ukweli ni kuwa ajirà zinatufanya tuweze kuishi tuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom